Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere


Tena huyu ni gaidi hatari kabisa, fikiria akiwa na waislamu wenzake wako na faraga atawafunza nini zaidi ya chuki na kuwatusha ?
 

Nipipo soma kuona neno Tehran, wazo la kwanza ni madawa , baadae nikaja gundua lengo ni udini. Hebu tafakari ,kuna nafasi ngapi kw amsafiri kutoka Vetican akabeba madawa ,ikiwa n amaana ya kwamba kusafirisha kutoka Europe kuja Africa? na kuna na fasi ngapi ya madawa kusafirishwa toka Iran kuja Tanzania? Walikua sahihi kabisa kukushuku ila kilicho kusumbua ni udini wako.
 
Mtoto...
Unanituhumu kwa udini na nadhani tuhuma hii ni kwa sababu mimi nimeweza
kuthubutu kuuliza mengi ambayo wengine walishindwa.

Kubwa ambalo wengi limewachoma ni kule mimi kuandika kitabu cha Abdul
Sykes
na kupitia kitabu kile nikaweza kueleza historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika.

Kwa mara ya kwanza historia ya kweli ya uhuru ikajulikana na majina yale
ambayo kwa miaka yalikuwa hayamo katika historia hii yakajitokeza.

Ikiwa wewe unaona huu ni udini basi hii ni bahati mbaya kwako.

Tuje kwenye mimi kukamatwa uwanja wa ndege kwa kushukiwa kuwa ni
muuza unga.

Tatizo halikuwa unga tatizo langu lilianza Chuo Kikuu Cha Ibadan, Nigeria mwaka
wa 2006.

Nilialikwa kwenye mkutano kuhusu ugaidi na nilitoka mada ambayo iliwakera
Marekani ambao walikuwa waandaaji wa mkutano ule wakishirikiana na Iran na
Chuo Kikuu Cha Ibadan.

Maneno yaliyowachoma ni mimi kueleza historia ya taifa lile katika mauaji mengi
duniani kwa njia za dhulma.

Nikaeleza pia Sheria ya Ugaidi iliyopitishwa Tanzania mwaka wa 2002 na kwa hakika
niliichambua na kueleza athari yake kwa Waislam wa Tanzania na nikatoa mifano ya
vipi Waislam ambao wanajishughulisha na maendeleo ya umma wa Kiislam kwa
miaka mingi walivyokamatwa na kuwekwa mahabusi baada ya kupitishwa sheria hiyo.

(In Shaa Allah nitaiweka hiyo paper mwisho ili uisome na uelewe kile nnilichosema).

Wakati naeleza haya Wamarekani ambao walikuwa na timu kubwa katika mkutano ule
walikuwa wanachukua, ''notes,'' na video.

Mmoja wa waliokuwapo katika mkutano ule alikuwa mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania
kutoka Lagos.

Nilirudi Dar es Salaam salama na nikasahau.

Mwaka unaofuatia yaani 2007 nilialikwa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran
kwenye Hawli ya Imam Khomeni.

Iran ilialika watu dunia nzima na mkutano ulikuwa mkubwa.

Tanzania walialikwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na waandishi wa habari kutoka
''electronic'' na ''print media,'' yaani magazeti na televisheni.

Ilikuwa nilipofika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ndipo nilipokamatwa kwa
kushukiwa kusafirisha mihadarati.

Nilifanyiwa mahojiano na vyombo vya usalama na nikafanyiwa upekuzi wa mizigo yangu
lakini hapakuwa na chochote.

Wakati mwingine maswali yao yalikuwa ya kuchekesha.

Waliniuliza kwa nini ninaingiza vitabu vya Khomeni Tanzania na mimi nikawa nawajibu
kwa kuwauliza kuwa kwani hauruhusiwi?

Waliniuliza imekuwaje nimefahamika na Iran kiasi cha mimi kualikwa huko.

Nami nikawapa orodha ya nchi ambazo nimealikwa na nimezungumza katika vyuo vyao
na nikawaeleza kuwa hata mimi sifahamu wananijua vipi ila huwa napata mialiko tu na
mimi sijaona haja ya kuwauliza wamenijuaje.

Waliniweka pale uwanja wa ndege hadi asubuhi na wakanieleza kuwa hawawezi kuniachia
hadi wapate maelekezo kutoka juu.

