Moja kati ya matukio hodari kabisa ya jeshi la Tanzania

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
828
Reaction score
2,110
Ilikuwa siku ya Jumapili ya tar. 8 Machi, mwaka 1987, saa nane za usiku, katika viunga vya jiji la Dar es Salaam, kambi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini chini ya Chama cha ANC iliyokuwa Dakawa Morogoro, ilikuwa tayari imepika wapiganaji wa kutosha walioitwa Umkhonto-Wesizwe, ambapo palihitajika ndege ya kuwapeleka Afrika Kusini, kwenye uwanja wa vita vya ukombozi.

Mwl. Nyerere alifanya mawasiliano na viongozi wa ANC waliokuwa Afrika kusini, akiwaambia kuwa kwa sababu za kiusalama, haikutakiwa ndege ya Tanzania itue Afrika Kusini kupeleka wanajeshi hao. Chaguo la kijasusi lililikuwa ni kuazima ndege kutoka Nigeria. Kisha Mwl. Nyerere akazungumza na Rais wa Nigeria, Jenerali Ibrahim Badamasi Babangida, kwa lengo la kuomba msaada wa kupatiwa ndege.

Nyakati hizo Satelaiti ya mawasiliano ya kimataifa kwa Afrika Mashariki ilikuwa Nairobi, yaani ukitaka kupiga simu kwenda nje ya Tanzania ilikuwa lazima mawasiliano yako yafike Nairobi ndipo uunganishwe na mtu umtakae. CIA na MI6 wakanasa mawasiliano kati ya Mwl. Nyerere, Rais wa Nigeria na ANC, haraka sana wakawashtua shirika la ujasusi la BOSS. Nao BOSS halikuchelewa likachukua ndege yake iliyopakwa rangi ya kubandika ili ionekane ni ndege ya Nigeria ambapo kama saa mbili tu hivi ndege hiyo ikawa tayari ipo anga la Dar es salaam ikiomba njia ya kutua.

Lakini maofisa wa Usalama wa Tanzania walishtuka kwa sababu muda iliyochukua ndege hiyo kufika ulikuwa mfupi mno. Rubani hakushuka katika ndege. Hatua ya kwanza kabla askari wa ANC hawajatolewa mafichoni na kuletwa katika ndege, ilikuwa ni kujiridhisha kupitia ubalozi wa Nigeria. Upande wa Ubalozi walithibitishiwa ndege yao imeondoka muda mrefu Lagos, Nigeria kuja Dar es salaam, wakati upande wa mamlaka ya viwanja vya ndege ilikuwa na mawasiliano ya ndege hii iliyotua.
Katika hofu na mkanganyiko huo, ikapendekezwa rubani ashushwe na Maafisa Usalama wakatumia mbinu ya kutambua kwa lugha, wakazungumza naye kwa lugha tatu, Kiingereza, Kihausa, na Kizulu. Rubani wa ndege hiyo hakujua Kihausa bali Kiingereza na Kiz..

Kujua zaidi, Soma kitabu cha Ujasusi, #SafishaGhala kwa 30,000 tu popote ulipo unaletewa.

Nunua kwa 0715865544/ 0755865544 (Yericko Nyerere)
 
mafahari wawili mimi ngoja niweke bando la kutosha nichaji na simu kabisa
 
Daah mda ambao nimekolewa zaidi kusoma upepo huu usiokuwa wa kisulisuli ndio ghafla naambiwa ninunue kitabu daah
 
Bila shaka leo sio 1st.April!! ndege iruke kutoka Dar hadi Afrika ya Kusini kipindi hicho!!tuweni makini wakati wa kushusha uzi kama huu,au ndio yale yale ya lori lenye makomandoo wa jeshi la kikaburu eti kukamatiwa pale msamvu morogoro!!,na kwa taarifa zaidi ukweli kuhusu hivi vyama vinavyojiita vya ukombozi unaanza kujitokeza,na tuelewe kuna mchango mkubwa mno uliozima siasa za kibaguzi ndani ya SA kuliko mapambano ya silaha,jisomee kuhusu muungano wa UDF ulivyosaidia kukomesha siasa hizi,uchumi wa SA kipindi hicho,mabadiliko ya uongozi ndani ya Uingereza,na US,kilichotokea ndani ya Vita Angola.
 
