TANZIA Mohammed “Muddy Physics” wa Mchikichini afariki dunia

Alituokoa sana sana huyu mwamba.Nilisomaga Simple &Harder mechanics buree kwa huruma maana nilikuwa hell of poverty.Olevel ndio usiseme.Ukisikia wanasema anazikwa wapi naomba nitag ndugu Mwifwa
Nimeona huko Juu wanasema Mwandege Vikindu
 
Uwe makini unaweza tongonza hata mkeo/girl friend wako. Mnabadilishana number siku ya kukutana inakuwa msala.
Niliwaza hivyo hivyo [emoji23][emoji23]nikaona nisiandike. Iwe hivyo halafu nikute ni wife daaa! Lakini lazima achezee mitama [emoji23]
 
Mwenyezi Mungu amrehemu,ni mtu ambaye kwamba alikuwa na mchango mkubwa kwa Taifa.

Kwa kufanya vijana wengi kuipenda Physics na kuona moja ya somo rahisi sana

Na amechangia vijana wengi kufika kwenye taaluma za juu kabisa,amechangia vijana kuwa wadadisi na kupenda kuelewa mambo sio kukariri.

Hakiki Muddy ana mengi mazuri ambayo ameitendea haki Physics.

Kwa bahati mbaya watu kama hawa Taifa haliwaoni kama ni asset,wanaachwa tu bila msaada wowote.

Hakika sisi wote ni Mwenyezi Mungu na kwake ndio marejeo.
 
Alinifundisha pia Physics ya advance nikashangaa kuiona kuwa ni rahisi kuliko ile ya O'Level ambayo sikufundishwa nae, jamaa alikuwa mcheshi anapenda kila mtu na kazi yake 2008-10 nilipita mikononi mwake.

Ameitenda vema Kazi yake, mwendo ameumaliza na imani yake kuilinda Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ampokee kwake Mbinguni.🙏🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…