Mbunge Khalifa Mohammed Issa (ACT) kutoka Jimbo la Mtambwe, Zanzibar amesema Rais Samia anabaguliwa kwa Uzanzibar wake. Amebainisha kuwa wanzanzibari hubaguliwa kwa uzanzibari wake na kauli zingine husema Rais Samia anatawala nchi isiyo yake, amekopeshwa kutoka Zanzibari aje kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge Mohamed ameitaka Serikali kupitia vyombo yake kufanyia kazi suala hili ili kuondoa sintofahamu zinazoibuka baada ya kuendelea kutolewa kwa kauli hizi. Aidha, amebainisha kuwa Freeman Mbowe na genge lake ndio wamekuwa wanatoa kauli hizi za kiubaguzi dhidi ya Rais Samia na wazanzibari wote.
Amesema Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibari hivyo hakuna haja ya kubaguana.
Huyu ndiye Mbunge ambaye aliwahi kusema watu kutoka Tanzania Bara wakitaka kuingia Zanzibar wawe na passport.
Huyo alipaswa kueleza ni kina nani hao na kivipi wanambagua Rais wetu kwa uzanzibar wake.
Pia anapaswa kujua, Rais Samia ni Mzanzibar kwa 100%, watu wanapo mtambulisha kama mzanzibar sio kuwa wanambagua bali wanamsifia, maana ndivyo alivyo na anajivunia kuwa Mzanzibar.
Napinga andiko lako!
Nimesikiliza bunge live na nimemsikia vizuri!
Ameelezea hakuna muungano, Zanzibar na Tanzania NI nchi mbili tofauti
Anayo hoja, asikilizwe
Mbunge wa Konde (ACT Wazalendo), Mohamed Said Issa amesema siku yoyote anaweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo vyombo vya ulinzi na usalama vidhibiti ubaguzi dhidi ya Wanzibari.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano anabaguliwa kwa sababu ni Mzanzibari, hivyo na yeye anaweza kubaguliwa atakapokuwa Rais.
Issa ameyasema hayo leo Jumatano, Mei 15, 2024 wakati akichangia kwenye makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Mbunge huyo Aprili 23, mwaka huu alinukuliwa bungeni akitaka urudishwe utaratibu kuingia Zanzibar kwa pasipoti ili kudhibiti uingiaji wa watu visiwani humo wanaochukua ardhi ya Wazanzibari.