Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Baada ya mwaka jana chama cha ANC kupata kiasi cha asilimia 40 tu ya kura, mwaka huu wamekuja na sera ya kuwezesha kufanyika land redistribution. Kwa miaka yote wazungu wachache wa SA bado walikuwa wanashikilia asilimia 70 ya ardhi yote ya nchi hiyo. Serikali ya ANC kushindwa kuwapatia ardhi weusi walio wengi ni moja ya sababu kubwa iliyofanya waanguke vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka jana. Ili kurudisha imani kwa wananchi wamekuja na sera itakayoiwezesha serikali kuchukua ardhi kwa wachahce na kugawia walio wengi.
Mugabe naye baada ya kuona kuwa chama chake kinapoteza uungwaji mkono maeneo ya vijijini akaamua kuja na sera ya kuwapora ardhi wazungu wa Zimbabwe na kuwagawia weusi. Wote ZANU na ANC wamefanya hayo kwa sababu za kisiasa, na si kuwa wanawapenda weusi au wanawachukia wazungu.
Hapa kwetu CCM imekuwa inaenjoy sana uungwaji mkono huko vijijini. Sababu moja kubwa ni kuwa sera ya ardhi ya Tanzania inawapa fursa ya kuwa na ardhi kirahisi. Inaonekana mtu wa kijijini akiwa na ardhi inayomuwezesha kulima na kufuga anaridhika kabisa na maisha yake. Pengine CCM itakuja kosa ushawishi siku watu wa kijijini wakikosa kupata fursa ya ardhi au wakiishindwa kuishi kwa kutegeea hiyo ardhi.