Mohammed Mchengerwa: Rais Samia Ameipandisha Hadhi Geita kuwa Manispaa na Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Hayo ndio maelezo ya Waziri wa Tamisemi bwana Mohammed Mchengerwa akirejea maamuzi ya Rais Samia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipandisha hadhi Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji na Halmashauri ya Mji wa Geita kuwa Manispaa.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Desemba 13, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Rufiji kwenye uwanja wa ujamaa - Ikwiriri walifurika kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la Bibi Titi Mohamed.

Soma Pia: Mchengerwa: Rais ameridhia kuipandisha hadhi Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji. Soko kubwa na Stendi kuanza kujengwa

Amesema “Bibi Titi Mohamed huko aliko atakua anafurahia sana maendeleo ya Rufiji maana ndiye Mbunge wa kwanza aliyeasisi jimbo hili alifanya kazi kubwa sana na mimi Mbunge wa tisa naendeleza kazi aliyoianza Hayati Bibi Titi na pia Mhe. Rais amefanya kazi kubwa kwa kuleta miradi mingi katika Wilaya yetu na sasa ameipandisha hadhi kuwa Halmashauri ya Mji.”

Amefafanua kuwa hadhi ya Mji ina maana kubwa sana kwa wananchi wa Rufiji kwa kuwa itakua miongoni mwa Halmashauri zinazojufaika na miradi mikubwa ya Benki ya Dunia na maendeleo yanakwenda kwa kasi katika kila Kata masoko yatajengwa, huduma za Afya zitapatikana karibu zaidi na miradi ya elimu itaongezeka.

“Hivyo tunamshkuru Mhe. Rais kwa kuiona Rufiji na kuipa hadhi ya kuwa Mji na sasa maendeleo katika Wilaya hii katika nyanja zote yataenda kwa kasi zaidi,”amesema.

Tamasha la Bibi Titi linafanyika wilayani Rufiji kwa siku tatu kuanzia tarehe 12-14/12/2023 kwa lengo la kumuenzi shujaa Bibi Titi Mohamed kama mwanamke wa kwanza kupigania uhuru na Mbunge kwa kwanza wa Rufiji.

Kwako mdau Kwa maoni zaidi 👇👇

View: https://x.com/Jambotv_/status/1867627948863594579?t=KyUmIvaK4s-j5jvqNaF9Mw&s=19
 
Hongereni Rufiji...

Hongereni Geita...
 
Back
Top Bottom