Asubuhi wakaniachia na wakanitaka radhi wakisema kuwa kumekuwa na makosa kwa upande
wao na wakajitolea kunipa usafiri kunipeleka nyumbani kwangu.

Niliwashukuru na nikawaambia kuwa nitachukua taxi.

Kitu kilichonifurahisha ni pale nilipoona wahojaji wangu wakinibebea mizigo yangu hadi nje
ya uwanja huku wakizungumza na mimi kwa adabu na bashasha na kuniambia kuwa ninapopita
hapo nikiwa nasafiri nisikose kuwapitia ofisini kwao kuwasalimu.

Ukweli ni kuwa ile yote ya mie kukamatwa haikuwa katika madawa ya kulevya bali ilitokana
na ile mada ambayo niliwasilisha Chuo Kikuu Cha Ibadan.

Wamarekani hawakupendezewa na yale niliyosema na kwa hivyo walileta taarifa hapa nyumbani
kuhusu mimi.

Haikuishia hapo.

Mimi bila kujua pasi yangu ikawekewa alama ambayo haionekani kwa macho ila inasomeka katika
''computer,'' za Uhamiaji.

Ikawa sasa kila ninaposafiri inajulikana nakwenda wapi na kwa shughuli ipi na nikiwa ''transit,''
napekuliwa kwa uangalifu zaidi.

Nafuatiliwa wapi nimefikia, ''transactions'' za ATM wakati napokea fedha kutoka nje ya nchi na pia
ninapokuwa safarini.

Huchukua zaidi ya siku moja kwa mimi kupokea fedha Western Union jambo ambalo
kwa kawaida ni kazi ya dakika chache.

Kadi yangu ya ATM ilikataa kutoa fedha New York kwa kweli ni hali si nzuri sana.

Nimepata kutolewa katika foleni ya kuingia katika ndege Schipol Airport Amterdam nikielekea
Marekani.

Usumbufu ni mwingi.
Nakuwekea hapo chini paper niliyowasilisha Chuo Kikuu Cha Ibadan ambato ilisababisha haya yote:
Mohamed Said: ISLAM, TERRORISM AND AFRICAN DEVELOPMENT



Tehran, Iran nikiwa katika Ukumbi wa Mkutano
 
Tena huyu ni gaidi hatari kabisa, fikiria akiwa na waislamu wenzake wako na faraga atawafunza nini zaidi ya chuki na kuwatusha ?
Mtoto...
Hakuna Muislam yeyote Tanzania ambae kashitakiwa kwa kosa la ugaidi
na kutiwa hatiani toka sheria ya ugaidi kupitishwa 2002.

Ingekuwa mimi ni gaidi ningeshakamatwa.
 
Mzee Mohammed Said ni mwanahistoria mzuri sana, lakini ungejinafasi kama Mtanzania na si kama mwislamu usingekuwa mjinga kiasi hiki.

Mimi siku zote najihesabu kama Mtanzania na si kama mkristo, usidhani ni wewe peke yako unayesafiri au unakutana na adha hizi.

Sikiliza upande wa sisi wakristo wa majina kwenye passport zetu shida tunazokutana nazo.

Mwaka 1997 nilikuwa naingia South Africa kupitia Border ya Beit brigde, alfajiri ya saa 11 baada tu ya border kufunguliwa tulianza kupita immigration hakukuwa na shida niligongewa entry tena wakati huwa tukitumia Viza, nikapita custom nikawaambia sina mzigo wa kudeclare, kivumbi sehemu ya mwisho ya police check hapo ndipo walipoona passport yangu ya Tanzania mimi peke yangu nikapelekwa kwenye chumba cha upekuzi na kuanza kupekuliwa.

Kwakuwa mimi siyo punda wala mzungu wa unga hawakunikuta na kitu wakaniambia sorry wakaniachia lakini ukumbuke hapo nimeshapoteza muda mwingi na kama ningekuwa nimetoka na basi Lusaka au Harare to Johannesburg maana yake lile basi lingeniacha lakini uzuri mimi nilitoka Harare na usafiri mwisho border.

