Princemwalejr
JF-Expert Member
- Nov 9, 2017
- 496
- 489
Prince...nimekueleza lazima kwanza ufahamu kwa nini iliundwa BAKWATA ndipo utakuwa katika hali ya kufanya mjadala wa maana.
Ikiwa hujui jana yako kamwe hutoijua leo yako.
Historia ni mwalimu mzuri wa kufundisha na kukuelewesha kwa nini leo uko hivi ulivyo.
Ingekuwa bora ukaachana na ulalamishi ukafanya ya muhimu kwa sasa kusaidia hao unaona wanaonewa. Wanachohitaji ni elimu. Elimu ndiyo inayowafanya wawe wachache katika nyadhifa za juu. Tunazungumzia watu wanaogomea sensa ya taifa. Watu wanaogomea kuchukua vitambulisho vya taifa. Na wanakatazwa na mashehe wasio na elimu ya shule. Watu ambao wakiwa masikini wanaamini Mungu kawapangia wawe masikini.
Mtikila alikuwa anakamatwa. Gwajima kalala central. Ingekuwa Gwajima ni shehe ungesema waislamu wanaonewa. Halafu unatoa mifano ya kusadikika. Mapdri hawatakaa wafanye mikutano ya vurugu iliyofanywa na mashehe wa Zanzibar. Na wakifanya hivyo na wao watakamatwa.