Gavana,
Gavana,
Unyama uliotokea Zanzibar baada ya mapinduzi umeacha kovu kubwa sana.
Bahati mbaya walioshika madaraka wameshindwa kutibu kovu hili.
Na hii ndiyo sababu kuu leo CCM Zanzibar kila uchaguzi inashindwa imekata tamaa kama wataweza kushinda uchaguzi huru na wa haki.
Imefika mahali inashindwa na njia ya kujinusuru ni kufuta uchaguzi na kuitisha uchaguzi upya.
Wanazidi kudidimia kama wako katika "quick sand."
Lakini baya zaidi kisaikolojia CCM Zanzibar imeathirika kiasi inaamini njia ya kubaki madarakani ni matumizi ya silaha hata kama itabidi Wazanzibari kuuliwa.
Fikra hii imevunja juhudi yoyote kwa upande wao wa kushinda kwa haki.
Mapinduzi yamepoteza maana.