MOI, JAIPUR warejesha furaha kwa wahitaji 507 kwa kuwapatia viungo bandia bure

MOI, JAIPUR warejesha furaha kwa wahitaji 507 kwa kuwapatia viungo bandia bure

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
Watu 507 waliopoteza viungo, vikiwemo mikono na miguu wamefaidika na uwepo wa kambi maalum ya kutoa viungo bandia bure iliyoandaliwa na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Taasisi ya Jaipur (India) na Ubalozi wa India nchini.

Mratibu wa Kambi hiyo kutoka Taasisi ya MOI Bi, Mary Chandeu amesema hadi kufikia jana Desemba, 30, 2025 watu wenye uhitaji wa viungo saidizi 507 wamepatiwa viungo hivyo bila malipo yeyote katika kambi inayoendelea eneo la Swami Vivekananda, Masaki jijini Dar es Salaam.

Amesema kambi hiyo iliyoanza Novemba 26, 2025 ililenga kutoa miguu na mikono bandia bure kwa wahitaji 600 na kwamba maendeleo ya zoezi hilo linaonesha mafanikio makubwa huku likitarajiwa kufikia tamati Januari 8, 2026.

“Kazi inaendelea vizuri ya ugawaji wa viungo bandia kwa wahitaji 600, zaidi ya asilimia 90 ya walengwa wamepatiwa viungo saidizi…hili ni jambo la kujivunia kwa sababu tumerejsha furaha kwa wenzetu” amesema Bi, Chandeu na kuongeza kuwa

“Wanufaika hawa walikuwa hawawezi kufanya shughuli zao za kiuchumi kikamilifu kutokana na kukosa baadhi ya viungo muhimu vikiwemo mikono na miguu, kwahiyo kwa msaada huu wanaenda kurejea katika shughuli zao za uzalishaji mali bila kikwazo”

Amebainisha kuwa hata hivyo Taasisi ya MOI inaendelea na uandikishaji wa wahitaji na hadi sasa wahitaji 1,260 wamejiandikisha, hivyo kuwa na ziada ya wahitaji 660.

“Hawa ambao hawatapata viungo katika awamu hii, Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na wadau wengine itandaa utaratibu mwingine ili kuhakikisha wahitaji waliobakia wanapatiwa viungo hivyo saidizi.
IMG-20251231-WA0060.jpg
IMG-20251231-WA0057.jpg
IMG-20251231-WA0056.jpg
 
Hawa siyo wale walipigwa risasi siku ya maandamano?wamewapiga halafu wanawapa msaada.create problem and solve.
 
Back
Top Bottom