Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Kimsingi siku nikija kua rais wa nchi hii,lazima wananchi wangu wawe na majina matatu.majina yakua kama ifuatavyo

1.Jina la kikiristu
2.jina la kiislam
3.Jina la kiinyeji (siyo jina la kikabila wala mila ila litakua kama mti,kijiji,wilaya,mlima,mto au ziwa wa eneo ulipozaliwa
au wazazi wako walikozaliwa )

Nb,jina la mwanzo linaweza kuanza la kikiristu au kiislam ila la mwishi lazima liwe la kiinyeji.

Mfano,mtu kazaliwa Ngorongoro

Huyu ataitwa.

Hussein Thomas Ngorongoro

Mtu amezaliwa mlima kitonga

Donald khalid Kitonga

Mtu amezaliwa chato

Abdul John Chato

Kwa mtazamo wangu tunaweza kupunguza japo mtazamo hasi iliopo wa kiimani kwa kufanya hivo.
Na wewe umeamini kama Mohamed Said alipekuliwa kwasababu ya uislamu wake? Msome mwanzoni pale, anasema eti "wakati huo mambo ya ugaidi yalikua yamepamba moto" Sasa swali, je kwanini alijiwazia yeye kua ni gaidi? Something is wrong with this mzee!
Kwenye ile list ya Makonda, hivi ni Waislam tu ndio waliotajwa? Mtu aliyefirisika (kisiasa) hua anatafuta uhalali kwa either udini au ukabila, alisema Nyerere.
 
  • Thanks
Reactions: 365
Si hivo my Dada Kwa tz waislamu ndo wanaongoza kiuchumi na masuala yote ya biashara na uwekezaji fanya sensa angalia asilimia kubwa ya malori,daladala, mabasi,taxi soma ubavuni wamiliki wao 80% ni waislamu, anza viwanda vya dar Pugu road, Mandela,kilwa road,bagamoyo road, ingia maghorofa ya kkoo,nk nenda madukani,magengeni,nk asilimia 85 ni waislamu, ttzo nn sasa,waislamu wa tza wanashida moja hawapendani,ni wabinafsi,hawachangii masuala ya maendeleo yao mfano tu ni nadra sana kukuta hata kwenye michango mfano harambee za Ujenzi wa shule,misikiti,nk kukuta tajiri kajitolea zaid km ilivo Kwa upande wa dini zingine mfno ukistro,uhindu,nk ambapo wao ufanya harambee za michango ya kufa MTU unakuta MTU mmoja tu tena wa chini utoa na kutimiza ahadi ya kitu kikubwa,michango yao tu inaendesha tasisi zao bila kutegemea msaada nk,tofauti na waislamu ni wazito sana kuchangia manufaa yao zaid ya vile vifurahishavo macho mfano mashindano ya michezo,burudani nk.Tatizo haliko mfumo Kristo wala msikalie historia ndo vitu viwafanyavo mbaki nyuma japo mnanguvu kubwa kiuchumi anyway labda ni mipango ya Mungu kuleta mizania ya ubalance, wakristo kiuchumi ni wachache zaid kwenye nafasi za kitaaluma wanaonekana wana nguvu sababu ya Upendo na umoja wao.Cha msingi kitakiwacho muondoe dhana ya kujiona muu duni kitu ambacho akipo ni dhania tu hakuna abaguliwae nchini Kwa kunyimwa fursa kulingana na kuweza kwake,pia muondoe ubinafsi faidikeni nyote ki manufaa yenu na sote, futeni historia na dhana mfumo Christo ambayo ni dhana ya inferiority complex zaid kuliko hali halisi ni sawa na ukishaweka dhana ya kubaguliwa ukienda nchi za weupe kila wakufanyia wahisi unabaguliwa kumbe ni hisia tu.Wekezeni zaid kwenye elimu zote,harambee nk,ondoeni chuki za kuwabagua wengine wasio wa imani yenu kwenye shughuli zenu nk maana kuna kazi upewi kwenye maduka,viwanda,hotel,magari,biashara nk km wwe unatokea imani nyingine. Nakaribisha Hoja.

