Moja ya harusi bora kabisa hii

Moja ya harusi bora kabisa hii

Mimi mwanaume naweza amua sherehe simple kama hivyo ila kama mwanamke anataka mambo makubwa aisee sasa haita pendeza, maana Sendoff mambo mengi sherehe kubwa alafu harusi simple kama hivyo, wabongo wata anza maneno tuu, aah upande wa mume wame tuangusha sana tunajuta kumpeleka mtoto wetu kule, wabahili sana mara wachoyo wale sherehe hivi je tukienda salimia watatupa hata maji kweli ?! Nafikiri sherehe simple kama hizi ni nyie wote muamue kuanzia Sendoff mpaka harusi ila shida Wanawake nyie ndiyo hamuelewi mnataka mashindano all the time.
Swali...unaogopa maneno ya hao ndugu zake??? Mwanamke hawezi kuamua sherehe yake anataka iweje kama anategemea mfuko wa wazazi wake. Kwani wakiongea maneno na tayari mmeoana utakatika nanii au?
 
Vijana nawashauri fungeni ndoa za hivyo. Hautapata vidonda vya tumbo wala kugombana na mtu. Kama mkristo na hautaki macho mengi, funga siku za katikati ya wiki.
 
Swali...unaogopa maneno ya hao ndugu zake??? Mwanamke hawezi kuamua sherehe yake anataka iweje kama anategemea mfuko wa wazazi wake. Kwani wakiongea maneno na tayari mmeoana utakatika nanii au?
Hakuna kitu kina katika, ila mipango na mke lazima kwanza, muambiane sherehe yetu iwe ya aina hii na yeye awe na msimamo upande wa wazazi wake kwamba ana taka kitu simple, ni ndugu tuu na marafiki kadhaa basi kama 60 wanatosha
 
Nafikiri sherehe simple kama hizi ni nyie wote muamue kuanzia Sendoff mpaka harusi ila shida Wanawake nyie ndiyo hamuelewi mnataka mashindano all the time.
Watu hawajiozi wanaozwa.Ndio.maana maamuzi ya send off au ndoa iweje wazazi na ndugu na marafiki wana maamuzi yao.Send 9ff mfano huwezi.mtoa tu mtoto kienyeji.eti ohh awe Mama peke yake na mumewe wawili wanafanya send off haiwezekani na haipo hata familia iwe maskini vipi.Kifupi ni kitu kisichowezekana
 
Kama hiyo hapo million 5 maximum nahisi. Still hata kama ingekuwa millioni 7 bado ni kidogo tofauti na zile za million 18, 16 kuendelea
Very good..kwa mantiki hii, shughuli hii haitazidi watu 25....niamini mimi. Sasa usifkiri ndugu zako watafurahia..maana kumbuka wewe ndo utaamua nani awepo na nani asiwepo. Sana sana utawainclude ulozaliwa nao tu, na friends maybe 2 na upande wa kikeni. Sasa una mashangazi, wajomba ambao lazima utawaacha, usifikir watachekelea...niamin mimi. Tena afadhali utokee kwenye clan ya watu wenye elimu/uelewa lakin kama ni hiz familia zetu za kiswahili....jipange kuchukiwa na kusemwa unaringa/unajiona sana....
 
Hakuna kitu kina katika, ila mipango na mke lazima kwanza, muambiane sherehe yetu iwe ya aina hii na yeye awe na msimamo upande wa wazazi wake kwamba ana taka kitu simple, ni ndugu tuu na marafiki kadhaa basi kama 60 wanatosha
Tutarud palepale...kama mkeo ana pesa kwamba anaweza akafanya part kubwa mwenyewe basi hapo sawa. Lakin kama ana pesa na wazazi nao wanazo muache ashirikiane na wazazi wake kupanga wanachokitaka.

What I see ni kwamba sijui ni huna confidence..ile like unaona watafanya mambo makubwa then mi ndogo, wazazi wangu wataonekanaje ama watadharaulika na vitu kama.hivyo. Kipimo kikubwa cha mwanaume ni kutojali whatever that happens. Ili mradi mke anakusikiliza na kukuheshimu, basi wewe fanya kwa kadri ya uwezo wako imeisha iyo. Masuala yake atajuana mwenyewe na wazazi wake..ila wewe unaangalia mustakabali wa ya kwako unayoenda kutengeneza...basi.
 
Kiukweli ukiangalia waturuki,wazungu ndoa zao hazina mambo mengi fanyeni ndoa kwa uwezo wenu ndio kama yule aliandika wamebaki na madeni
 
Very good..kwa mantiki hii, shughuli hii haitazidi watu 25....niamini mimi. Sasa usifkiri ndugu zako watafurahia..maana kumbuka wewe ndo utaamua nani awepo na nani asiwepo. Sana sana utawainclude ulozaliwa nao tu, na friends maybe 2 na upande wa kikeni. Sasa una mashangazi, wajomba ambao lazima utawaacha, usifikir watachekelea...niamin mimi. Tena afadhali utokee kwenye clan ya watu wenye elimu/uelewa lakin kama ni hiz familia zetu za kiswahili....jipange kuchukiwa na kusemwa unaringa/unajiona sana....
Basi sioi boora sogea tukae tuu. Siwezi spend million 18 wakati nipo nyumba ya kupanga.
 
Basi sioi boora sogea tukae tuu. Siwezi spend million 18 wakati nipo nyumba ya kupanga.
Kwanini unaruhusu ndugu wakupangie maisha. Kama una milioni tano OA....ili mradi upate mwanamke atakaeweza kuhimili huu msimamo na hiki kipato. Maana unaweza pata mwanamke lakin hana msimamo na akaruhusu wazazi wake wampeleke peleke....hapo hutaweza. By the way hata hiyo sogea tukae ni gharama vile vile.....
 
Mtu MWEUSI ni mtu mwenye shida zaidi DUNIANI. Kila kitu shida
 
Hizo ni harusi za jamii yenye akili sana

Harusi ya majizo mmiliki wa EFM na Lulu ilikuwa kama hizo. Jiulize Je lulu na majizo hawana watu wa kuwachangisha ?, ama hawana network ?

Harusi ya Millard Ayo ilikuwa kama hizo, je millard Ayo hana watu wa kuwachangisha ?

Jibu ni hapana. Bali ni ushahidi wa wazi kwamba ni mfano wa vijana wenye akili kubwa Tanzania

Akili zao ndizo zimewafanya watajirike wakiwa wadogo
Hivi kumbe Millard kaoa!!!
 
Sio kweli ni ya watu wapumbavu wabinafsi na wasiokuwa watu wa watu iwe majirani ,ndugu,marafiki,wanaofanya nao kazi au biashara nk

Ndoa kama hixo ni watu ambao hata ndugu hawataki wanajioza wenyewe.Wakati kawaida jamii ndio inatakiwa ikuoze .Watu wanaofurika ndio waozaji ukiona wachache jua hao sio wati wa watu kaa nao mbali ni watu wa maisha self-contained hao.
Utakuwa mc wewe!! 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom