Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Nasubiri press conference ya ijipii, ila naomba asiseme kuwa walimteka bila kujulikana na wamemrudisha bila kujulikana.
 
Anayekulinda wewe na mali yako hata ukaweza kila mara kuandika humu JF ni nani? Au anayewalinda hao Mabwana zako, ambao kila kukicha hukimbilia kwenye vyombo vya habari kuilaumu Serikali, kama hufanyavyo humu JF, wakiwa huru na salama, ni nani?
Ni Mungu mwenye nguvu na mamlaka yote.
 
Tena watekaji wamepita hapo hapo kwenye ulinzi wakiwa na confidence kubwa
 
Sasa umekuja na theory nyingine .....!!
 
Sirro ndio kawatisha kuwaonyesha wapo kwa mstari na wamejua yao..

Hongera kwa jeshi la Polisi
Jana Sirro alikuwa shujaaa na kawaonyesha ni moto moto na wametikisika haswaaa na kumuachia.
Usisahau kuchukua toilet paper ukachambie mkuu.
 
Yote yatasemwa,ila Tumshukuru Mungu Mo kurudi salama.Maana haikua kitu cha mchezo kuingia kwenye mdomo wa mamba na kutoka salama.
 
Ukiona taifa linaamka na habari mbili-moja ya IGP anaonyesha gari likaelezwa ndilo lilitumika katika utekaji wa MO, na nyingine JPM anakula chakula cha mchana na wachezaji wa Taifa Star Ikulu na kuwapa milioni 50 mengine jaza mwenyewe!
 
Ndugu yangu hawa niwakuhurumia tu
hovyo kabisa
Wanatafuta Kiki hata kwa pikipiki hali ni tete
Kilaza anamfariji kilaza mwenzie
 
Wanyonge tumeungana tukapiga kelele tajiri kapatikana,ila hawa matajiri hawajawai kuungana hata kukemea lolote kwa umoja wao ili masikini apatikane.
Tumejifunza.
Unafikiri kapatikana Kwa sababu ya we mnyonge kupiga kelele? Kapatikana sababu ya Utajiri wake.Utajiri wake ndo umesababisha apatikane na wala sio kelele za Wanyonge
 
Anayekulinda wewe na mali yako hata ukaweza kila mara kuandika humu JF ni nani? Au anayewalinda hao Mabwana zako, ambao kila kukicha hukimbilia kwenye vyombo vya habari kuilaumu Serikali, kama hufanyavyo humu JF, wakiwa huru na salama, ni nani?
Hirizi
 
Mimi sina uenyeji na jiji la joto ebu nijulisheni hapo MO alipotupwa ni mbali na mjini au ni nje kidogo kama ni mjini means hawa watekaji wanazurura tu mjini daslaam mjini bila tatizo
Kama ni hapo Gymkana pale ni jirani kabisa na makao makuu ya jeshi la polisi na wizara ya mambo ya ndani. Yaani unavuka barabara tu
 
mkuu hii ransom.inanywa na mamraka halisi za inchinau mahalamia kama wale waliokuwa wakiteka meli za mafuta kule somalia? Kama mamlaka halali za nhi zinaingia huko basi hahitajiki kuwa tajiri.maana ukowa tajiri ni issue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…