Hivi maana ya "mdini" ni nini?
Maalim Faiza,
Nakuwekea hapa kisa kilichotokea Bukoba na Kigoma mwaka wa 1963 katika uchaguzi wa serikali za mitaa huenda labda likasaidia kujibu swali lako:
''Tarehe 11 Machi, 1963, Kamati Kuu ya TANU iliyokutana Dar es Salaam ilipiga kura kuvunja kamati ya wajumbe kumi na moja ya Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake
Idd Tulio. Wazee walikusanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na wakasomewa uamuzi wa Kamati Kuu ya kulivunja Baraza la Wazee.
Taarifa ilisema wazee hao ni kero kwa sababu ''dini na siasa vilikuwa vitu viwili tofauti na hawa wazee walikuwa wanachanganya dini na siasa.'' [1] Hiki kilikuwa chombo cha ushauri ambacho wajumbe wake wote walikuwa Waislam; chombo kilichokuwa ndani ya TANU ambacho kilimuunga mkono
Nyerere na TANU tangu siku za mwanzo kabisa, kwanza chini ya uongozi wa
Sheikh Suleiman Takadir na kisha chini ya
Idd Tulio baada ya kufukuzwa kwa
Sheikh Takadir kutoka TANU.
Wakati haya yote yakitendeka Kanisa ambalo wakati wa kudai uhuru lilijiweka mbali na halikutoa msaada wowote sasa likawa linanyemelea kujiingiza katika siasa likiwa na agenda yake: kuwaweka viongozi Wakristo katika nafasi za uongozi na kuutoa nje ya uongozi Waislam ambao Kanisa liliwaona hawana elimu.[1]
Jumuiya za Kiislam kama Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na EAMWS zilikuwa sasa zinapigwa vita na serikali ya
Nyerere kama vyombo ambavyo havikuwa na umuhimu wowote katika Tanganyika mpya. Katika kumuhakikishia utiifu wao juu yake, Waislam walijitahidi mwisho wa uwezo wao kuziweka taasisi zao kando na chuki za kidini dhidi ya Wakristo.
[1] Juhudi hizi hazikuthaminiwa. Serikali ilifanya juhudi za siri kuhakikisha kuwa jumuiya zote za Waislam zinapigwa marufuku. [1]
Huu ndiyo ukawa mwanzo wa kampeni za kufuta historia ya Uislam katika TANU na mwisho wa Waislam kuwa na sauti katika siasa baada ya uhuru kupatikana. Baada ya kupatikana kwa uhuru, ile nguvu ya Waislam iliyotumika kupambana na Waingereza kuleta uhuru, ikaonekana haina maana yoyote na haifai kitu tena.
Kuvunjwa kwa Baraza la Wazee ndiyo ilikuwa kishiko cha mwisho cha Waislam katika TANU. Baada ya hapo Kanisa lililokuwa pembeni wakati wa kudai uhuru sasa likajitokeza waziwazi kuwapiga vita Waislam katika TANU. Katika kitendo ambacho Kanisa halikupata kufanya, Kanisa Katoliki Bukoba liliteua wagombea wake wenyewe wapambane wa wagombea Waislam walioteuliwa na TANU kugombea nafasi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kanisa lilisema limeweka wagombea wake binafsi kwa kuwa wana elimu kupita wagombea wa TANU Waislam. Kampeni kama hii ilifanyika vilevile Kigoma. Hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kuwa
Nyerere, serikali au TANU yenyewe ilichukua hatua zozote dhidi ya Kanisa kwa kuchanganya ''dini na siasa.''
(Haya ni kutoka katika kitabu cha
Sykes)
Ikiwa wana jamvi mtapenda naweza kukuwekeeni hapa historia ya harakati za kudai
uhuru Bukoba muone vipi ghafla mambo yalibadilika baada ya uhuru 1961.