Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Wakati vyama na wadau wakianza kujiweka mguu sawa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kina hakika wa kupata ushindi wa kishindo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu (CCM-Bara), John Mongella baada ya kupokea taarita ya utekelezaji wa Mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao kwa uhakika wa ushindi wa kishindo.
Akizungumza baada ya kupokea utekelezaji wa llani ya CCM mwaka 2020-2024 kutoka Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga, Mongella amesema kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani chama hicho kina uhakika wa ushindi na kwamba waendelee na kasi ya kuleta mendeleo ili kero zote ziishe.
Mongella ambaye yupo kwenye ziara ya siku saba mkoani Shinyanga kama mlezi wa mkoa huo, pia amewataka viongozi wa ngazi ya mkoa na hadi mitaa kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuboresha maisha ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuleta pembejeo za kilimo kwa wakati, na maafisa ugani kutoa elimu kwa wakulima.
Akiwa mkoani humo, Mongella amepongeza juhudi za Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa barabara, hospitali na shule na kusema kuwa juhudi hizo zimeongeza imani ya wananchi kwa chama hicho.
Amesema Serikali inatekeleza kwa vitendo ahadi zake na kwamba wananchi wanaona mabadiliko.
Katika ziara yake, Mongella atatembelea Shinyanga Mjini, Kahama, Msalala, Ushetu, Shinyanga Vijijini na kufanya mikutano ya ndani na hadhara.
SOURCE: MWANANCHI