HOJA Moja ya mambo yanayonikera ni kulipa tozo unapoingia stendi. Kwanini abiria atozwe pesa wakati haingizi pesa?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
We vipi aisee, hujanywa chai? Na kama hujanywa nani amekwambia unatakiwa kuja kutolea hasira kwangu? Pita hivi kama ni stress mimi mwenyewe nina zangu
Uache uongo..Kuingia Stendi yoyote abiria ni lazima ulipie getini kwanza Sh mia 3 bwana
 
Habari, abiria halipi ushuru stand. Ukiwa na tiketi mtandao unaingia bure. Kama huna tiketi unahesabika kama unafata huduma za stand hivyo lazima ulipe.
 
Ni kweli kuna kiingilio getini ukiwa unasafiri
 
Sasa wewe ukilalamika na wengine wafanyeje?. Wewe ni kada mtiifu unatakiwa usifie kila kitu mbona unakiuka mihiko ya chama chetu?. Jiangalia chama hakikutufundisha hivyo wakati wa kutujenga kama vijana wa chama.
Tangu lini nikawa kada? Nina kadi namba ngapi?

Ukiwa kada hutakiwa kulalamika?
 
Gari analopanda abiria linatozwa ushuru hiyo Tiketi ina kodi 18% bado kuingia kwenda kupanda hilo bus mtu alipie hela tena abiria wanaibiwa sana aisee ni Tozo moja ya kiduanzi sana kuwahi kutokea..
Ni wizi ndio maana naikataa
 
Inatakiwa ukiingia uonyeshe tiketi ya safari.
Hata hivyo stendi bado zimejaa watu wengi tu wanaoingia bila kulipa ushuru na wanasumbua abiria
Utaipataje hiyo tiketi Kwa magari ambayo hayana website za online? Ndio maana mabasi yameamua kuondoa huo usumbufu Kwa abiria wao Kwa kuwa na ofisi zao maeneo tofauti na hizo mnaita stendi.

Ile ni tozo ya wizi Haina maana kabisa.
 
Wengine wanaenda kufanya biashara, wengine kuchukua mizigo, wengine, kupokea ndugu zao, wengine, kupoteza muda, wengine kwenda chooni
Wanaoenda kwenye biashara ndio watozwe na bila shaka watakuwa wametambuliwa na kuwekewa utaratibu.

Naeenda kupanda basi au kusubiria mgeni wangu Kwa nini nitozwe? Ndio maana kampuni kubwa za mabasi zimewaondolea abiria wao huo upuuzi Kwa kuwa na vituo vyao.
 
Safari hii naona mmekosa agenda mnaanza kuichafua serikali sikivu ya Mama yetu Kipenzi Daktari Samia Suluhu Hassan. Hizo tozo ni lazima kutoa na kama hutaki kutoa hama nchi. Kwanza nimshukuru mama yetu Kipenzi Daktari msikivu, sauti ya Watanzania Hodari Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu tozo hizi ziendelee kuwepo na sisi kama Watanzania tunabubujikwa na machozi ya furaha kila mara tunapotoa hela zetu stendi kwa ajili ya kujenga taifa. Mabeberu wanaumia kuona Watanzania wazalendo wakitoa tozo wanapoingia stendi hivyo wanaanza kuwashawishi mtuharibie nchi yetu maana sisi ni tishio kubwa sana kwa uchumi wa mabeberu
 
Unalialia nini? Wewe si umeamua kuwa CHAWA? Na uchawa wako kumbe huna hata kiingilio cha kuingia stendi.

Tukisema chama na serikali yenu ni wezi na wakandamizaji nyie mnatupinga mnasema mama anaupiga mwingi.

Endeleeni na uchawa wenu
 
Kwa abiria kweli hatakiwi kutozwa lakini kama sio abiria unatakiwa ulipie sababu hatuna ustaarabu wa kutosha. Kama unapokea abiria mgeni unatakiwa uwe nje ya stendi na sio ndani.
 
Unalialia nini? Wewe si umeamua kuwa CHAWA? Na uchawa wako kumbe huna hata kiingilio cha kuingia stendi.

Tukisema chama na serikali yenu ni wezi na wakandamizaji nyie mnatupinga mnasema mama anaupiga mwingi.

Endeleeni na uchawa wenu
Lini nilikwambia Mimi ni mwana CCM? Au kuwa chawa manake nini?

Mimi ni shabiki wa SSH na hizo tozo zimekuwepo miaka yote hazijaanza Leo.

Je kuwa chawa and the likes kunafanya ufumbie macho mambo kero? Kwani unadhani Chadomo mkiwa Marais ndio Nchi itakuwa ya awali na Maziwa?

Mwisho ni kweli ameuoiga mwingi kwani uongo? Kujenga stendi Kila mkoa Kila Mji sio kupiga mwingi?

Hoja ni kwamba tozo ziondolewe Kwa abiria ni wizi na kero,tozo za kihuni hazipaswi kuwa Mapato ya Halmashauri,stendi ni Huduma abiria haendi kufanya biashara

View: https://www.instagram.com/p/DbZ7LAxDENE/?igsh=dTF4Nm81dHZ4N3Ry
 
Mimi ni shabiki wa SSH na hizo tozo zimekuwepo miaka yote hazijaanza Leo.

Je kuwa chawa and the likes kunafanya ufumbie macho mambo kero? Kwani unadhani Chadomo mkiwa Marais ndio Nchi itakuwa ya awali na Maziwa?
Kaa kimya ewe CHAWA lialia uendelee kumsifu mama, umtukuze yeye na kumwabudu yeye na serikali yake.

Kumkosoa ni kukufuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…