Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

tundulisu kasema NISSAN NYEUPE no. ###'x mbona mpakaleo mmelala kwa Mo mmejua mpaka wazungu wanaongea kisouzi

Sasa ndiyo hicho kilichanifanya niseme wewe ni zuzu! Kwa kifupi unajikaanga kwa mafuta yako! Hoja yangu ni hii: Kama Lissu aliumizwa kiasi kile na akawa na ujasiri wa kuituhumu serikali (bila kujali tuhuma zake ni za kweli au la) ni nini kinachomfanya MO aogope kusema ukweli? Kulingana na maelezo ya awali ameishukuru serikali kwa kupatikana kwake. Kwanini ninyi mnang'ang'ania kuishutumu serikali?
 
Gymkana pale karibu na Ikulu, Gymkana karibu na Agakhan hospital. Gymkana pale karibu na Upanga Seaview. Kiujumla eneo lile ni very sensitive sana kwa mtu kufanya Ujinga. Yaani watekaji wanamteka mtu Oysterbay/Masaki wanatembea nae msasani yote, mpaka kawe na leo wanamrudisha mpaka Gymkana..

Halafu Mkuu mmoja anasema nchi iko salama, vipi kule Tandika, Mbagala, Manzese, Mtoni, Mbezi, Mbalizi, Tunduma, kyerwa, Tukuyu watakuwa salama kweli kama mtu anatekwa sensitive area halafu watekaje wanamrudisha sensitive area..Kichwa kinauma kwakweli.
Mkuu umejuaje walitembea nae huko msasani mpaka kawe?
 
Pongezi ni kwa jeshi la police Kwani kelele zake zimesaidia nini??Waliotekwa wote hakupiga kelele????? Na mbona bado hawajapatikana???? Nalipongeza kwa sababu MO amepatikana na binafsi niipongeze family ya MO kwa kutoa taarifa mapema Sana baada ya kijana wao kutekwa, yawezekana pia na hao wengine Kama taarifa zingetolewa mapema kungekuwa na nafasi kubwa ya kupatikana.mbinu ni hizi hizi kwanza zuia mipaka na Fanya upekuzi wa vyombo vyote vya usafiri majini na nchi kavu.
Kwa hiyo unalipongeza jeshi LA polisi kwa kumrudisha mo
 
Yaani eti waliomteka wamrudishe nyumbani wao wenyewe hawaogopi kudakwa na vijana wa Siro?, Au Mo katembea kwa miguu kutoka alipokuwa ametekwa, tena usiku wa manane mpaka nyumbani kwao?

Hahahah inachekesha sana hii tamthiliya ila ukifikiria inasikitisha sana!.

Ukiwa Gangster basi uwe angalau Smart!. Zero in papers translates Zero in missions!!
Yaan hawa majamaa ni mishamba kweli kweli halafu zero brain, hii staili waliyotumia kumteka mo ni ya kitoto sana
 
Sauti ya kamanda Mambosasa inatetemeka maana yake hajiamini kitu ambacho kinatia shaka sana kwa sababu Mambosasa ni muongeaji mzuri mbele ya kamera.
 
Nilikuwa sijawahi kulisikia na sikujua hilo eneo(Gymkhana) lilipo.

Baada ya kupata taarifa hizi nikaingia gopgle map kuona lililopo, nikabakia mdomo wazi....

Ilo eneo lina ulinzi na makachero wa kutosha 24/7... defender zao kila hatua... na TISS kutwa wapo wanatazama tuu... ukipanda juu kidogo unawakuta makilikili.... walimuteka wenyewe
 
Chadema wamechukizwa mno na kupatikana kwa Mo maana kiki yao imebuna.

Shida na Matatizo yanayoipata Tanzania ndiyo ufahari wa Chadema!
Na wewe kila siku chadema hata kama mada haihusu,kuwa makini wanaweza wasije kumalizia mahali.
 
Pole sana ila umeonyesha hauna ubinadamu, nilichojifunza kwako kumbe humu JF tunaweza kuwa tunajadiliana na watekaji wenyewe na wasiojulikana wenyewe.


Sina Ubinadamu kwa Muhindi, nina Ubinadamu watu wangu, wewe endelea na huo unaouita Ubinadamu wa upande mmoja na wa kujipendekeza kwa mtu asiyekuthamini.

Huyo Muhindi, Zito Kabwe, Lema &Co. wamecheza mchezo wa kujiteka, acheni kufanya watu mazuzu, maisha yatawaadhibu kama yalivyomuadhibu Tundu Lisu.
 
Wee bavicha, kwa taarifa yako Mo ni mwanachama wa ccm tena mwanachama hai. Na serikali ya ccm ndio ilikuwa bize kumtafuta huku chadema wakikesha kuomba asipatikane ili wapate kiki. Toka lini chadema ikamtakia mwanaccm mema?
Baada ya mo kupatikana ndio mnaanza kusema ni mwanaccm mwenzenu, Lumumba wenzako kina Barbarosa, ISIS, kina Elitwege walikuwa wakishangilia kutekwa kwake.

Kesho utaona polepole akiitisha press kumpa pole MO.
 
Braza siku hizi vipi tena , maana mada zako sizielewi elewi kabisa, nadhani ulio waandikia watajibu swali lako Braza
 
Nilikuwa sijawahi kulisikia na sikujua hilo eneo(Gymkhana) lilipo.

Baada ya kupata taarifa hizi nikaingia gopgle map kuona lililopo, nikabakia mdomo wazi....
Ni kweli mkuu eneo husika na ulinzi wa kutosha na askari wa patrol kila mara wanapita. Maswali magumu yanajibiwa na majibu mepesi sana
 
Back
Top Bottom