Ok, kisanga cha pili nilikutana nacho hapo JK Nyerere Airport nilikuwa nikitokea Nice France kupitia Zurich, nilifika Airport Dar saa 1 na dakika 50 usiku lakini amini usiamini kunda ndege tatu zilishusha abiria na abiria wote wametoka mimi bado w nimekomaliwa mule na watu wa uhamiaji na nipo home ground, watu wa usalama wamesachi mizigo yangu wametimuwatimuwa na hawakurudisha kama nilivyokuwa nimeipanga.

Pamoja na mikasa hii yote sijawahi kuihusisha dini na mikasa hii, ule mkasa wa Beit bridge tatizo lilikuwa ni Utanzania wangu na hiki kisi kilichonitokea home ground tatizo ni roho mbaya tu za waswahili hakuna kingine.

Nakumbuka kuna rafiki yangu Mwingereza tulikuwa tukifanyakazi pamoja Cardiff UK siku moja tukiwa njiani akiendesha gari kwenye maongezi na story nyingi aliniambia kitu ambacho mimi nakiamini mpaka kesho, aliniambia black is problem.

Sasa wewe mzee usipobadili mindset yako na kuanza kujihesabu kiutanzania wako na si kiuislamu wako basi utakuwa una ulemavu wa maisha.

Wasomali ni waislamu watupu lakini hawaeleni, na msivyo na aibu mtawasingizia Makafir ndio wanawagombanisha, basi hapa tukubaliane wazi kwamba waislamu ndio jamii ya watu wapuuzi zaidi kuwahi kutokea huku duniani.

Ukienda Uarabuni ni vita ya waislamu Sunni na Shia sasa huko nako kuna mfumo kristo?
 
Matola mimi na wewe ni watu wawili tofauti kwa kila kitu.

Kwangu mimi Uislamu wangu ni kila kitu na wala sioni aibu.

Mimi ni Mohamed Said Salum Abdallah...

Wako waloficha majina yao mimi sijapatapo kufanya hivyo.

Ikiwa kwako huu ni ujinga mimi ni radhi kuwa mjinga.

Mimi si mlemavu ni mzima Alhamdulillah na katika jamii yangu naheshimika sana.

Hayo mengine ya Wasomali si katika hoja tunazojadili hapa hivyo sina la kusema na hizo lugha za matusi "wapuuzi" nk. nimezizoea na nina uwezo wa kuzistahamilia.
 
Tumesikia mengi kuhusu ugaidi wa maaskofu ,na ugaidi mkubwa ambao ni bora hata kujilupua NI KUVILAWITI VITOTO VYA KIUME VISIVYO NA HATIA naichukia vatican hii ni kashifa ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara yaani ni katabia pendwa cha maaskofu shame on u
 
Kwa kweli serikali yetu ni mtihani sana. Naomba siku moja mungu alete uhuru uliyo wa haki mana hakuna haki. Udini umekuwa ndio kigezo kibubwa tz.
 
Inshaallah Allah akuepushe na fitina. Uisalamu nikusema kwl hata ukichukiwa Allah atakulinda inshallah.
 
ogopa halama hzi * alafu #
kwa nini * ina simama mfano:umejaribu kutafuta jamii ikuelewe kwa mda mrefu.
# ina simama mfano:kutokana na jamii kuto kuelewa umbaki kwa nini mimi.
zama iliyo kwa ndugu zetu waislamu wana # inayo wasumbua kuona kila jambo wao wanakandamizwa kutokana na wakristo.
mfano:mkoloni mwarabu alipo kuja hapa hakuja kwa misingi ya kufungua shure ndo maana shule zote tanganyika ni mishionari na wakoloni wajerumani na waingereza.kikubwa zaidi mwarabu tunacho shukuru kueneza dini na biashara zake.zama iliyo jengwa na mwarabu ndiyo ilipelekea hata babu zetu wanatuambia kipndi icho shule za kikoloni ndizo zilikuwa zimeletwa na wamisionari na wajerumani,wingereza wao waliona kuwa zimekuja kuwabadilisha dini na kuzuia watoto kusoma .ndo maana miaka ya nyuma na kidogo unakuta wasomi ni wengi wakristo si kwa udini kama nilivo toka kukuelezea nyuma hapo.
sitaki kufikia dini yoyote kwa lengo la kuchafua.# hii ndiyo iliyobaki kwa waislamu wengi kuona kama walionewa na kupandikiza chuki kwa watu wengi,na hata ukienda kwenye miazara mingi,# ndiyo inapandikizwa sana.
ni jukumu la waislamu kuelewa wapi palipo fanya kuonekana #.ndio maana unaona waislamu wengi nao wanajikita kwenye elimu siyo kama hile historia kwa ufupi niliyo kuwa nayo tu.
wote wamoja tujue nchi yetu si kutengana kwa rangi.
 
