Monica maisha yakuwa sehemu yake alipambana lakini alizidiwa na saikolojia .

Monica maisha yakuwa sehemu yake alipambana lakini alizidiwa na saikolojia .

Course Coordinator

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2019
Posts
1,738
Reaction score
3,236
Story ni ndefu lakini itakufundisha

Wiki mbili zilizopita nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu mmoja...hii ilikuwa ni tofauti kidogo kutokana na ukweli kwamba tulikaa muda mrefu bila kuwasiliana. Ni rafiki yangu wa shule ,tulisoma nae shule moja na alikuwa mrembo tangu nikiwa mdogo nilimuona mrembo sana.jina lake aliitwa Monica na tulikuwa tunatokea mtaa mmoja,kwa umbo yeye alinizidi kidogo urefu japo umri tulikuwa sawa labda miezi tu ya kuzaliwa tulipishana.
Wakati tunaanza form one walimu wenye tamaa walianza kumfuatilia si unajua tena watoto wanaotokea kijijini wengi wao huchomoza chuchu wakiwa wadogo kutokana na kubalehe mapema kwa kazi mbalimbali zaidi ni warembo wasioonekana ...shule tuliosoma ilikuwa ni ya dini(boys and girls) na wasichana walikuwa wachache sababu kila darasa lazima ufaulu kwa wastani mfano form ilikuwa 30 kwa girls boys 35,form two girls 35,boys 41 had form three 41 kwa 59 boys ,hivyo kuwepo kupelekea wanachana-wasichana wengi kuacha au kuhama ,so kutoka na uchache wa wasichana form one walikuwa wanakoodolewa macho na form two -four hadi walimu wa kujitolea ,nilikuwa najitahidi kumlinda kadiri navyoweza mara nyingi nilikuwa ninatembea nae hasa wakati wa kutafuta kuni, kutafuta maji,kujisomea evening class yani ni kumlinda dhidi ya vibaka.

In short sikupenda awe na mpenzi sijui wivu.sasa wakati tunaendelea na masomo alikuja mjomba wake kujitolea kufundisha baada ya kumaliza degree yake pale Arusha University ,hivyo monica ikabidi atoke Boarding aamie day kwa mjomba ake ,hivyo kuna muda alikuwa haji shule basi najipenyeza niende kumuulizia na kutaka kujua kama yupo safe mbona hujaja darasani,manake nilipokuwa simuoni class hata concentration ilikuwa inapotea kabisa ,sijui kumpenda, I was a young to know that....

Siku zimeenda hadi kidato cha tatu, tulivyofungua tu hivi muhula wa kwanza hakuja shule kama wiki moja hivi nilipoenda kwa mwalimu kwa kujipenyeza penyeza sikumuona ,nikamuuliza rafiki yake anaitwa Grace nae akasema hajamuona, labda alienda likizo kwa shangaz zake Bukoba, sikufuatilia sana manake nisingeweza kum-face mjomba wake ambae ni mwalimu na kumuuliza Monica yuko wapi!!?

Baada ya wiki moja alikuja shuleni na alikuwa amekonda sana zaidi hakuwa na furaha kama Monica niliyekuwa namjua, nilijaribu kupiga nae story ila bado lile tabasamu sikuliona kabisa ,ila akaniahidi kuwa angenambia tu ,baada ya siku kadhaa hivi kupita aliniandikia barua ilisomeka hivi ..rafiki yangu Charles najua unatambua urafki wangu kwako ulivyo naomba unisamehe kwani nimekosea mbele za Mungu nilipata mimba nikaenda kuitoa kienyeji huko mtaani nasikitika kuwa siwezi kukuambia ujauzito nilioutoa nilipewa na nani.Niombee kwa Mungu anisamehe ,basi nami nikamwandikia barua nikamjibu kwanza pole naandika barua hii nikiwa nalia machozi..hivi unamkumbuka Neema mtoto wa mchungaji wetu aliyepata ujauzito akiwa form akaenda kuutoa akafariki,kama wee ni rafiki yangu kweli nambie ukweli .

