Mohammed Matumla vs Wang Xing Hua ni hatari tupu leo Diamond Jubilee

Ududu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
1,020
Reaction score
556


Leo ni leo tusubiri kuthibitishiwa ule usemi ''Mtoto wa nyoka ni nyoka' au mtoto wa nyoka leo atakua mjusi pale ambapo bondia Mohammed Matumla toka Tanzania watazipiga na Wang Xing Hua toka China.

Pambano lingine leo la utangulizi ni kati ya Mada Maugo na Japhet Kaseba.

Binafsi nina imani sana na watoto wa Keko hivyo naamini Mohammed Matumla hawezi kutuangusha watanzania.

Ombi: Waandaaji wapunguze kiingilio mana Tsh 20, 000 ni nyingi sana ukizingatia hali za wapenzi wengi wa ndondi hapa Tanzania.

Tutakuwa pamoja Live nami kutoka hapa Diamond Jubilee kuanzia mida ya saa 12:30 jioni.

============
============

Mohammed Matumla ameshinda kwa pointi

 
Hizo za kaseba vs Maugo??? Ila kaseba bado sana kwenye ngumi.
 
Mchina mchina tu na mbongo mbongo tu, hapo mtz lazima atacharazwa.
 
Naskia yule mmarekani alokuwa apigane na Ashraf kaingia mitini wamemleta mkenya
 
the way to MGM grand arena, matumla nipigie mtu leo
 
Daah Maugo vs Kaseba ni rematch,sikumbuki Mara ya mwisho nani alipoteza Kati yso.

.kila la kheri kwa Matumla.
 
Mchina mchina tu na mbongo mbongo tu, hapo mtz lazima atacharazwa.

Tatizo Mchina akipigwa mtakuja na visingizio vingi hapa, mara oohh yule mchina wa kariakoo muuza mahindi!!! Si unakumbuka mbrazil na Cheka?
 
Matumla Jr,amwombe sana mwenyezi Mungu sijui bahati hii kaipatia wapi,ila nafikiri itakuwa imekuja kwa wakati muafaka ili aachane na Tabia yake ya kukabana kwa utaalamu wa Ngumi.

namtakia kila Raheli.
 
Tatizo Mchina akipigwa mtakuja na visingizio vingi hapa, mara oohh yule mchina wa kariakoo muuza mahindi!!! Si unakumbuka mbrazil na Cheka?

namjua Matumla Jr.Akishinda itakuwa mipango ya Mungu tu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…