Hebu andika kwa vituo na para, nimeshindwa kukuelewa kabisa.
 
pole sana...ndugu...kwakweli Tanzania imekuwa si nchi salama kwa watu wenye uelewa mpana kuishi..na mbaya zaidi ukiwa na uelewa mpana ukajaribu kuwaelewesha...unakuwa umejiponza...mbinu zozote zitatumika kukuzima...
 
Na wewe umeamini kama Mohamed Said alipekuliwa kwasababu ya uislamu wake? Msome mwanzoni pale, anasema eti "wakati huo mambo ya ugaidi yalikua yamepamba moto" Sasa swali, je kwanini alijiwazia yeye kua ni gaidi? Something is wrong with this mzee!
Kwenye ile list ya Makonda, hivi ni Waislam tu ndio waliotajwa? Mtu aliyefirisika (kisiasa) hua anatafuta uhalali kwa either udini au ukabila, alisema Nyerere.

= aliyefilisika

Hivi hizo shule mliemda kusomea ujinga?
 
Ha ha ha ha ha!
Mkuu, Mh Zungu, umefanya tukio kubwa, (kwa ref. zako) nadhani hata halilingani na kile tunachojadili, basi mi nikushukuru tu, na zaidi ni kwamba naishi kwa hofu juu ya u dini, na ninadhani kama kuna hatari kubwa nchi hii ni hiyo, ila mtazami wangu siyo sheria, nakushukuru kwa hayo!
Safari Safi,
Udini ndilo tatizo kubwa tulilokuwanalo Tanzania.
Ikiwa hujasoma kitabu cha Sykes fanya ukisome.

Ukimallza msome P van Bergen (1981), Sivalon
(1992) na Njozi (2002).
 
Pole kwa huo mkasa Mohammed Said.

Nilichojifunza kwenye hio safari,maofisa usalama wa Tanzania wako sensitive sana na shughuli za waislam kuliko issue za madawa ya kulevya,sababu kama walimaanisha leo hii madawa ya kulevya yasingekuwa habari ya mjini
Polite,
Ahsante sana.
 
= aliyefilisika

Hivi hizo shule mliemda kusomea ujinga?
MAma/dada yangu hua nakuheshimu sana, mara nyingi ukikosaga cha kusema hua unakimbilia kwenye usahihi wa neon hata kama unakua umeelewa. Still bado mi nakupendaga bure tu mama/dada yangu.
 
MAma/dada yangu hua nakuheshimu sana, mara nyingi ukikosaga cha kusema hua unakimbilia kwenye usahihi wa neon hata kama unakua umeelewa. Still bado mi nakupendaga bure tu mama/dada yangu.

= huwa
= huwa
= neno
= nakupenda

Huwa nimeelewa ndiyo nnakusahihisha nisichokielewa ntakisahihisha vipi? Fikiri.
 
John,
Hapana mimi naeleza kama ninavyokua kutokana na uzoefu.

Naamini kabisa kuwa wasingeweza kumfanyia mtu aliyetokea
Vatican haya waliyonifanyia mie.

Juu ya haya sikukatazi kuwa na fikra tofauti.

Kwa akili ya kawaida tu kati ya mtu anayetokea nchi yenye ebola na anayetokea nchi yenye malaria nani atawekwa quarantine kwanza? Huo utakuwa ubaguzi?
Nina mashaka sana na uwezo wako wa kufikiri kama mtu huru. Yonyesha kila tendo kwako huliweka kidini.
 
pole sana...ndugu...kwakweli Tanzania imekuwa si nchi salama kwa watu wenye uelewa mpana kuishi..na mbaya zaidi ukiwa na uelewa mpana ukajaribu kuwaelewesha...unakuwa umejiponza...mbinu zozote zitatumika kukuzima...

