Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeendelea kutoa huduma za kibingwa na kibobezi kupitia madaktari wake bingwa na bobezi wa mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika kambi maalum ya matibabu inayoendelea mkoani Arusha.
Wananchi wa Mkoa wa Arusha na mikoa jirani wameendelea kujitokeza kwa wingi leo, Juni 16, 2026, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ili kupata huduma za uchunguzi, ushauri na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa na bobezi wa MOI.
Kambi hiyo imeandaliwa na Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi na kuwawezesha kupata matibabu bila kulazimika kusafiri kwenda umbali mrefu.
Huduma hizo zinaendelea kutolewa bila malipo, huku wananchi wakihimizwa kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na fursa hiyo ya kupata huduma za kibingwa na kibobezi zinazotolewa na wataalamu wa MOI.