Disruptor1
Senior Member
- Aug 9, 2022
- 139
- 388
Daah maisha yanatupitisha kwenye moments ambazo ni ngumu kusahaulika. Moja ya moment ambayo sitakuja kuisahau ni jinsi Bank ya Finca ilivotufanyia somba somba alooo.
Nakumbuka mwaka 2010 tumekaa ofisini na mama (ofisi ya kushona nguo maana wazazi wangu wote ni mafundi kushona na kipindi hicho walikuwa wanatumia ofisi moja ambapo mama ni mavazi ya ke na mzee mavazi ya me).Tukashangaa kuna gari imeandikwa finca imefika pamoja Canter size ya kati hivi,wale jamaa walijitambulisha kisha wakatuonyesha makaratasi yalikuwa na majina ya mzee na sahihi zake kisha wakaomba tuwapishe wafanye kazi yao.
Aisee hatukuamini wale jama walianza kupikia mashine za mle ofisini,walipakia meza,tundua vitambaa,vitenge,wax na kanga zote.Walichukua kabati la kuuzia nyuzi,zipu,ruksi na vidude vingne kama lilivyo. Walivyotoka hapo wakaomba mama aingie kwenye gari na mimi nikachoma ndani wakatueleza tunaenda kwenye kiwanja chenu.
Daah tulivofika kule kiwanja kilikuwa na msingi tayari kikapigwa mnada mbele ya macho yetu. Daah siku ile mama machozi talimtoka ikabidi ampigie mzee kumuuliza vipi ndo mzee akamjibu kuwa alikopa na hela amemfungulia duka la vipodozi mchepu kashindwa kuliendesha kala mtaji af kasepa.
Mama ikabidi amuulize ko ukowapi saa hivi,mzee bila aibu akajibu nipo nakodi gari inakuja kupakia vitu vya ndani tunarudi nyumba ya kijijini kulima.
Aisee siku ile ilikuwa mpalangano yaani hadi tunakuja kusettle mimi na dogo tushahamishwa na shule ilitumia mda sana.
Bank ya kwanza kuijua ilikuwa Finca kisa hii issue
ILA MZEE ALIJUA KUTUUZA AISEE