Eddy,
Soma niliyomwandikia rafiki yangu mmoja anetaka kujua habari zangu za unga:

Wakati huo sasa ni usiku wa manane na nishapeleka SMS kwa sahib yangu mmoja bingwa wa mambo ya mtandao wa kompyuta kumjulisha kuwa nimekamatwa uwanja wa ndege kwa tuhuma za uongo za kuvusha mihadarati na yeye ile kuipata tu ule ujumbe wangu akaifahamisha dunia kuwa nimekamatwa uwanja wa ndege nikitokea mkutanoni Iran na nimebambikiziwa tuhuma za kuingiza nchini mihadarati. Waliponitia mbaroni tu walinionya kuhusu kutumia simu yangu ya mkononi lakini bahati nzuri hawakuninya’ganya. Aliyenipa onyo hili alikuwa mkuu wa kituo cha polisi cha uwanja wa ndege. Huyu rafiki yangu akawa kanisaidia sana maana hadi kumekucha wapenzi wangu wote ndani na nje ya nchi pamoja na vyombo vya habari vinavyonifahamu walikuwa na taarifa za kukamatwa kwangu. (Kwa kipindi takriban miaka ishirini nyuma kwa nyakati fofauti nimekuwa nifanya mahojiano na radio zote muhimu kama, BBC, VOA, Sauti ya Ujerumani, Sauti ya Iran nk.).

Kilichotokea Chuo Kikuu Cha Ibadan ni hiki: Unajua ile paper yangu ilibadili mwelekeo wa ule mkutano na mimi
nilikuwa kati ya wazungumzaji wa mwisho.

Waamerika ingawa wanajifanya wanajua lakini si kuwa kila kitu kiko
hadhir kwao.

Naamini walishtuka sana nilipowaambia kuwa Waislam wa Tanzania
hawana ugomvi na USA wao wana matatizo yao ya ndani na utawala
ulioko madarakani.

Walishtuka nilipowaambia kuwa Waislam wa Tanzania wangependa
kuwe na mjadala wa wazi kujadili matatizo yote wanayowakabili kama
elimu na fursa zingine.

Bahati mbaya Sheria ya Ugaidi imesababisha viongozi wao kukamatwa
na taasisi zao kufungwa kwa uonevu tu.

Sasa pale Chuo Kikuu Cha Ibadan kitabu cha Sykes kimekuwa kikisomeshwa
toka 2003 na rafiki yangu Oleduso huyu kijana ni ''political scientist,'' wa
haja na ndiye aliyenialika.

Tulifahamiana Kampala mwaka wa 2003 katika mkutano.

Wanafunzi na waalimu wakawa wanaijua hali ilivyo Tanzania na hii ndiyo
sababu ya wao kusema Sheria ya Ugaidi haiwezi kupitishwa Nigeria kwani
huko ni kutangaza vita na Waislam. Walikuwa tayari washaona athari yake
kwa Tanzania.

Waamerika wakawa kwa njia moja nimewavurugia mipango yao.
Yaliyofuatia hapo sasa ni historia.

Haya yameshapita na naamini ipo faida imepatikana katika kuandika na kusema maneno yale mbele ya Wamarekani siku ile pale Ibadan kwani 2011 nilialikwa Marekani na hao hao Waamerika na nikafanya mihadhara miwili Chuo Kikuu Cha iowa, Iowa City na Northwestern University, Evanston Chicago. Waliniambia kuwa nimewasaidia sana kujua historia ya Tanzania. Alhamdulilah. Hivi tunavyozungumza sasa kuna jopo linaongozwa na Prof. Shivji linaandika upya historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika kupitia maisha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nimefanya mahojiano na jopo hili mara tatu na nimewapa picha na nyaraka za wazee wetu.

zANheiH8lxo1CMBnRgffqHWPtjrAGffz_Cb3A24Mi4XAraJQtc9uayUAReib2Ut_JWareMWQauVeV-a6_CmyFMJGyGHn214X7Pa0aeyioXIVabzDZ_u3JqtfZT6HOHsylrSd9lEtsjJkxZckOopynK5eew8-CjuabfMwaI_2e8dIGuOj9__6JW9KXCacOsfFGM7sRYqJ1GhkbYOSMxgcu2XFmPArnSLzrVQ2fUQtflVh6k4JSGhd3ZB_QO9v7HMEhtoWKhYZiisZJZngLsz0YU8VLUfVSeWO7JDKrmU6-t1O6fgytxHgD6bQpGgdgRGc16mWQEFU_CJy0t48c7TaxnPGDXh-Tvc7Wx-eLFMPDweSuQdfyx0FDQzRw15u4cL1E7TpCeX0cDfBLhw4BkCsu8AWg2kZq8Ib784NEyYZXeYu_xcA_UfQani9e6R33KoOo-_e8xlGtJ1ClzQpHLwW-8T324w9n55mkxG5ujP7fn_AjVI9swJr9E3hplmIx_85vAjEQjdxVAzhgM6ySmWEjaFa8EnUAvFVe_73vHLCvHcX5TqiTlYeSz7-YLiareiV-I-G13K_G2T7OI2iiMhBfc6jSFtQCyMiQr2lq6GkWQlU5FrnHERV=w800-h534-no

