Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Kuna mambo yanastaajabisha sana. Huyu ni waziri anayepaswa kusimamia majukumu ya OR-TAMISEMI ambapo Majukumu ya OR-TAMISEMI yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Aprili 2016, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-
i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini;
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi; na
vii) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI
Katika majukumu yote hayo. Hakuna kipengele kinachoainisha kwamba waziri atahusika kusimamia na kutangaza chaguzi za serikali za mitaa.Jukumu hilo lilipaswa libaki na kuratibiwa na tume huru ya uchaguzi, Hususan ni uchaguzi unaohusisha vyama mbalimbali vya siasa, ambavyo waziri hana mandate navyo, isipokuwa Tume. Waziri anapaswa kuwa mtekelezaji pekee wa masuala ya utendaji wa serikali za mitaa. Majukumu ya Uchaguzi na masuala yote ya kuratibu uchaguzi yalipaswa kubaki mikononi mwa TUME HURU YA UCHAGUZI.
Inasikitisha sana.