Mohamed Salum: Nchi zenye Mitaji Mikubwa ya Uwekezaji Duniani kwa sasa zipo Uarabuni

Mohamed Salum: Nchi zenye Mitaji Mikubwa ya Uwekezaji Duniani kwa sasa zipo Uarabuni

Wadanganyika tuko pale pale. MKATABA MBOVU, WA KINYONYAJI, WA KULAZIMISHANA, HAUKO WAZI, HAUNA KIKOMO, WA KIFISADI.
KAMA WANA HELA ZA KUTOSHA HAWAHITAJI ZETU WALA RASILIMALI NA MALIASILI ZETU, WAENDE KWINGINE BASI?!😠😡🤬😫😩😣
 
Screenshot_20230702-035603~2.jpg

Screenshot_20230702-035531~2.jpg
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Kwa kipi haswa walicho nacho kutuzidi, iwe akili iwe mali asili hawana kitu kutuzidi.
Kwetu changamoto ni viongozi tuu
Ukishazidiwa viongozi matokeo yake utazidiwa kila kitu
 
Mwanasheria Mohamed Salum amesema Nchi zenye mitaji ya uwekezaji mkubwa duniani kwa sasa zipo Uarabuni.

Waarabu hawa wamewekeza kwenye nchi nyingi duniani ikiwemo Ulaya. Kwa DP World wana mtaji mkubwa wa kifedha, hakuna nchi inayofanya biashara bila kuruhusu sekta binafsi.

Amesisitiza kuwa nchi za Mashariki ya Kati ndio zinamiliki uchumi wa dunia kwa sasa hivyo nadharia za kutajana majina (Mabeberu) hazitatupeleka popote.

Ametoa jibu hili kwa mdau aliyetaja kufahamu ni kwa namna gani DP World ambayo ni kampuni ya waarabu (Mabeberu) ilivyo safi, kwa kukumbuka kuwa ndugu zetu wa Loriondo wamepitia mateso makubwa yaliyosababishwa na waarabu.

Chanzo: Msemaji Mkuu wa Serikali (Clubhouse)
Hiyo data umepata wapi? Nchi zenye mitaji mikubwa ukiacha G7 ni BRICS, hizo za middle east ni zipi unazosema? Tupe data....Au unataka kusema Israel? Labda! UAE ni sawa lakini ni nchi moja tu kaka Mohamed Salum, usivutwe na jambo usilolijua kwa ajili ya ushabiki,asili au dini....Ongea ukweli.
 
Hakuna anaebisha kwa hilo tunachotaka ni kurekebishwa vipengele vyenye utata ni hayo tu.
U have a very good point ,issue kubwa ambayo wananchi wanatakiwa kwenda nayo ni hiyo, lakini wao mara muarabu mara mzanzibari mara uislamu hapo ndio wanspoteza nguvu ya hoja zao .
 
Hiyo data umepata wapi? Nchi zenye mitaji mikubwa ukiacha G7 ni BRICS, hizo za middle east ni zipi unazosema? Tupe data....Au unataka kusema Israel? Labda! UAE ni sawa lakini ni nchi moja tu kaka Mohamed Salum, usivutwe na jambo usilolijua kwa ajili ya ushabiki,asili au dini....Ongea ukweli.
Israel kuna njaa na dhiki hali ys maishz ni ngumu sana, uae, saudi arabia, qatar ,kuwait etc wananchi wana kipato kikubwa ndio maana wakenya wengi sasahivi wapo huko wamechungulia fursa wewe utabakia na ulokole wako kuendeleza chuki zako ,wale hawakopi bank mzee kama matajiri wa kizungu wengi na hawana propaganda ila hela yao inaongea, wazungu wenyewe walikaa midomo wazi kwa jinsi qatar walivyoonyesha kufuru ya hela kwenye kombe la dunia
 
Alisoma huyo mtu wenu kabla hajasign?
Hapo ndo shughuli ilipoanza kuwa ngumu
 
Man City, PSG , Newcastle FC zote ziko chini ya warabu na ndo zinatetemesha soka la Ulaya. Soon Man Utd nae anaenda kuwa chini ya warabu

Huo ndo ukweli.
WAnaonufaika ni waarabu au wazungu?
 
Mwanasheria Mohamed Salum amesema Nchi zenye mitaji ya uwekezaji mkubwa duniani kwa sasa zipo Uarabuni.

Waarabu hawa wamewekeza kwenye nchi nyingi duniani ikiwemo Ulaya. Kwa DP World wana mtaji mkubwa wa kifedha, hakuna nchi inayofanya biashara bila kuruhusu sekta binafsi.

Amesisitiza kuwa nchi za Mashariki ya Kati ndio zinamiliki uchumi wa dunia kwa sasa hivyo nadharia za kutajana majina (Mabeberu) hazitatupeleka popote.

Ametoa jibu hili kwa mdau aliyetaja kufahamu ni kwa namna gani DP World ambayo ni kampuni ya waarabu (Mabeberu) ilivyo safi, kwa kukumbuka kuwa ndugu zetu wa Loriondo wamepitia mateso makubwa yaliyosababishwa na waarabu.

Chanzo: Msemaji Mkuu wa Serikali (Clubhouse)
Haya ndiyo madhara ya kuongozwa na viongozi wajinga ambao wameshindwa kufikiri na wanataka kuongoza nchi kwa mawazo ya kuazima.
 
WAnaonufaika ni waarabu au wazungu?
Its business wote wananufaika, huyu anaingiza mtaji akitegemea kupata faida ,huyu mzungu anapata kodi ,ajira etc ,ndio ulimwengu wa biashara ulivyo hakuna cha bure
 
Man City, PSG , Newcastle FC zote ziko chini ya warabu na ndo zinatetemesha soka la Ulaya. Soon Man Utd nae anaenda kuwa chini ya warabu

Huo ndo ukweli.
Nonsense.

Rasilimali za taifa kuwekwa rehani ni zaidi ya kuimiliki PSG, Man City, na Newcastle.
 
Its business wote wananufaika, huyu anaingiza mtaji akitegemea kupata faida ,huyu mzungu anapata kodi ,ajira etc ,ndio ulimwengu wa biashara ulivyo hakuna cha bure
Kwa hiyo huruhusu raslimali zetu zichukuliwe kienyeji kwa mikataba ya hivyo ya kifisadi? Ulaya wanaweza kukubali mkataba kama huu wa DPW
 
Kumbe sasa hivi tuna Mwanasheria Mkuu Muslim, du sikufahamu.
Awamu hii Muslim mkikosa vyeo,mtajilaumu sana.
 
Jamani hivi inakuwaje watu wazima wanakuwa na arguments za hovyo hivi,kwani hapo issue ni mtaji au ubovu wa mikataba.
 
Kwa hiyo huruhusu raslimali zetu zichukuliwe kienyeji kwa mikataba ya hivyo ya kifisadi? Ulaya wanaweza kukubali mkataba kama huu wa DPW
Kwani hujui kwamba dp world wapo hadi uingereza, na marekani walikataliwa kwa sababu tu ni waarabu na kwamba itahatarisha usalama wai ukizingatia sera zao kuhusu waarabu, ila bush alishakubali wapewe bandari
 
Back
Top Bottom