Kwanza nitoe pole kwa familia na Mo kwa magumu mliyopitia na ambayo labda bado mnayapitia kwa Sasa na siku za usoni.
Pili nimshukuru Mwenyenzi Mungu atoaye uzima na ajuaye yale yatupasayo na kutupa njia ya kuvuka salama katika majaribu mbalimbali.
Tatu niwapongeze wale wote waliosimama kidete kuzungumza adharani kuhusu utekwaji wa MO jambo ambalo linatoa mwanga kwamba binadamu tunapaswa kuheshimiana na kutomdharau mtu kwani wakati wa shida marafiki wengi wasiowakweli ujitenga na kukaa pembeni nakurejea kukufariji wakati unapovuka viunzi.Natumai kupitia njia mbalimbali utatambua namna wengi wa waliokuwa wa karibu yako walivyokaa kimya na baada ya wewe kurejea naamini watakuja kukuona na kukufariji.Kaa nao kwa umakini na uishi nao kwa akili.
Napenda kukupongeza kwa moyo wako wa upendo uliokuwa nao na naamini unao, nasema moyo wa upendo kwa sababu waliolia na wewe si matajiri wala wanasiasa pekee bali maskini na wanyonge walilia kutetea uhai wako.
Baada ya hayo naomba kukupa ushauri huu wewe na familia yako...
FAMILIA ILITOA AHADI YA BILIONI MOJA KWA MTOA TAARIFA NA NAAMINI KWA MAZINGIRA YA UPATIKANAJI WAKO HAKUNA MTU ALIYELIPWA KIASI HICHO, HII NAAMINI NI SADAKA NA ITALIKOMBOA TAIFA LETU HUKO MBELENI ENDAPO TU ITATOLEWA KWA MAZINGIRA HAYA
1.Endapo utaitoa basi ipeleke kujenga nyumba za ibada aidha kanisa au msikiti, watakaoingia katika msikiti huo wataokolewa kiroho na nafsi zao kupona kutuepusha na binadamu wasio na hofu ya Mungu katika Taifa letu.
2.Endapo utaitoa kujenga chuo au shule basi tambua wapo wasomi watakaozalishwa katika vyuo hivyo na ambao kila watakapokumbuka kitendo ulichotendewa watapambana kwa nafasi zao kupiga vita watekaji na maharamia wa aina hii.
3.Endapo utaona yafaa pia waweza anzisha kituo maaalumu Cha kulelea watu wenye ulimavu, wasiojiweza na maskini nao watapata chakula, watalala, watapata huduma za kijamii na kupunguza vibaka na wavutabangi ambao ndio uzaa jamii ya utekaji.
4.Vinginevyo vyovyote uonavyo inafaa.
Natumaini utayasikia haya na kuona namna ya kuyatekeleza, tupo tayari kuunga mkono juhudi zako hata kwa kidogo tulichonacho.
Yawezekana huko ulikotoka wamechukua fedha nyingi kwako kuliko tunavyodhani, lakini ni bora ukatoa sadaka hi mbele za Mungu aliyekupa maarifa na utajiri ili akibariki upate zaidi na kuwaaibisha hao waliokunyanyasa kwa sababu tu wewe ni mbunifu na haukuzaliwa kuajiriwa balibkuqjiri.