Kiukweli mi kwenye suala la dini sipendi kuchangia sana kwa sababu kila mtu atazungumzia dini yake na wengine kuponda dini ya mwenzake.

Ila napenda kuwa muwazi kuwa marekani haipendi kabisa dini ya kiislam kwa sababu zao na inataka sana support ya nchi nyingi.

Vile vile waislam na waarab hawawapendi wamarekani kwa sababu ya kutengwa na kushutumiwa hasa katika misimamo yao ya kidini.

Mi nadhani chimbuko la uhasama huu ni kwa sababu mmarekani anataka kutawala dunia, kujiweka kuwa yeye ni polisi wa dunia, kukandamiza nchi za kiarabu ili ziwe chini yake na kuweza ku-explore vizuri mafuta.

Na kwa kuwa mafuta ndo yanaifanya nchi za kiarabu kuwa na maendeleo, hata hela yake kuwa juu zaidi ya dollar, basi hapo ndo vita ya biashara,kiuchumi na kimaendeleo huanzia hapo na ndo chanzo cha nchi za kiarabu kuwekewa masharti na marekani au kushambuliwa ili zisinyanyuke kuizidi marekani na ndo vita vya mara kwa mara na kunyang'anywa mafuta na kudhoofishwa.

Ila kwa kuwa jamii ya kiislam huwa na hasira za haraka na kuwa aggressive ukizungumzia dini au jambo lolote la dini, na hata wao kwa wao kugombana kisa kushutumiana jambo pasipo kufanyia research au kuwa na subira, hapo ndo marekani anapochezea karata yake na bila ajizi marekani anafanikiwa sana kwa hilo. Kumbuka kuwa vita vyote hivi tunavyoshuhudia, basi niliyoyaeleza hapo juu tactic hyo hutumika.

Pia ikumbukwe kuwa marekani nayo hutumia kufunika history ya viongozi wa kiislam, basi hapo ndo utashangaa kuona wasomi wa kiislam nao hawataki historia hizo zipotezwe na sababu hiyo ndo ndugu yangu hapa mohamed said anaitetea sana kila sehemu.

Nahitimisha kwa kusema kuwa nawaasa ndugu zangu waislam, historia iliyopita haina nafasi katika ulimwengu huu wa science na technology. Hebu fanyeni km libya, ambapo kiongozi wao alietolewa madarakani, hakuangalia na kukazania historia bali aliweza kujenga shule nyingi, kusomesha wananchi wake wengi na hivyo watu hao kuishi vizuri,kuendeleza nchi, huku wakiwa wamesoma.

Ningependa tushindane kuhusu dini zetu kwa maendeleo. Wakristo waliachiwa sana properties nyingi na wamisionari kama vile nyumba, shule, makanisa, mahospital na vitega uchumi kibao.

Tuachane na mashindano ya kusaka historia maana kipindi hiki ni cha technolojia, anzisheni shule nyingi, vitega uchumi vingi, shule nyingi, somesheni watoto wenu wengi sana, mjenge na sehemu nyingi sana za ibada. Changisheni hata hela sehemu za ibada kama wakristo ili mshindane kwa maendeleo na si kwa historia huku elimu mkiwa nyuma sana.

Na mtaeleweka na mtaonekana kuwa mna busara, kuliko baadhi yenu kushika bunduki, kujitoa mhanga, mabishano ya siasa na mengineyo yasiyo na tija.

Ila hongera mkuu kwa kazi nzuri unayoifanya japokuwa marekani walikutafsiri kivingine. Suala la kila siku kuwa na negative thinking kuwa mnaonewa, toeni vichwani mwenu maana mtashindwa kupata maendeleo wakati wengine wakiendelea kuwazidi, najua kwa hilo mtaendelea na kuwazidi hata wazungu.
 
Safi sna
 
Hufahamu kitu kwa sababu hayajakukuta,kitanda usicholalia huwezi jua kunguni wake!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…