Ilikuwa siku ya Jumapili ya tar. 8 Machi, mwaka 1987, saa nane za usiku, katika viunga vya jiji la Dar es Salaam, kambi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini chini ya Chama cha ANC iliyokuwa Dakawa Morogoro, ilikuwa tayari imepika wapiganaji wa kutosha walioitwa Umkhonto-Wesizwe, ambapo palihitajika ndege ya kuwapeleka Afrika Kusini, kwenye uwanja wa vita vya ukombozi.

Mwl. Nyerere alifanya mawasiliano na viongozi wa ANC waliokuwa Afrika kusini, akiwaambia kuwa kwa sababu za kiusalama, haikutakiwa ndege ya Tanzania itue Afrika Kusini kupeleka wanajeshi hao. Chaguo la kijasusi lililikuwa ni kuazima ndege kutoka Nigeria. Kisha Mwl. Nyerere akazungumza na Rais wa Nigeria, Jenerali Ibrahim Badamasi Babangida, kwa lengo la kuomba msaada wa kupatiwa ndege.

Nyakati hizo Satelaiti ya mawasiliano ya kimataifa kwa Afrika Mashariki ilikuwa Nairobi, yaani ukitaka kupiga simu kwenda nje ya Tanzania ilikuwa lazima mawasiliano yako yafike Nairobi ndipo uunganishwe na mtu umtakae. CIA na MI6 wakanasa mawasiliano kati ya Mwl. Nyerere, Rais wa Nigeria na ANC, haraka sana wakawashtua shirika la ujasusi la BOSS. Nao BOSS halikuchelewa likachukua ndege yake iliyopakwa rangi ya kubandika ili ionekane ni ndege ya Nigeria ambapo kama saa mbili tu hivi ndege hiyo ikawa tayari ipo anga la Dar es salaam ikiomba njia ya kutua.

Lakini maofisa wa Usalama wa Tanzania walishtuka kwa sababu muda iliyochukua ndege hiyo kufika ulikuwa mfupi mno. Rubani hakushuka katika ndege. Hatua ya kwanza kabla askari wa ANC hawajatolewa mafichoni na kuletwa katika ndege, ilikuwa ni kujiridhisha kupitia ubalozi wa Nigeria. Upande wa Ubalozi walithibitishiwa ndege yao imeondoka muda mrefu Lagos, Nigeria kuja Dar es salaam, wakati upande wa mamlaka ya viwanja vya ndege ilikuwa na mawasiliano ya ndege hii iliyotua.
Katika hofu na mkanganyiko huo, ikapendekezwa rubani ashushwe na Maafisa Usalama wakatumia mbinu ya kutambua kwa lugha, wakazungumza naye kwa lugha tatu, Kiingereza, Kihausa, na Kizulu. Rubani wa ndege hiyo hakujua Kihausa bali Kiingereza na Kiz..

Kujua zaidi, Soma kitabu cha Ujasusi, #SafishaGhala kwa 30,000 tu popote ulipo unaletewa.

Nunua kwa 0715865544/ 0755865544 (Yericko Nyerere)
Kumbe NI hadithi ya kubuni nilitakushagaa Sana. Tangu 1975 nilikuwa mjeda. Baada ya kumaliza shule Umbwe Sec. Sijaiwai au kushiriki.Nilikuwa Mwl kwa ANC
 
Mwalimu Nyerere was no longer at the helm in 1987! Ilikuwaje Mwalimu ndiye akawa mratibu wa operation ya kijeshi wakati wa utawala wa Rais (commander-in-chief) mwingine (A.H. Mwinyi)?
 
