Mohamed Salah asaini kandarasi ya miaka 5 na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu

Mohamed Salah asaini kandarasi ya miaka 5 na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu

Kifupi ikifika jumapili saa 6 dakika 1 usiku akaunti yake inasoma Milioni 600 Tsh
Mishahara ya UK kwa wanaolipwa kwa week ni kila ijumaa account inacheka. Saa sita na dk zake usiku wa ijumaa account inakua ishanona
 
Daaah ila bado ndefu sana


Kuna Ronaldo mwenye 360,000 GBP pia Mbappe yupo kwenye range hiyo hiyo pia. Halafu unamkuta Lionel Messi wanasema anaweza kuwa anachukua 500,000+ GBP kwa wiki.

Ndio dunia ilivyo. Hata huwa sihuzuniki sababu hao jamaa ni nyota. Isingekuwa fair mtu ambae anaangaliwa na Watu bilioni kila mechi awe sawa kipato na mwalimu au Daktari ukiachilia mbali kuwa vilabu hivyo vinaingiza mamia ya mabilioni kwa kimoja kimoja na vingine kama Manchester United vinaingiza takribani Tsh Trillion 2 (TZS 2,000,000,000,000/=) na vimeingiza pesa nyingi hizo kwa ajili ya jasho na vipaji vya hao nyota
 
Mishahara ya UK kwa wanaolipwa kwa week ni kila ijumaa account inacheka. Saa sita na dk zake usiku wa ijumaa account inakua ishanona
Dah kumbe ijumaa
Ndo mana sishangai waafrika kwenye timu za afrika wanaocheza UK walikua wanacheza kama hawataki ili wasiumie na ligi inakaribia kuanza wasipoteze mamilioni kwa wiki
 
Alaa, kumbe imeshuka hadi 3000 !

Nilichokuwa nimemsahihisha huyo jamaa ni kuwa mara nyingi kama mtu atatumia rate wanazooffer hawa Bureau de change inabidi atumie bei ya "SELL" na sio "BUY" sababu currency ambazo sio hard currency Bureau de change zote duniani huziwekea spread kubwa ili kucompensate faida tofauti na hard currency. Mfano mimi ningekuwa naishi UK basi ninaporudi TZ ningekuwa nabadili GBP kwenda USD huko huko ndio kisha nije kubadili kwenda Madafu nikishatua Bongo, nisipofanya hivyo nitakuwa ninapoteza zaidi ya shilingi mia mbili kwa kila pauni nitakayoibadilishia ambapo , kwa mfano kwa pauni elfu kumi kama nitachange huku bongo tayari nimepoteza kama milioni mbili unlike ningechange kule kule UK kwenda USD

Fact kiongozi nimekuelewa vizuri kabisa, yani umeongea point moja muhimu sana. Nashkuru bro MASAMILA..hata kama ni mimi ningekuwa UK ningechenchia huko huko kwenda USD.. pesa yetu haina thamani kila siku inashuka
 
Back
Top Bottom