Moja ya harusi bora kabisa hii

Swali...unaogopa maneno ya hao ndugu zake??? Mwanamke hawezi kuamua sherehe yake anataka iweje kama anategemea mfuko wa wazazi wake. Kwani wakiongea maneno na tayari mmeoana utakatika nanii au?
 
Vijana nawashauri fungeni ndoa za hivyo. Hautapata vidonda vya tumbo wala kugombana na mtu. Kama mkristo na hautaki macho mengi, funga siku za katikati ya wiki.
 
Swali...unaogopa maneno ya hao ndugu zake??? Mwanamke hawezi kuamua sherehe yake anataka iweje kama anategemea mfuko wa wazazi wake. Kwani wakiongea maneno na tayari mmeoana utakatika nanii au?
Hakuna kitu kina katika, ila mipango na mke lazima kwanza, muambiane sherehe yetu iwe ya aina hii na yeye awe na msimamo upande wa wazazi wake kwamba ana taka kitu simple, ni ndugu tuu na marafiki kadhaa basi kama 60 wanatosha
 
Nafikiri sherehe simple kama hizi ni nyie wote muamue kuanzia Sendoff mpaka harusi ila shida Wanawake nyie ndiyo hamuelewi mnataka mashindano all the time.
Watu hawajiozi wanaozwa.Ndio.maana maamuzi ya send off au ndoa iweje wazazi na ndugu na marafiki wana maamuzi yao.Send 9ff mfano huwezi.mtoa tu mtoto kienyeji.eti ohh awe Mama peke yake na mumewe wawili wanafanya send off haiwezekani na haipo hata familia iwe maskini vipi.Kifupi ni kitu kisichowezekana
 
Kama hiyo hapo million 5 maximum nahisi. Still hata kama ingekuwa millioni 7 bado ni kidogo tofauti na zile za million 18, 16 kuendelea
Very good..kwa mantiki hii, shughuli hii haitazidi watu 25....niamini mimi. Sasa usifkiri ndugu zako watafurahia..maana kumbuka wewe ndo utaamua nani awepo na nani asiwepo. Sana sana utawainclude ulozaliwa nao tu, na friends maybe 2 na upande wa kikeni. Sasa una mashangazi, wajomba ambao lazima utawaacha, usifikir watachekelea...niamin mimi. Tena afadhali utokee kwenye clan ya watu wenye elimu/uelewa lakin kama ni hiz familia zetu za kiswahili....jipange kuchukiwa na kusemwa unaringa/unajiona sana....
 
Hakuna kitu kina katika, ila mipango na mke lazima kwanza, muambiane sherehe yetu iwe ya aina hii na yeye awe na msimamo upande wa wazazi wake kwamba ana taka kitu simple, ni ndugu tuu na marafiki kadhaa basi kama 60 wanatosha
Tutarud palepale...kama mkeo ana pesa kwamba anaweza akafanya part kubwa mwenyewe basi hapo sawa. Lakin kama ana pesa na wazazi nao wanazo muache ashirikiane na wazazi wake kupanga wanachokitaka.

What I see ni kwamba sijui ni huna confidence..ile like unaona watafanya mambo makubwa then mi ndogo, wazazi wangu wataonekanaje ama watadharaulika na vitu kama.hivyo. Kipimo kikubwa cha mwanaume ni kutojali whatever that happens. Ili mradi mke anakusikiliza na kukuheshimu, basi wewe fanya kwa kadri ya uwezo wako imeisha iyo. Masuala yake atajuana mwenyewe na wazazi wake..ila wewe unaangalia mustakabali wa ya kwako unayoenda kutengeneza...basi.
 
Kiukweli ukiangalia waturuki,wazungu ndoa zao hazina mambo mengi fanyeni ndoa kwa uwezo wenu ndio kama yule aliandika wamebaki na madeni
 
Basi sioi boora sogea tukae tuu. Siwezi spend million 18 wakati nipo nyumba ya kupanga.
 
Basi sioi boora sogea tukae tuu. Siwezi spend million 18 wakati nipo nyumba ya kupanga.
Kwanini unaruhusu ndugu wakupangie maisha. Kama una milioni tano OA....ili mradi upate mwanamke atakaeweza kuhimili huu msimamo na hiki kipato. Maana unaweza pata mwanamke lakin hana msimamo na akaruhusu wazazi wake wampeleke peleke....hapo hutaweza. By the way hata hiyo sogea tukae ni gharama vile vile.....
 
Mtu MWEUSI ni mtu mwenye shida zaidi DUNIANI. Kila kitu shida
 
Hivi kumbe Millard kaoa!!!
 
Utakuwa mc wewe!! 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…