Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Iyengamuliro,
Itapendeza tujadili mada iliyoko mezani.
Hayo majina unaweza kuelezwa na yeyote huko mitaani.
 
huo ni mtazamo wako pia: ila ulichokiweka hapa kwenye jukwaa umeweka mada mbili tofauti

ambazo ya kwanza ni tuhumu dhidi yako pili izo tuhuma umedhiingiza kwenye udini wakati tukiangalia tu. kwenye hoja zako hapo hakuna mahali ambapo utaushitak ukrt moja kwa moja kwa wametuma pilis juu ya kukamatwa kwako. ila unahis juu ya ukrst.



wee unajaribu kujitoa tu. kwenye hili ila ni kweli kabsa baasi yenu mnachuki binafsi juu ya ukirsto.
 
Kichengere,
Hapana neno khitilafu baina ya watu lazima ziwepo.
 
Leloo...
Nimesema kuwa nitakuwekeeni kidogo maana ni mkasa mrefu.
Sikutaka kuwachosha wasomaji wangu.

Ila ikiwa unataka kujua nini kiliendelea naweza nikakuwekea
kipande cha mwisho In Sha Allah.
Tuwekee sheik
 
wee kama ni mshitakiwa fwata sheria achana na maswala ya udini umekamatwa na polisi udini unatoka wap apo. afu ukitaka kuingia ndani zaid utakuta kati kati ya hawo polisi waisilm wapo.


Kichengere unaweza kutuambia kesi hii ilienda vipi ???


PADRI AKAMATWA KWA UJANGILI HUKU BUNDUKI 48, RISASI 764 ZIKIKAMATWA




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, akionyesha bunduki aina ya AK47 kati ya silaha zilizokamatwa katika msako maalum wa ujangili.

Na Daniel Mbega, Namanyere
PADRI wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga (jina linahifadhiwa) ni miongoni mwa watu 50 waliokamatwa kwa ujangili na Kikosi Kazi cha Taifa katika Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa.
Padri aliyekamatwa ni wa Parokia ya Kirando katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, ambaye bunduki yake aina ya Rifle yenye darubini inadaiwa kutumika katika ujangili ndani pori hilo la Lwafi wilayani humo.
Taarifa za kipolisi zimeeleza kwamba, mbali ya kukamatwa kwa watu hao, pia jeshi hilo limekamata bunduki 48 za aina mbalimbali ikiwemo ya Padri huyo anayoimiliki kihalali, pamoja na risasi 764 na maganda ya risasi 101.
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Jacob Mwaruanda amesema kuwa baadhi ya waliokamatwa silaha zao wanazimiliki kihalali lakini zinatumika kinyume na utaratibu wa kumilikishwa kwao.
"Watu hawa bado wanahojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Kamanda Mwaruanda.
Kamanda Mwaruanda alisema kati ya bunduki 48 imo moja ya kivita aina ya AK47, bunduki 8 aina ya Rifle na risasi zake 83, Shortgun 19 na risasi zake 138, bastola 5 na risasi zake 133, magobore 15, magazine nne za bunduki aina ya Sub-Machine Gun, maganda matano ya bunduki aina ya Rifle, maganda 96 ya risasi za bunduki ya shortgun pamoja na vifaa vya kutengenezea bunduki za kienyeji na mitutu sita.
Watuhumiwa hao walikamatwa pia na nyara za serikali ambazo ni mikia sita ya tembo, nyama ya nyati kilo 20, miba ya nungunungu, ngozi moja ya paka-pori na pembe ya Nshya.

Kamanda Mwaruanda akifafanua jambo huku nyuma yake wanaonekana maofisa wa Kikosi Kazi cha Taifa pamoja na askari wa wanyamapori.

Kama Mwaruanda alitoa muda wa mwezi mmoja kuanzia sasa kwamba watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha mara moja kwenye vituo vya polisi au ofisi za serikali za vijiji kabla operesheni kabambe ya kuwatafuta watu hao haijaanza.
Rukwa na Katavi ni miongoni mwa maeneo ambayo ujangili kuua tembo umeshamiri sana hasa katika mapori ya akiba ya Lwafi na Hifadhi ya Taifa ya Katavi kutokana meno ya tembo kuonekana kuwa na soko katika mikoa mingine nchini na nchi jirani.

Kamanda Mwaruanda akionyesha kigudulia ambacho hutumiwa na majangili kubebea risasi.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Davies Mushi alinukuliwa hivi karibuni kuwa kuwepo kwa soko zuri la biashara haramu ya nyara za Serikali hususan meno ya tembo ni moja ya sababu zinazochangia ongezeko la ujangili katika hifadhi hizo.
"Soko zuri la meno ya tembo lililopo katika mji wa Mpanda (Katavi), Sumbawanga (Rukwa), Tabora na maeneo mengine ya nchi linachangia sana kushamiri kwa ujangili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, lakini tunajitahidi kufanya doria ndani ya hifadhi na kukabiliana na kasi hii iliyopo ya kuua tembo inayofanywa na majangili ambao wengi wao ni kutoka nje ya nchi," alisema Mushi.
 
NDUGU ULISHAWAI SIKIA KUWA VATICAN KUNAPATIKANA MADAWA YA KULEVYA? LAZIMA SERIKALI IFANYE KAZI YAKE MAMBO YA UDINI HAYO NI YA KWAKO TIHI SHERIA BILA SHURUTI,VINGINEVYO UTANYOOKA TU."HAPA KAZI TU".
 
Kankiza,
Unafanya haraka ya kujibu tena kifedhuli wakati somo lenyewe hujalifahamu.

Tatizo si kuwa mimi nauza madawa ya kulevya na hapa ndipo kwenye kichekesho chenyewe.

Tatizo lilianza kwenye mkutano kuhusu ugaidi uliofanyika Chuo Kikuu Cha Ibadan
2006 na mimi nilikuwa mmoja wa watoa mada.

Hebu jitulize usome kisa kizima kisha ndiyo urejee hapa jamvini kuchangia.
 
Dadanguri kuna mmoja mfano wa huyu nilimwambia akawaulize wakubwa zake kuhusu Banco Ambrossiano
...hajarejea...
 
Huyu Mzee ni mdini sana
Wa kusoma,
Hapana mimi si mdini.

Soma Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).
Wadini wote wameelezwa humo na vitimbi vyao vyote.

Wewe ni mgeni na mimi na ni mgeni hapa jamvini.
Wenzako wote niliowapa hizo rejea baada ya kuzisoma
walipata mshtuko mkubwa.

Hawajarudi tena hapa jamvini.
Wameamua kukaa kimya.

Mimi nilinyanyua kalamu takriban miaka zaid ya 30 iliyopita
baada ya kuona kuwa kuna kitu katika jamii yetu hakijakaa
sawasawa.

Haukuwa udini ulionisukuma kufanya utafiti ule na kuandika
kitabu.

Kilichonisukuma kilikuwa ni kutafuta haki na ukweli.
 
Nimeogopa sana kwa namna ukivyonijibu kistaarabu,
Hongera sana Mzee kwa hilo.

Lkn ni kwa nini katika maandiko yote huachi kusema waislam wanaonewa Tz?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…