Prof. Shivji, Prof. Saida Othman na Mwandishi
 
Aiseeeee mnashida kweli na uislam wenu..... Eti kwa uwingi wa waislam Tanzania.... Inaonyesha wewe mwisho wako ni mikoa ya pwani tuu maana ndo angalau yenye waislam... Usithubutu tena kusema mpo wengi utaonekana darasa kwako ni zero...... Huko unakosema Nigeria wenzio walidanganyana hivohivo... Wakaanza kuwaletea Shida wakristo walichokipata hata wewe unakijua.... So kaa kimya
 
Kwa akili ya kawaida tu kati ya mtu anayetokea nchi yenye ebola na anayetokea nchi yenye malaria nani atawekwa quarantine kwanza? Huo utakuwa ubaguzi?
Nina mashaka sana na uwezo wako wa kufikiri kama mtu huru. Yonyesha kila tendo kwako huliweka kidini.
Miki,
Tatizo liko kwako.
Wewe ndiye unaetishwa na historia ambayo hukupata kuijua kabla.

Magazeti yote hapa nchini wanachapa makala zangu bila matatizo yoyote.

Naalikwa kwenye TV na radio stations kwa mahojiano na mengine huwa
mubashara.

Wahariri wote hao wala hawana shida na mimi na mimi huzungumza kama
ninavyozungumza hapa.

Napokea mialiko kila uchao ndani na nje ya nchi.
Tatizo haliko kwangu tatizo unalo wewe.
 
“Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.

Hii inaonyesha mambo Mawili makubwa.

1.Inferiority Complex kutokana na kutokuiona Imani dhaifu uliyonayo dhidi ya dini yako.
2.Kuamini kwamba Wakristo ni watu wanaoaminika Duniani hivyo vyombo vya Dola havina shaka nao.

Umeonyesha udhaifu mkubwa sana.Naomba nikupe moyo na kukufundisha mambo mawili.

1.Jipe moyo na iamini dini yako maana ni miongoni mwa dini zenye heshima ila baadhi ya Magaidi ndio wanaitumia vibaya.
2.Kuna Wakristo wasio waadilifu na wanakamatwa kama ulivyokamatwa wewe.
 
Aiseeeee mnashida kweli na uislam wenu..... Eti kwa uwingi wa waislam Tanzania.... Inaonyesha wewe mwisho wako ni mikoa ya pwani tuu maana ndo angalau yenye waislam... Usithubutu tena kusema mpo wengi utaonekana darasa kwako ni zero...... Huko unakosema Nigeria wenzio walidanganyana hivohivo... Wakaanza kuwaletea Shida wakristo walichokipata hata wewe unakijua.... So kaa kimya
KPS...
Unaweza ukasoma hapo chini:
About two-thirds of East African Muslims reside in Tanzania[1] which is the most populous of the East African countries, i.e. Kenya, Uganda and Tanzania. This includes Zanzibar-a predominantly Muslim country with a 99% Muslim population and once the centre of Islamic

learning in East and Central Africa. According to the 1957 population census, Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two. This, at that time, meant that Tanzania was a leading Muslim nation South of the Sahara. But in the first post-independence census of 1967 the total figures for Tanzania Mainland were 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief. These figures show Pagans as a leading majority in Tanzania. The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of animists amidst believers in the span of the last ten years.

