Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Polisi katika Mji wa Mombasa nchini Kenya wanamshikilia kondakta wa Basi la Shule kwa madai ya kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka mitano alipokuwa akimpeleka nyumbani kutoka shule.
Mwanafunzi huyo wa Shule ya Msingi Maryjoy mjini humo alikuwa akirudishwa nyumbani, na anadaiwa kubaki peke yake kwenye basi baada ya wenzake wote kuwa wameshushwa majumbani mwao, ndipo Kondakta huyo alipotumia mwanya huo kumwingilia kingono hapo Mei 18.
“Tulimwandaa kama kawaida asubuhi, na aliporudi alipokelewa na mfanyakazi wetu ambaye aligundua kasoro katika mwendo wake,” amesema Baba wa mtoto huyo.
Baada ya ripoti ya Hospitali kuthibitisha kuingiliwa kimwili kwa mtoto huyo, mtuhumiwa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Miembeni akisubiri kupandishwa kizimbani.
Uongozi wa Shule umesema hauelewi namna tukio hilo lilivyotokea, ikidai basi liliondoka shuleni likiwa na wanafunzi 28 na waalimu 6 wa kike. Umedai kuwa haiwezekani mwanafunzi huyo kubaki peke yake kwenye basi wakati kulikuwa na wenzake waliotakiwa kushushwa majumbani baada yake.
Mzazi wa mtoto amewasihi wazazi kuwakagua watoto wao wanapotoka shule.
Chanzo: Nation