Mohammed Hussein ni moja ya mzigo na udhaifu wa Simba

Mohammed Hussein ni moja ya mzigo na udhaifu wa Simba

Ok nimeangalia tena hilo, nakiri hapo nimekosea ila mengine yote niliyosema yanabaki hivyo hivyo. Kabla ya ile penati Zimbwe ndiye aliachwa na mchezaji wa Primeiro, nikachanganya nikidhani yeye ndiye alikuja kunawa.
fikiri kwa kichwa na sio makalio
 
Penati kasababisha Kennedy
Pili zimbwe alikuwa busy leo....., nadhani upande wake anacheza mchezaji tegemeo/ ndio upande wanaoutumia sana hawa jamaa...
Winga wao hatari anaitwa camilo anacheza upande ule leo zimbwe alikua na kazi ya ziada sana
 
Wewe umewahi kucheza angalau chandimu!mpira unamambo mengi unawaza kuokoa ,unawaza umpekipa, fikiria vizuri
Pira nimelipiga saana tu ndiyo maana naweza kuona madhaifu ya mchezaji.
 
Tabia za kinafiki hizo wanazo mashabiki wa Utopolo.

Sisi ni watulivu sana na bora uzungumzie mengine lkn sio Zimbwe jR
 
Ok nimeangalia tena hilo, nakiri hapo nimekosea ila mengine yote niliyosema yanabaki hivyo hivyo. Kabla ya ile penati Zimbwe ndiye aliachwa na mchezaji wa Primeiro, nikachanganya nikidhani yeye ndiye alikuja kunawa.
Mpaka hapo umeonekana huna uhakika na unachoongea, mpaka ukumbushwe ndio uone tatizo lilipoanzia? usirudie tena kuleta Utopolo wako hapa
 
1.Upande wa zimbwe kulikua na winga hatar anatumia shoto
2. upande wake alikua na okra na hakua anarud kumsaidia kukaba
 
Katika tathmini yangu ya uchezaji na mchango wa Mohammed Hussein kwa timu ya Simba, uchezaji wake umekuwa unaleta makosa mengi kwa timu.

Mfano katika mechi ya leo, Zimbwe alifanya makosa mengi sana. Yaani inafikia wakati kila akipata mpira, unategemea kuna ujinga ataenda kufanya. Akiwa anakaba lazima atafanya kosa.

Kuna kona alisababisha kipindi cha kwanza, yuko nje ya goli, mchezaji pinzani yuko mbali, akautoa mpira nje akiwa peke yake ili iwe kona!

Akiwa uwanjani anajiamini sana kama vile anafanya vitu vya maana ila ni moja ya mapungufu ya timu kwa sasa.
Kweli wajinga kama wewe mpo wengi sana na wote mnamajina ya Chura!
 
Penati kasababisha Kennedy
Pili zimbwe alikuwa busy leo....., nadhani upande wake anacheza mchezaji tegemeo/ ndio upande wanaoutumia sana hawa jamaa...
Upande wake yule winga hatari sana mara nyingi alikuwa anajaribu kumchekecha sana Hussein ili aingie ndani ya box la 18.

Lakini Hussein anasalia kuwa Beki bora kabisa upande wa kushoto Simba SC.
 
Upande wake yule winga hatari sana mara nyingi alikuwa anajaribu kumchekecha sana Hussein ili aingie ndani ya box la 18.

Lakini Hussein anasalia kuwa Beki bora kabisa upande wa kushoto Simba SC.
Sio Simba tu......
Tanzania nzima kwa Muongo mmoja sasa.
 
Ok nimeangalia tena hilo, nakiri hapo nimekosea ila mengine yote niliyosema yanabaki hivyo hivyo. Kabla ya ile penati Zimbwe ndiye aliachwa na mchezaji wa Primeiro, nikachanganya nikidhani yeye ndiye alikuja kunawa.
Umejawa na chuki tu. Kwa hiyo wewe una haki ya kukosea ila Zimbwe hana haki hiyo?
Kwanza inaonesha umesimuliwa hukutazama mpira hata. Bodaboda huwa mnajazana ujinga sana vijiweni.
 
Kuna wachezaji Simba Wana bahati ya kupendwa mkude na Mohamed husein ila wote hao Wana mapungufu makubwa.
Sifa kubwa ya Shabalala ni kupendwa kushambulia lakini mipira yake mingi ya mwisho haiendi inapotakiwa sababu anapenda kukaa na mpira muda mrefu na anapoamua kupiga tayari adui anakuwa amejipanga.
Pasi zake nyingi za uchonganishi, anaweza kuacha kutoa pasi Kwa mchezaji ambaye hajakabwa lakini akatoa pasi Kwa mchezaji aliyekabwa na watu 3.
Hana kasi na anapata shida sana anapokutana na winga mwenye kasi pia ana tabia ya kukaba Kwa macho.
 
Back
Top Bottom