Mojtaba: Jeshi pekee halitoshi kuifanya Iran iwe na Nguvu. Ataka watu waongeze kasi ya Kuzaa

Mojtaba: Jeshi pekee halitoshi kuifanya Iran iwe na Nguvu. Ataka watu waongeze kasi ya Kuzaa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
My Take
Naunga mkono hoja,watu ndio Nguvu ya Taifa kiuchumi,kijeshi na kiteknolojia.
============
Kiongozi mkuu mpya wa Iran, Mojtaba Khamenei, ameibua mjadala mkubwa kimataifa baada ya kusisitiza umuhimu wa kuongeza idadi ya watu kama mkakati wa kuimarisha nguvu ya taifa.

Kupitia ujumbe wake, Khamenei amesema mustakabali wa Iran hautategemea nguvu za kijeshi pekee, bali pia kuwa na kizazi kikubwa kitakachochochea uchumi, ulinzi na maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo imekuja wakati kiwango cha uzazi nchini humo kikiwa kimepungua hadi takribani watoto 1.7 kwa mwanamke, huku serikali ikianzisha sera na motisha mbalimbali kuhamasisha wananchi kupata watoto wengi zaidi.

Soma Pia; Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Hata hivyo, baadhi ya wananchi na wachambuzi wamekuwa wakipinga juhudi hizo wakitaka serikali kwanza kushughulikia changamoto za kiuchumi na maisha.
 
Wao wanachukua pesa zote kwenda kufadhili ugaidi halafu wanasema watu wazaane tu na huku hawa waliopo wako hoi kiuchumi. Bure kabisa.
 
Ameshaonekana au bado kajichimbia shimoni kama panya?
 
Back
Top Bottom