Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Mwanasiasa

Wewe unataka Pombe Magufuli ajiunge na Chadema Eh. ....................................................Kwa nini usiwasiliane nae kuliko kuandika humu. Hizo nchi ulizozitaja sidhani kama ni mfano mzuri wa demokrasia katika Afrika and For your information I think Magufuli is in a better position to judge his own destiny.
 
Mwanasiasa

Hizo nchi ulizozitaja sidhani kama ni mfano mzuri wa demokrasia katika Afrika and For your information I think Magufuli is in a better position to judge his own destiny.

Sasa kama Ghana na Senegal sio mfano mzuri wa demokrasia Afrika, basi hatuna mfano kabisa!
 
Ipo nchi moja ambayo inasifiwa - Botswana
 
WAHESHIMIWA WANA JAMBO EBU NAOMBA MUDA WENU KAMA DAKIKA 10-15 HIVI ILI MUWEZE KUSOMA HII ARTICLE KIDOGO.. NAAMINI HAKUNA ANAYEONEWA !!

HAKUNA anayeweza kukana ukweli kuwa Waziri John Magufuli ni mchapa kazi. Hii inatokana na rekodi aliyojiwekea kwa takribani miaka 12 tangu alipokuwa Naibu Waziri wa Ujenzi kati ya mwaka 1995-2000, Waziri wa Ujenzi 2000 hadi 2005 na sasa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Katika kipindi hicho chote alichofanya kazi, Magufuli ameweza kuonyesha kwamba anaweza kuwajibika. Tunakumbuka jinsi alivyosimamia usajili wa magari na mitambo ya serikali iliyokuwa inatumiwa kwa maslahi binafsi.

Tunamkumbuka Magufuli alivyopambana pengine hata na wakubwa wenzake ndani ya serikali, akionyesha ni jinsi gani anataka kusimamia haki, sheria na taratibu. Ni Magufuli huyu huyu alitangaza kufutwa kwa makandarasi zaidi ya 3,000, ambao alisema walikuwa wameshindwa kukidhi sheria inayowatambua.

Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wachache wa nchi hii wanaoweza kukumbukwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukumbuka takwimu muhimu za barabara alizokuwa akisimamia, wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi. Magufuli hata kama ungemwamsha usingizini, angeweza kutaja urefu wa kila barabara iliyokuwa ikijengwa, inajengwa na kampuni gani, nani ni mshauri (consultant), itagharimu kiasi gani cha fedha na hata itakamilika lini. Magufuli alikuwa na uwezo wa kukumbuka vitu vyote hivyo kwa kichwa.

Huu ni ushahidi kwamba kiongozi huyu alikuwa anafanya kazi yake vizuri, hivyo halikuwa jambo la ajabu mchambuzi wa mambo ya kijamii na kisiasa, marehemu Bugingo kumpachika jina la Mtakwimu.

Alimpachika jina hilo baada ya kumsoma katika makala moja ndefu aliyofanya mahojiano na Salva Rweyemamu wa gazeti la Rai. Katika makala hiyo, mwandishi alisema kwamba Magufuli aliweza kutoa takwimu za barabara zote kuu nchini zilizokuwa zikisimamiwa na wizara yake bila kusoma mahali.

Hata hivyo, ni katika makala hiyo, kasoro moja muhimu ya Magufuli ilijionyesha, jinsi alivyoshughulikia suala zima la uuzaji wa nyumba za serikali. Ingawa hakuweza kujenga hoja ya msingi sana katika makala hiyo kuhusu uuzwaji wa nyumba hizo, mfumo wa uuzaji uliotumika, na hasa swali la kwanini nyumba hizo ziuzwe? Hapa ukawa mwanzo wa kudadisi utendaji wake na uadilifu sawia!

