MOI yaandaa kambi ya upasuaji kwa Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi itakayofanyika Aprili 20, 2024

MOI yaandaa kambi ya upasuaji kwa Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi itakayofanyika Aprili 20, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WhatsApp Image 2024-04-09 at 19.28.59_598ab650.jpg
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Taasisi ya MO Dewji Foundation imeandaa kambi ya upasuaji kwa Watoto 50 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi itakayofanyika 20/04/2024 katika Taasisi ya MOI.
WhatsApp Image 2024-04-09 at 19.28.57_d0a843ac.jpg

WhatsApp Image 2024-04-09 at 19.28.56_dd94e6ac.jpg
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Lemeri Mchome amesema Taasisi ya MOI imepanga kuhakikisha Watoto wengi wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo Wazi wanafikiwa na kupatiwa huduma ikiwemo na upasuaji bila gharama yoyote na kuwaomba wazazi wenye Watoto hao kufika MOI Aprili 13, 2024 kwaajili ya kliniki maalum, na wenye vigezo watafanyiwa upasuaji april 20, 2024.

“Lengo letu ni kuwafikia watoto wengi zaidi ambao hawajabahatika kupata matibabu kwahiyo tunashirikiana na Taasisi ya MO Dewji foundation kufanya kambi hii ya upasuaji kwa watoto 50 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi,” amesema Dkt. Mchome.

Dkt. Mchome ameishukuru Taasisi ya MO Dewji Foundation kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanapata huduma bora za kibingwa na kibobezi bila gharama yoyote.

Naye, Mratibu wa mradi kutoka MO Dewji, Amina Ramadhan amesema Taasisi hiyo itasaidia watoto hao 50 kabla na baada ya huduma ya upasuaji ikiwemo vipimo vitavyohitajika vya radiolojia, maabara na muendelezo wa matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (ASBATH), Suma Mwaipopo ameishukuru Taasisi ya MOI na MO Dewji foundation kwa ushirikiano wao wa kuwasidia watoto hao pia amewasihi wazazi kutoka mikoa yote wasikose kushiriki kambi hiyo.

Daktari wa ubongo wa MOI Dkt. Consolata Shayo amesema MOI imekuwa ikiwahudumia kwa ukaribu watoto hao wakiwa wodini, kwenye kliniki, vipimo na vyumba vya upasuaji hivyo amewaalika wote waliopo majumbani na mikoani waliowaficha watoto hao ndani waje kwa wingi siku ya kliniki tarehe 13/4/2024.

Meneja wa Ustawi wa amii MOI, Jumaa Almasi amesema MOI ni Taasisi ya umma ipo kwaajili ya kuhakikisha watoto hao wanapata huduma hivyo wazazi wenye watoto hao wawasiliane na MOI.
 
Hongera Serikali kwa maboresho mengi ktk sekta ya afya licha ya changamoto za hapa na pale.

Taasisi ya mifupa MOI ni taasisi yenye mapana ktk utoaji tiba kwa kuzingatia takwimu za ajali,magonjwa mtambuka yanayohitaji specialised treatment..Hivyo eneo na miundombinu ya sasa bado ni finyu lichs ya uwekezaji mkubwa na upanuzi.

Nashauri kutengwe eneo kubwa la ekari 25 mpaka 100 nje ya jiji kisha ijengwe Hospitali kubwa ya kisasa yenye huduma na vitendea kazi vya kisasa.

Gharama za matibabu MOI ni kubwa sana kwa sasa na Watanzania walio wengi wanashindwa kumudu ama kuzimudu kwa mahangaiko makubwa..Upo utaratibu wa kusamehe wagonjwa wasio na uwezo -HONGERA KWA SERIKALI YETU.

Tatizo ni hizi taasisi za Afya Muhimbili ikiwemo ni kuelemewa na madeni ya wazabuni na kupekelea huduma kuzorota..Ktk hili nadhani kunapaswa kuwa na namna sahihi ya Serikali kuongeza fungu la fedha la kulipia misamaha inayotolewa kwa wagonjwa,ndugu wa wafu wasio na uwezo mara baada ya kuhudumiwa.

Mungu ibariki Tanganyika,Zanzibar na JMT
 
Back
Top Bottom