This was the last population census showing religious distribution. It is widely believed that the figures for the 1967 census were doctored for political reasons to show that Muslims were trailing behind Christians in numerical strength. There is evidence that the government in 1970, having realised that Muslims were a majority in Tanzania, directed the Statistical Department to destroy all the 1967 census results. [2]

Unfortunately power sharing in the political system in Tanzania is very much skewed against Muslims, although it is known that the stability of any nation depends on proper balancing of these facts. Different sources provide different Muslim-Christian religious distribution figures. These conflicting figures are as a result of sensitivity of the issue. Among African countries with sizable population of Muslims and Christians, like Tanzania and Nigeria,[3] the inquiry as to which faith commands a leading majority, is a source of potential conflict and controversy. Tanzania is of no exception. D.B. Barret[4] gives figures which show Muslims as a minority in Tanzania. The Muslim population is purported to be 26%, Christian 45%, local belief 28%. Tanzania National Demographic Survey figures for 1973 put Muslims in Tanzania slightly above Christians at 40%, Christians 38.9% and local belief 21.1%. But according to Africa South of The Sahara, [5] Muslims in Tanzania are a leading majority at 60%. This figure has remained constant in all its publications since 1982. Since research by Tanzanian Muslims on Islam is scant or almost non-existent, the issue of Muslim population has yet to be tackled from an Islamic point of view. [6]



[1] August H. Nimtz Jr, Islam and Politics in East Africa, University of Miannapolis, 1980, p.11.

[2] See Family Mirror, Second Issue, November, 1994, p. 6.

[3] Ali A. Mazrui, ‘African Islam and Competititive Religion: Between Revivalism and Expansion’, in Third World Quarterly Vol. 10. No. 2 April, 1988, pp. 499-518.

[4] D.B.Barret, Frontier Situations for Evangelisation in Africa ,Nairobi, 1976.

[5] Africa South of The Sahara, Europa Publication, London, No. 20, 1991, p. 1027.

[6]The only conclusive Muslim research is by Dar es Salaam University Muslim Trustee (DUMT), see 'The Position of Muslims and Islam in Tanzania', in Al Haq International (Karachi) September/October1992.
 
Lizarazu,
Mimi nasisimkwa sana kila ninapokutana na mtu mzima na akanipa historia
za wazalendo waliopita ambao wengi hawajui michango yao.

Hebu soma kisa cha Salum Abdallah:
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.

Shekh. Mohamed
Binafsi nimeufuatilia uzi wako toka mwanzo mpaka hapa ulipofikia na nimeona vitu vikuu vitatu;

1.wewe ni mtu mwenye busara nyingi unaoweza kukabiliana na hali yoyote hatarishi katika namna sahihi.

2.mkufunzi mzuri mwenye kufahamu mengi kuhusiana na historia ya taifa letu hususani yale ambayo yamekuwa akifichwa na kufahamika kwa wachache.

3.ni mwana propaganda ulio makini sana unaeweza kufikisha ujumbe fulani kwa waledi wa hali ya juu sana pasipokuvuruga hali hewa kwa wale wote wasiofurahishwa na ujumbe huo.

Mimi ni msomaji mzuri sana wa makala zako siku zote na huwa nikipitia sikosi kuokota lililo jipya, nakumbuka jinsi ukivyokuja kujibu humu kuhusu ile sanamu ya bwana Bismin iliyopo pale posta ulitoa maelezo ya kutosha tu.. Vile vile pia hata kwenye huu uzi sikuwahi kudhani kama mashujaa wetu wa kiislamu legacy yao imepuuzwa namna hii ndio kwanza nimekuja kuelewa kiundani kwenye bandiko hili.

Bwana Salum Abdallah sikuwahi kumfahamu hapo kabla wewe ndio umekuja kunijuza wasifu wake alikuwa ni nani.

Baada ya kusema hayo nirudi kwenye hii comment yako!!

Mkuu naona kama umenirushia tuhuma zisizonihusu kabisa, hasa kwenye hiyo paragraph yako ya mwisho.. sijui hata ni wapi mimi nimeandika hilo neno "chokochoko" hii ni comment yangu ya pili kwenye huu uzi wako au pengine labda comment yangu uliyoquote hujaelewa ndio maana umenihisi hivyo.

Mimi nimemquote Bak kwa kumtania tu na sio vinginevyo.
 
Hii inaonyesha mambo Mawili makubwa.