.Baadae tulivyoonana hakuwa tena na furaha kama kawaida
Tulivyofika kadato cha nne alikuwa amekwisha sahau kidogo ile dhiki na maisha yakaendlea kama kawaida...tulivyomaliza form four matokeo yalitoka bahati nzuri mimi nilienda A level na yeye akaenda zake chuo cha ualimu lakini hakumaliza, dunia duara akaanza kuzunguka na kutafuta maisha ..Baada ya siku kadhaa kupita nikasikia ameolewa na taita mmoja pale skan yule jamaa alikuwa na pesa sio nyingi kama za Mo ila hakuwa na njaa ila hakuna aliyekuwa anajua biashara zake wengine walikuwa wanasema ni jambazi wengine ni tapeli kila mtu lwake,wengine alichukua mali za babake mdogo alikuwa rubani akamwachia basi hakuna aliyewahi kuthibitisha kingekuwa kipindi hiki tungesema ni freemason ...
Mwaka 2010 huyu taita alikufa kwa ajali wengine wanasema washikaji walimlengesha baada ya kuzinguana ma-deal yao. Ila alimwacha Monica na watoto wawili na hata baada ya huyo mmewe kafariki ndoa yao ilikuwa imeingia doa na kuamua kupambana kivyake, kinachosikitisha ni kwamba kabla ya kutengana huyo taita Monica tayari alikuwa na HIV+ na aliambukizwa na huyo mmewe kwa maelezo yake mwenyewe aliniambia "yule baradhuli aliniletea magonjwa" lakini pia mateso ya kupigwa na matusi ya mmewe yalichochea kumtengana na mmewe zaidi alikuwa anapambana na ndoa pamoja na kulea watoto wake wawili.shida juu ya shida

Monica baada ya kugundua ni mgonjwa alienda Marie stopes kwa ajili ya kupata ushauri nasaha na kuanza dozi, katika kuachika kwenye ndoa yake mmewe alimpatia milioni 2 kama pesa ya kulea watoto na kuanza maisha yake "zimwi likujualo halikuli ukakwisha "...na kuna usemi wa baniani mbaya kiatu chake dawa:..Basi Monica akawa anafuata vitenge nchi jirani Kenya na Uganda anakuja kuwakopesha akina mama pale kitaani kwetu na mara chache nilikuwa namkumbusha kufuata dawa kila mwezi.Kuna kipindi alinambia amechoka amechoka kuishi na amechoka kumeza madawa kila siku ,nilimsihi ameze dawa na kuna watu huwa wanatoa shuhuda wameishi na HIV kwa muda mrefu tu, usichoke Monica wanao bado ni wadogo kiasi hicho, kumbe alimaanisha ni kweli Monica alikuwa amechoka kumeza dawa, aliona mtaji alokusanya unatosha kuwakuza wanae.
Monica aliacha kumeza dawa ,akawapeleka watoto wake kwao na babu yake kizaa mama ,kiwanja alichonunua akaandika majina ya watoto wake na kuwaanzishia junior account kisha akaachana na umezaji wa dawa ,akaacha mwili wake ushambuliwe na virusi baada ya siku kadhaa alinipigia simu niende kwa ajili ya maongezi moyo ulipiga paaa
Monica alinambia Chalz usipokuja kwenye msiba wangu usihudhurie ,nilishtuka kidogo kwa maneno yake nilikuwa sina jinsi niliamua kwenda kumuona kama alivyoniomba..Monica alikuwa amechoka sana ,nilipomwangalia nilijikuta nalia, hakunipa nafsi ya kumlilia alisema hajafa akanambia siku akifa ninyamaze nisilie ila niomboleze, alinambia nimskilize na nimsamehe kwa nini ameamua kufupisha safari yake iwe fupi kwa kuacha dawa za kufubaza HIV, alinambia kuwa Chaz sio kwamba nimeamua kuwaacha wanangu kwa makusudi, ila nimechoka kuishi naumia na kuteseka tatzo sio UKIMWI, hapo akanisimlia kitu kilichofanya niandike uzi huu.
kumbe katika safari zake za kibiashara na kuleta vitenge yupo Bwana mmoja aliomba wafanye biashara nae hakuona shida akakubali ,kumbe lengo lake halikuwa biashara, siku moja wakati wanahesabu mzigo kwa yule Bwana ambae ni mkongomani kuna watu watatu(njemba) waligonga mlango na wakafunguliwa na waliingia wanaume watatu na mwanamke mmoja ambae Monica alikuwa hamfahamu..wakati wanashangaa shangaa wale jemba watatu wakamkaba yule mwanamke akatoa maneno kwamba "hawezi kubali nyota yake ipotee kwa sababu ya malaya mmoja mshenzi " shughulikeni vijana mbaya zaidi waliondoka na mzigo wa milioni 9 pamoja na vitenge vyake..yote kwa yote akanieleza ukweli kuwa ile mimba aliyoipata akiwa form three alibakwa na mjomba wake (yule mwalimu wa kujitolea) halafu yule mjomba wake nae alikujaga kunywa sumu badae kwa sababu lile tendo lilikuwa limrudia kichwani.Tutaonana Chalz kama ni jehanamu au kanani..

