Momba: TARURA Yafungua Barabara Mpya ya KM 8.24 Wilayani Momba

Momba: TARURA Yafungua Barabara Mpya ya KM 8.24 Wilayani Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MOMBA: TARURA YAFUNGUA BARABARA MPYA YA KM 8.24 WILAYANI MOMBA​

Kwa mara ya kwanza wananchi wa Kata ya Mpemba na Mpande wananufaika na kufurahia matunda ya ujenzi wa barabara itakayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi na Maisha yao kwa ujumla.

Mhandisi Yusuph Shabani Meneja TARURA Wilaya ya Momba ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma amesema wamejenga barabara ya Mpande - Katenjele inayounganisha Kata hizo.

Amesema barabara hiyo ina urefu wa Km. 8.24 na tayari imekamilika na imejengwa na Mkandarasi HSS ENGINEERING kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.

"Huko nyuma barabara hii haikuwepo na wananchi wa maeneo haya ambao kimsingi wanajihusisha na shughuli za kilimo, walikuwa wanapata changamoto kubwa ya usafirishaji wa mazao yao kuyatoa maeneo ya mashambani kuyapeleka sokoni.

"Lakini sasa kama mlivyowasikia wenyewe wanatoa ushuhuda huo kwamba sasa barabara hii itawasaidia kuhakikisha mazao yao ambayo wanavuna yanafika sokoni kwa wakati”.

"Walikuwa wakipita kinjia kidogo sana, sasa tumeifungua na wanapita” Aliongeza

Mhandisi Yusuph amebainisha wana jumla ya Halmashauri mbili wanazozihudumia ambazo ni Halmashauri ya Mji Tunduma na Halmashauri ya Wilaya Momba .

"Tunduma tuna barabara zenye urefu wa Km. 230.5 na Momba Km. 649.21 jumla Km. 879.71 kama Taasisi tumekuwa na utaratibu wa kuhudumia barabara zetu kwa matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi, matenegenezo ya vipindi maalumu na miradi ya Maendeleo.

"Kimsingi sasa tunapokea bajeti kutoka maeneo mbalimbali kuna bajeti inayotokana na fedha ya Mfuko wa barabara (Road Fund), mfuko wa Jimbo(Constituency Fund), na fedha zinazotokana na tozo ya mafuta ambazo tumeanza kuzipokea toka mwaka wa fedha 2021/2022.

"Fedha hizi zimetusaidia kufanya kazi kubwa sana hasa kufungua barabara nyingi na kuzifanyia matengenezo barabara ambazo kimsingi huko nyuma zilifunguliwa lakini zilikuwa na hali mbaya.

"Katika Wilaya yetu ya Momba tuna kanda tatu yaani Mji wa Tunduma, Ukanda wa Juu (Halmashauri ya Mji wa Momba) na Ukanda wa Chini eneo ambalo ndipo ilipo Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba .

Amesema eneo hilo la ukanda wa chini ndio eneo lenye changamoto kubwa kutokana na jiografia yake kuwa na mito mingi na mikubwa inayopeleke maji katika Ziwa Rukwa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-03-21 at 13.35.09.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-21 at 13.35.09.jpeg
    218.2 KB · Views: 32
  • WhatsApp Image 2025-03-21 at 13.35.08.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-21 at 13.35.08.jpeg
    235.7 KB · Views: 30
  • WhatsApp Image 2025-03-21 at 13.35.08 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-21 at 13.35.08 (1).jpeg
    168.4 KB · Views: 37
Back
Top Bottom