1.Inferiority Complex kutokana na kutokuiona Imani dhaifu uliyonayo dhidi ya dini yako.
2.Kuamini kwamba Wakristo ni watu wanaoaminika Duniani hivyo vyombo vya Dola havina shaka nao.

Umeonyesha udhaifu mkubwa sana.Naomba nikupe moyo na kukufundisha mambo mawili.

1.Jipe moyo na iamini dini yako maana ni miongoni mwa dini zenye heshima ila baadhi ya Magaidi ndio wanaitumia vibaya.
2.Kuna Wakristo wasio waadilifu na wanakamatwa kama ulivyokamatwa wewe.
Farudume,
Isome historia ya Sultani Abdul Rauf Songea Mbano kisha ndiyo useme maneno
ya ''complex'' ya aina yoyote:

Wanamajlis,
Naona ukumbi umepoa.
Yuko aliyesema ana maswali kuhusu Nyerere anataka kuniuliza.

Kapotea sijamsikia.

Yuko aliyekuja na mpya kuwa Waislam sio walioanza harakati dhidi
ya ukoloni akataja Maji Maji.

Nikaweka jibu.

Hakuridhika akadai kuwa majibu nimejinukuu mwenyewe kwa hiyo
ni ajua.

451px-Chief_Songea_Mbano.jpg

Chief Songea Mbano

Nikaja na jibu kutola nyaraka za Wajerumani wenyewe waliopigana
na Chief Abdul Rauf bin Songea.

Najua kapata mshtuko kwa kuwa hajapatapo kumsikia Chief Abdul
Rauf bin Songea
katika Vita Vya Maji Maji ingawa inawezekana kuwa
kasikia Chief Songea Mbano.

Najua ametatazika kama wengi wanavyotatazika hivi sasa wakinisoma.
Hawa ni watu wawili au ni mtu mmoja?

Abdul Rauf bin Songea ndiyo huyu Songea Mbano?
Kuchakachua historia kuna hatari zake na hii ni mojawapo.

Hakuwa anajua kuwa Vita Vya Maji Maji Waislam walisimama dhidi ya
Wajerumani.

Majemadari 60 Waislam walinyongwa na kuzikwa kaburi moja Mahenge,
Songea na kumbukumbu ya iko hapo kwenye kumbukumbu ya Maji Maji
Songea.

Katika kaburi la peke yake amezikwa Songea Mbano.
Je huyu ndiye yule Abdul Rauf bin Songea?

Kuna mahali Abdul Rauf bin Songea anaitwa kwa jina la ''Chief Songea
Luwafu Mbano.''



Soma hapo chini:


One of these is Chief Songea Luwafu Mbano, from whom the town takes its name. As the most famous of the Ngoni resistance leaders, the Germans honoured ...

CYgjIZKWYAA1G2j.jpg

Hii ''Lwafu,'' ndiyo Rauf?

Huyo hapo juu kwenye picha ndiye Chief Abdul Rauf Songea Mbano
Jemadari Muislam wa Vita Vya Maji Maji.

Angalia hapo chini ghafla majina ya hawa Waislam hayaonekani badala
yake kuna majina mengine lakini ni ya wale wale Waislam walionyongwa:

DSC02264.jpg


Nani huyu anaepotosha haya majina mazuri ya Waislam katika historia
ya Maji Maji?

Sasa soma hapo chini:


Islam has always been the ideology of resistance against colonial rule or any other authority which tried to subjugate Muslims. Consequently, no government in power either indigenous or foreign has ever been kind or supportive to Islam, and likewise Muslims have always been engaged in a continuous struggle to preserve their faith and fight for their rights. Christianity was resisted by Muslims right from the beginning. In any uprising against the colonial government, Muslims took the opportunity to attack missionaries and Christian establishments. Muslim perceived both missionaries and the colonial government as fellow collaborators and therefore enemies to Islam. Islamic radicalism has therefore a long history in the struggle against colonial rule and Christianity. Christianity became a reactionary force siding with the colonial authority. One needs only to read the letter written by the Chief Songea bin Ruuf at the time when he was mobilising his people for war while at the same time trying to cement alliances with other chiefs in Southern Tanganyika and across the River Ruvuma in Mozambique. This letter written to Sheikh and Sultan Mataka bin Hamin Massaninga reads:
''Sultan Songea bin Ruuf writes: To the Shaykh and Sultan Mataka bin Hamis Massaninga. Greetings, etc. I am sending you a letter throughKazembe. We have received an order from God that the Europeans must leave the country. We are in the process of fighting them here. I believe that we have long since been reconciled,[so] send me your children, so that we may make an alliance. I had wanted to send you some cattle as a gift, but am not able to do so, as the war which God desired is continuing. Send me a hundred riflemen, and support me in storming the Boma (Songea).