Poleni kwa wana jamii forum wote wanaopitia magumu kama ya Monica ,poleni akina dada msikate tamaa ya maisha..Mungu analofungu lenu.
 
Inasikitisha sana!but sijajua Monica bado mzima au amekufa?kama bado mzima ni jambo la kushukuru na pole sana,chengine hapo ulipoandika jina “Chalz” umenikumbusha workmate wangu akipenda kujiita hivyo tulimpoteza 28 April 2020 kwa vidonda vya tumbo.

Mungu awarehemu marehemu wote wapumzike kwa amani.
 
Monica. Kuna kadada kalinipigia simu kakidai kanaitwa monoca eti kakasema kamekosea namba saa 9 usiku.
Na kakanipa angalizo kuwa nisikapigie mchana bali katanitafuta yeye mwenyewe kesho yake usiku kama ule pia.
Na mbaya zaidi kalinipa masharti mpaka nikaamua kufuta
zile namba kadada kalikuwa na mikwala hako.
Kalikuwa kanatumia voda
Huu uzi umenifanya nikumbuke lile tukio aisee sinto sahau
 
Monica. Kuna kadada kalinipigia simu kakidai kanaitwa monoca eti kakasema kamekosea namba saa 9 usiku.
Na kakanipa angalizo kuwa nisikapigie mchana bali katanitafuta yeye mwenyewe kesho yake usiku kama ule pia.
Na mbaya zaidi kalinipa masharti mpaka nikaamua kufuta
zile namba kadada kalikuwa na mikwala hako.
Kalikuwa kanatumia voda
Huu uzi umenifanya nikumbuke lile tukio aisee sinto sahau
Kalikuwa kafanyakazi ka benk hako. Kalidhani na wewe unataka mkopo!!!!
 
Majina ya Monica ni Wanawake waliojaliwa uzuri wa Ajabu na wanajali sana lakini Shetani amewaandama hao hatari. Hata mimi nina Ushuhuda nao.
 
Inasikitisha sana!but sijajua Monica bado mzima au amekufa?kama bado mzima ni jambo la kushukuru na pole sana,chengine hapo ulipoandika jina “Chalz” umenikumbusha workmate wangu akipenda kujiita hivyo tulimpoteza 28 April 2020 kwa vidonda vya tumbo.

Mungu awarehemu marehemu wote wapumzike kwa amani.
Amina..Monica tulimzika wiki iliyopita4
 
Back
Top Bottom