Kupaka rangi ndege kifanyike kwa nusu saa? Hii riwaya unafaa kufundishia chekechea
 
hadithi ya uongo, Nyerere alishang'atuka, Yericko muongo sana, naona umekopi " operation entebe" iliyofanya na waisraeli uganda
 
Hahahaaa watu wadukuzi hatari washadukua kuwa uzi una magumashi
 
Mwaka 1987 JK Nyerere alikuwa ameshang'atuka urais sasa aliyafanyaje ilihali yeye alikuwa Butyama?
Ilikuwa siku ya Jumapili ya tar. 8 Machi, mwaka 1987, saa nane za usiku, katika viunga vya jiji la Dar es Salaam, kambi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini chini ya Chama cha ANC iliyokuwa Dakawa Morogoro, ilikuwa tayari imepika wapiganaji wa kutosha walioitwa Umkhonto-Wesizwe, ambapo palihitajika ndege ya kuwapeleka Afrika Kusini, kwenye uwanja wa vita vya ukombozi.

Mwl. Nyerere alifanya mawasiliano na viongozi wa ANC waliokuwa Afrika kusini, akiwaambia kuwa kwa sababu za kiusalama, haikutakiwa ndege ya Tanzania itue Afrika Kusini kupeleka wanajeshi hao. Chaguo la kijasusi lililikuwa ni kuazima ndege kutoka Nigeria. Kisha Mwl. Nyerere akazungumza na Rais wa Nigeria, Jenerali Ibrahim Badamasi Babangida, kwa lengo la kuomba msaada wa kupatiwa ndege.

Nyakati hizo Satelaiti ya mawasiliano ya kimataifa kwa Afrika Mashariki ilikuwa Nairobi, yaani ukitaka kupiga simu kwenda nje ya Tanzania ilikuwa lazima mawasiliano yako yafike Nairobi ndipo uunganishwe na mtu umtakae. CIA na MI6 wakanasa mawasiliano kati ya Mwl. Nyerere, Rais wa Nigeria na ANC, haraka sana wakawashtua shirika la ujasusi la BOSS. Nao BOSS halikuchelewa likachukua ndege yake iliyopakwa rangi ya kubandika ili ionekane ni ndege ya Nigeria ambapo kama saa mbili tu hivi ndege hiyo ikawa tayari ipo anga la Dar es salaam ikiomba njia ya kutua.

Lakini maofisa wa Usalama wa Tanzania walishtuka kwa sababu muda iliyochukua ndege hiyo kufika ulikuwa mfupi mno. Rubani hakushuka katika ndege. Hatua ya kwanza kabla askari wa ANC hawajatolewa mafichoni na kuletwa katika ndege, ilikuwa ni kujiridhisha kupitia ubalozi wa Nigeria. Upande wa Ubalozi walithibitishiwa ndege yao imeondoka muda mrefu Lagos, Nigeria kuja Dar es salaam, wakati upande wa mamlaka ya viwanja vya ndege ilikuwa na mawasiliano ya ndege hii iliyotua.
Katika hofu na mkanganyiko huo, ikapendekezwa rubani ashushwe na Maafisa Usalama wakatumia mbinu ya kutambua kwa lugha, wakazungumza naye kwa lugha tatu, Kiingereza, Kihausa, na Kizulu. Rubani wa ndege hiyo hakujua Kihausa bali Kiingereza na Kiz..

Kujua zaidi, Soma kitabu cha Ujasusi, #SafishaGhala kwa 30,000 tu popote ulipo unaletewa.

Nunua kwa 0715865544/ 0755865544 (Yericko Nyerere)
 
tarehe tajwa mwl. alikuwa butiama analima ulezi na mtama, we unatupiga kamba hapa. na kuna ndege inabandikwa rangi kwa dakika 20? unajua ndege inatumia muda gani kutoka US hadi Dar? ni over 12hrs, wewe unaleta ngonjera za masaa 2
 
huyu kijana na hadithi zake za 'ujasusi' uchwara anawaibia watu hela zao..
ni matumaini yangu hauwadanganyi CDM na hizi ngano zako.
 
Ukisikia "story" za vijiweni ndio hizi hapa!.. Lakini swali la kujiuliza ni > Mtoa hoja hii ana lengo gani hasa?. 😳
 
Back
Top Bottom