I am also sending you a flask of the Prophet Muhammad, which contains the means for conquering the Europeans. Have no doubt about it, it possessed great power. And when we have taken the Boma (Songea), we shall go on the stations on the Nyasa together, you and I. Now, let us forget our old quarrels.
This bottle, with a da’wa, has been sent by Chinyalanyala himself, the war leader. He also sends the container (kombe), and sends you many greetings.
If your men will come, then Chinyalanyala himself will come and will give you many of the holy things.
Hassan bin Isma’il greets you.
Many salutations,
Sultan Songea bin Ruuf.” [1]
A point to note here is that this letter, beautiful as it is, it is being doubted by Becker, who maintains that the origins of the letter are dubious.[2] This is the stand which many Christian researchers have taken when faced with the realities of Islam in Tanganyika.


[1] C.H. Becker, ‘Material for the Understanding Islam in German East Africa’, Tanzania Notes and Records, No. 68, February, 1968, p.58.
[2] Ibid.
Angalia jina la Kazembe no. 51 na Hassan bin Ismail no, 53 majina ambayo Chief Abdul

Rauf bin Songea kayataja katika barua yake.

Angalia neno ''bin'' katika baadhi ya majina kisha jiulize na wapi likawekwa neno ''bin,'' kwa
asiyekuwa Muislam.

DSC02267.jpg

Kaburi la Chief Abdul Rauf Songea Mbano katika Maonyesho ya Taifa ya Maji Maji
Mahenge, Songea ambae kazikwa kwa jina la Songea Mbano.

Kutoka: Mohamed Said, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of The Muslim Struggle Against British Colonialism in Tangnayika, Minerva Press, London 1998."[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Sultan Songea bin Ruuf huyu hapo juu ndiyo huyu anayoelezwa tena hapa chini kama Chief
Songea Mbano?:


"Anasema hali hiyo ilitokea kwa sababu Chifu Songea Mbano alikuwa ndiyo Jemedari Mkuu wa Jeshi la Wangoni na alikuwa ni hodari sana asiyeogopa lolote kwa hiyo Wajerumani walitaka abakie ili wamtumie kwa malengo yao.

"Yeye Chifu Songea alidai na yeye anyongwe kama walivyonyongwa ndugu zake, basi alinyongwa na Wajerumani ambao waliondoka na kichwa chake wakiwa wamekiweka ndani ya kasha kwenda Ujerumani ambako hakijarudi hadi leo na kiwiliwili chake kuzikwa katika kaburi la peke yake."
(Kutoka:Historia Ya Vita Vya majimaji.)
Wanajamvi,
Naamini mnaiona tofauti iliyopo.
Au hawa ni machifu wawili tofauti?

Nani anahusika na uchakachuaji huu wa majina haya ya Kiislam katika historia ya Vita Vya Maji Maji?

Farudume,
Waliotingwa na ''kujihisi wadogo,'' chembelecho, ''inferiority complex,'' ni hao
waliofuta historia ya majemadari hao hapo juu.
 
Shekh. Mohamed
Binafsi nimeufuatilia uzi wako toka mwanzo mpaka hapa ulipofikia na nimeona vitu vikuu vitatu;

1.wewe ni mtu mwenye busara nyingi unaoweza kukabiliana na hali yoyote hatarishi katika namna sahihi.

2.mkufunzi mzuri mwenye kufahamu mengi kuhusiana na historia ya taifa letu hususani yale ambayo yamekuwa akifichwa na kufahamika kwa wachache.