Hivi karibuni gazeti hilo hilo (Rai), lilikuja kubainisha mambo fulani kuhusu nyumba ambayo Magufuli alihusika nayo na kwa hakika hadi leo hajaweza kusema lolote kuhusu ukweli wa nyumba hizo ambazo anadaiwa kujipendelea mwenyewe akiwa kiongozi wa serikali. Kwamba kumbe naye ana kile Wazungu wanachosema ‘dark side’.

Lakini lililofurahisha hapa, kama ambavyo amekuwa akilalamika wakati wote kwamba kuna watu wanamwonea wivu; ni maadui wake; hawamtaki, wanataka kumuua hali ambayo iliilazimu serikali ya awamu ya tatu kumwekea ulinzi wa ziada hadi ulipokuja kuondolewa na awamu ya nne, hata sasa bado ana visingizo vya namna hiyo, kuwa anaonewa kwa sababu ya utendaji wake hata kama atakuwa anahojiwa kuhusu kukosea kwake. Ndiyo, anaweza kukosea kwani yeye ni binadamu wa kawaida tu licha ya uwezo wake wa kukariri.

Safari hii suala la nyumba likafunuliwa na Rai, Baada ya Rai kumgusa tu kidogo kuhusu nyumba hizo, Magufuli alikimbilia polisi kuwashitaki wahariri wawili wa Habari Corporation, John Bwire na Muhingo Rweyemamu.

Kwamba wahariri hao wakitumia tu kalamu zao kujua kilichomsibu hata akajipendelea katika ununuzi wa nyumba za serikali, yeye akasema waandishi hao wasiomiliki silaha ya aina yoyote mbali ya kalamu zao tu, eti wanataka kumuua kwa sababu wamehoji kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali ambazo amehusika kama kiongozi wa umma. Kesi hii hadi sasa haijulikani majaliwa yake, isipokuwa wahariri hao walihojiwa na polisi kuhusu kutaka kumuua Magufuli!

Hili likiwa halijafutika vichwani mwa watu, karibuni hapa imeibuka hoja ya baa ya Rose Garden, iliyoko Barabara ya Garden eneo la Mikocheni.

Sakata hili limemuweka Magufuli kwenye mgongano mkubwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Mgogoro huo unaodaiwa kuwa ulianza mwaka 2004, wakati huo Magufuli akiwa Ujenzi, umeingia sura mpya kwa sababu moja tu, kwamba juhudi zote za Manispaa ya Kinondoni ya kutaka sheria na taratibu za mipango miji ifuatwe, zimetupiliwa mbali na Magufuli, na baada ya kufanya hivyo analia kwamba kuna watu wanamwandama kisiasa.

Suala lenyewe kama lilivyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima Jumapili Februari 25, 2007, ni mgogoro wa baa ya Rose Garden, ambayo inaelezwa kumilikishwa kiwanja juu ya eneo la hifadhi ya barabara, Waziri Magufuli anaelezwa kuhalalisha kiwanja hicho licha ya kwamba kwa muda wote tangu mwaka 2004 Manispaa ya Kinondoni ilikwisha kusema wazi kwamba ni eneo la hifadhi ya barabara.

Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni lilitoa tamko kwamba baa ya Rose Garden ipo kwenye eneo la hifadhi ya barabara na hivyo itabomolewa, lakini Waziri Magufuli anasema mwenye baa hiyo amemilikishwa kihalali eneo hilo na hivyo yeyote atakayembughudhi atawajibika kumlipa fidia.

Sakata hili hasa linaanzia wapi? Mwaka 1995 mwenye baa ya Rose Garden aliomba kibali kwa Kampuni ya Simu ili aendeshe biashara ya maua mbele ya eneo lao, ambalo ni kiwanda cha kuchapa (Printing Unit) cha TTCL. Aliruhusiwa na kuendesha biashara hiyo ya maua na miche ya miti.

