Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Hanga anajua alichokifanya ila wapinzani wa SMZ waga hamusemi ukweli
 
Kwahiyo kaka unataka kutuambia hizbu na shamte na waarabu walikua waungwana kuliko babu zetu waliowapindua!!!Na tukuulize kwanini babu zetu waliwapindua sultan na hizbu????

Mkuu Kwani Zanzibar ndio nchi Peke iliyofanyika mapinduzi Afrika? Kwanini Iddi Amini alipindua Uganda? Kwanini Zaire kulifanyika mapinduzi? Burundi je? Seychelles ? Au hufaham kuwa hata Tanganyika Mapinduzi yalifanyika ila hayakufanikiwa baada Serikali ya U.K kuingilia kati.

Mapinduzi ni trend iliyoingia Africa kuanzia miaka ya 50's mwishoni mpaka miaka ya karibuni tu hapa. Hakuna popote pailipokua na sababu za msingi za hayo mapinduzi zaidi ya Tamaa za kisiasa tu.
 
Hanga anajua alichokifanya ila wapinzani wa SMZ waga hamusemi ukweli

Hanga ndie alieongoza mapinduzi, Hilo ndio lilikua kosa lake kuu, Kila alieshiriki kiundani kuandaa yale mapinduzi aliuwawa, kwa ajili ya kupoteza ushahidi.
 
Nakushauri uisome historia ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka katika vyanzo sahihi.
 
Hanga ndie alieongoza mapinduzi, Hilo ndio lilikua kosa lake kuu, Kila alieshiriki kiundani kuandaa yale mapinduzi aliuwawa, kwa ajili ya kupoteza ushahidi.
Hayo maoni yako au utafiti wa kikachero na source zake ni zipi???
 
Kwahiyo babu zetu walikua hawanyanyasiki na waarabu na vizazi vyao vya machotara wsliowafanya wabantu kua raia wa tabaka la chini???Ni tamaa za kisiasa tu sababu sultan na hizbu walikua wema kwa wabantu kaka?????Tujuze kidogo mema ya sultani kaka???
 
mkuu mbona mpaka vitabu vipo, tatizo lako umekua obsessed na propaganda uchwara za CCM.
Kaka hivyo vitabu aliandika nani?????Na huyo mwandishi lengo lake ni nini????Au vile vitabu vya mzee wangu said mohamed!!!!!Na mkuu kwahiyo tuamini kila kitu kinachoandikwa kwenye vitabu tusihoji kaka????
 
nahicho unachokiamini wewe unahisi kimetoka wapi? kama si masimulizi kutoka kwa watu wa upande fulani. Unachotakiwa ni kupitia historia za pande zote huku ukiwa na fikra huru na ndipo utakapoona akili inafunguka kuona ukweli.
 
Kwahiyo babu zetu walikua hawanyanyasiki na waarabu na vizazi vyao vya machotara wsliowafanya wabantu kua raia wa tabaka la chini???Ni tamaa za kisiasa tu sababu sultan na hizbu walikua wema kwa wabantu kaka?????Tujuze kidogo mema ya sultani kaka???

hiyo ni mada nyengine kabisa mkuu. Waarabu waliishi Zanzibar na Maeneo ya Pwani na wazee wakiafrika waliokua wakiishi maeneo hayo kwanini waliwapenda waarabu? kwanini wamekua ndio role models wao na mpaka dini yao wakaifuata? mtu mmbaya kupindukia anakuaje na influence kwenye jamii kiasi hicho? Kuanzia mavazi, dini, chakula, Ustaarbu. Mbona hatuoni hilo kwa wareno na wajerumani katika influence katika jamii?
Sisemi waarabu kama walikua ni watu watukufu ili napinga hizo propaganda uchwara za kuwachafua kupindukia tulizolishwa.

Unapoambiwa changanya na zako.
 
nahicho unachokiamini wewe unahisi kimetoka wapi? kama si masimulizi kutoka kwa watu wa upande fulani. Unachotakiwa ni kupitia historia za pande zote huku ukiwa na fikra huru na ndipo utakapoona akili inafunguka kuona ukweli.
Upo sahii lakini tatizo la baadhi ya watu hasa waarabu na machotara wenye nasaba za kiarabu na wafuasi wa hizbu na maswaiba wao wa kibantu wanapondea upande mmoja tu SMZ hasa kwenye vitabu vyao!!!Mimi siamini upande wowote kishabiki ila katika hili dhulma ya walowezi wa kiarabu na wakoloni dhidi ya wabantu wa zanzbar ipo wazi toka karne na karne
 
Wewe umejuaje wazee wetu wa pwani waliwapenda waarabu kuamini katika uidlamu nakuchukua tamaduni za kiarabu ndio kumekuhakikishia kua babu zetu wsbantu wa pwani waliwapenda waarabu kaka???
 
Hakuna propaganda waarabu walowezi hawakuwahi kuwapenda wabantu!!!Wao walikua daraja la juu na wabantu watwana na vijakazi kwenye nyanja nyingi tu kaka
 
nahicho unachokiamini wewe unahisi kimetoka wapi? kama si masimulizi kutoka kwa watu wa upande fulani. Unachotakiwa ni kupitia historia za pande zote huku ukiwa na fikra huru na ndipo utakapoona akili inafunguka kuona ukweli.
Mimi msomi siamini katika vitabu bali nachimba historia kisomi!!!!Na sio dhambi kusema mabaya ya walowezi wa kiarabu unguja na pemba kaka
 
ipo wazi kwa njia gani?
 
Hakuna propaganda waarabu walowezi hawakuwahi kuwapenda wabantu!!!Wao walikua daraja la juu na wabantu watwana na vijakazi kwenye nyanja nyingi tu kaka
Wewe umejuaje wazee wetu wa pwani waliwapenda waarabu kuamini katika uidlamu nakuchukua tamaduni za kiarabu ndio kumekuhakikishia kua babu zetu wsbantu wa pwani waliwapenda waarabu kaka???

Ili tujue kama wana wapenda tunahitaji ushahidi gani? kuzipenda na kujinasibihisha na mila zao hayo je sio mapenzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…