3.ni mwana propaganda ulio makini sana unaeweza kufikisha ujumbe fulani kwa waledi wa hali ya juu sana pasipokuvuruga hali hewa kwa wale wote wasiofurahishwa na ujumbe huo.

Mimi ni msomaji mzuri sana wa makala zako siku zote na huwa nikipitia sikosi kuokota lililo jipya, nakumbuka jinsi ukivyokuja kujibu humu kuhusu ile sanamu ya bwana Bismin iliyopo pale posta ulitoa maelezo ya kutosha tu.. Vile vile pia hata kwenye huu uzi sikuwahi kudhani kama mashujaa wetu wa kiislamu legacy yao imepuuzwa namna hii ndio kwanza nimekuja kuelewa kiundani kwenye bandiko hili.

Bwana Salum Abdallah sikuwahi kumfahamu hapo kabla wewe ndio umekuja kunijuza wasifu wake alikuwa ni nani.

Baada ya kusema hayo nirudi kwenye hii comment yako!!

Mkuu naona kama umenirushia tuhuma zisizonihusu kabisa, hasa kwenye hiyo paragraph yako ya mwisho.. sijui hata ni wapi mimi nimeandika hilo neno "chokochoko" hii ni comment yangu ya pili kwenye huu uzi wako au pengine labda comment yangu uliyoquote hujaelewa ndio maana umenihisi hivyo.

Mimi nimemquote Bak kwa kumtania tu na sio vinginevyo.
...
Liza...
Hilo neno, ''chokochoko,'' lilisemwa na Nanren ambae ndiye niliyempa jibu
hilo nililoweka hapo na wewe ukalisoma.

Sijakukusudia wewe ndugu yangu.
Ukirejea kusoma tena utaona.

Huyu Salum Abdallah bibi zangu wakisema kuwa ule, ''wazimu,'' wake umewaruka
wanae wote umenikumba mie.

Huyu mtu ana mengi bwana katika struggle ya Tanganyika maana yeye kapambana
na Waingereza toka enzi za African Association 1929.
 
Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza.

Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo.

Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama.

Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.

Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha kuwa yawezekana wamefananisha majina.

Niliwaambia huenda Mohamed Said muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa.

Wakaniamuru sasa tutoke twende nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa haraka huku nikisoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu.

Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike na shari yangu.

Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka Tehran mizigo ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama.

Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa zilizowafikia. Wakasema, “Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni msafirisha madawa ya kulevya.”

Nikawauliza,“Baada ya kupata taarifa hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?” Wakasema, “Ndiyo maana leo tumekukamata.” Nikawaambia, “Si kweli kama kwa sababu mie nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni “Mzungu wa Unga” kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya.”

Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi nini katika hii safari ya Iran?

Niliwaeleza kuwa miezi michache iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano umefadhiliwa na serikali ya Marekani na wamenipa na tiketi toka Dar es Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha.

“Mbona hamkunikamata wakati ule?” Nikafungua mlango mwingine nikawaambia, “Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.

Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu.

Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule. Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa.

Nikakataa kujisaidia pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.

Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na “audio cassette” nilizokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini. Nikawauliza, “Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa Tanzania?
Ni kisa kizr kujifunza lakini kimeniboa ulipoingiza utetezi wako wa kidini,,
Vatican na Tehran kwa kipindi hicho cha 2007 wapi kuliongoza kwa mihadarati,,

Nyie watu kwann badala ya kusimamia kwenye KWELI yenu ili mpate HAKI yenu mnakimbilia kulilia udini wenu,,
Si kosa lenu nasikia Kitabu chenu eti tangia mwanzo wa Aya hadi mwisho wake hakuna neno,, KWELI,, bali mna HAKI tu.
Wew umekamatwa kwa kuhisiwa tu ,, na ktk nafsi yako una hakika na KWELI yako kwamba ktk mizigo yko yote huna mihadarati hata kidogo,,

Sasa kwann usisimamie ktk KWELI yko badala yke unajitetea kwa kusema Vatcani kuna Wakristo wengi kuliko hapo Airpot,,

Huu ni utetezi wa kishamba na kutojiamini ktk Imani yako,, maana Huamini ktk KWELI ,, muda wote roho yko imejaa kutojimini ktk KWELI,,
 
Back
Top Bottom