Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mbunge Khalifa Mohammed Issa (ACT) kutoka Jimbo la Mtambwe, Zanzibar amesema Rais Samia anabaguliwa kwa Uzanzibar wake. Amebainisha kuwa wanzanzibari hubaguliwa kwa uzanzibari wake na kauli zingine husema Rais Samia anatawala nchi isiyo yake, amekopeshwa kutoka Zanzibari aje kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge Mohamed ameitaka Serikali kupitia vyombo yake kufanyia kazi suala hili ili kuondoa sintofahamu zinazoibuka baada ya kuendelea kutolewa kwa kauli hizi. Aidha, amebainisha kuwa Freeman Mbowe na genge lake ndio wamekuwa wanatoa kauli hizi za kiubaguzi dhidi ya Rais Samia na wazanzibari wote.
Amesema Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibari hivyo hakuna haja ya kubaguana.
Huyu ndiye Mbunge ambaye aliwahi kusema watu kutoka Tanzania Bara wakitaka kuingia Zanzibar wawe na passport.