Mkurugenzi wa Usalama anaenda kuondolewa kwa kushindwa kuzuia ufisadi ?
Hujui chochote.
Toka uhuru, na zaidi kuanzia Mwinyi administration, Usalama wa Taifa unaongoza nchi hii kwa ubadhilifu, ujambazi wa mali ya umma, ule wa halali ya kupeana ( employmemt perks) na ujambazi wa wazi wazi (blatant embezzlement). Haya yote hufanyika chini ya pua ya Ikulu, ambayo ina fungu lisilohasibiwa, black budget.
Wakurugenzi Wakuu wa Usalama, na wale wa idara ndani ya TISS tunawajua binafsi, tumeishi nao, ni baba zetu, ni baba wakwe, ni wajomba, ni family friends. Ujangili wao upo machoni petu.
Kwa wewe kusema Mkurugenzi anaenda kuondolewa kwa sababu ya kushindwa kusimamia kukithiri kwa wizi sehemu mbali mbali serikalini inaonyesha hujui chochote cha TISS wa nchi hii, wala ofisi kuu yao, IKULU.
Mtu asiyejali wizi anawezaje kumfuta kazi mwizi kwa kushindwa kupambana na wizi ?