Baadaye alijenga kibanda na kuanza kuendesha baa, kisha baadaye viwanja vikapimwa eneo hilo, ambalo kimsingi ni hifadhi ya barabara, lakini pia ni eneo la mbele la viwanja namba 171/5, 717/3 na 717/4, ambavyo ni sehemu ya kilipokuwa Kiwanda cha Printing Unit.

Baada ya kupimwa viwanja sehemu hiyo kijanja, vyombo vya serikali vilishtuka, na kushauri vifutwe na asimilikishwe mtu. Miongoni mwa vyombo vya serikali vilivyopendekeza kufutwa kwa viwanja hivyo, ambavyo vilipimwa bila kufuata taratibu na sheria za upimaji, ni pamoja na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Manispaa ya Kinondoni; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam; lakini juu ya yote ni ukweli uliothibitika baadaye kwamba, eneo hilo lililobuniwa viwanja 948, 949, 950 na 951, kimsingi vililazimishwa hapo na maofisa wa ardhi wa Kinondoni ambao hawakufuata taratibu za upimaji.

Mawasiliano ya kiofisi kati ya Manispaa ya Kinondoni na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, yapo kuthibitisha ukweli huu hata kabla ya Magufuli kuteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo Januari 4, mwaka jana.

Ninaamini Waziri Magufuli alijua kwamba kiwanja hicho cha Rose Garden kilikuwa na mgogoro, na alijua wazi kabisa kwamba kulikuwa na kesi mahakamani kuhusu kiwanja hicho, na kwa hakika kabisa alijua watangulizi wake katika wizara hiyo walikwisha kutambua matatizo ya kiwanja hicho, ndiyo maana michoro yake (plan) ilipendekezwa kufutwa sambamba na hivyo vingine, yaani viwanja namba 948, 949, 950 na 951.

Haya Magufuli aliyajua, lakini mwaka jana akiwa amekaa wizarani hapo kwa takribani miwezi sita tu, aliamua kuruhusu umilikishwaji wa kiwanja chenye mgogoro bila hata kutaka kupata taarifa za suala hilo kutoka Manispaa ya Kinondoni. Uamuzi huo umezua mgogoro wa kiutendaji baina yake mwenyewe na mamlaka nyingine za serikali kama manispaa na hata watu wengine wenye maslahi na eneo hilo, kwa sababu wapo hapo kisheria.

Baada ya kuibuka yote haya, Magufuli, ambaye kama ilivyoelezwa hapo juu kwamba ni mchapakazi, amerejea moja kwa moja kwenye ile ngome yake ya ‘kulia’ kila anapoelezwa awajibike kwa maamuzi yake mengine ambayo si mazuri.

Safari hii hoja inayojengwa hapa, eti ni ya kummaliza kisiasa! Yaani kisiasa maana yake nini? Yaani anamalizwa na Manispaa ya Kinondoni ili wapate kiti chake? Kwani nani katika madiwani wa Kinondoni anatoka Biharamulo ili ielezwe kwamba wanataka jimbo lake la uchaguzi?

Kwani Magufuli si alipita bila kupingwa, hata kama kuna mtu alikataliwa kupokewa kwa fomu zake ndani ya CCM? Mizengwe ya ajabu jimboni kwa Waziri Magufuli!

Katika mgogoro wa kiwanja cha Rose Garden, ni lazima Waziri Magufuli atambue kwamba amevurunda kama ifuatavyo:

Moja, amepuuza mamlaka nyingine za serikali ambazo zilifanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Pili, ni lazima ajue kwamba pamoja na kujua kwamba suala la kiwanja hicho lilikuwa mahakamani, alishindwa kuheshimu uhuru wa mahakama na hivyo kuchukua hatua ambazo zilifanya shauri lililokuwa mahakamani kupoteza maana.

Tatu, kwa maamuzi hayo ya kutambua kiwanja hicho na kukipa hati, sasa amefanya kiwanja namba 717/4 kiwe kisiwa ambacho hakiwezi kufikika kabisa.

Nne, muhimu zaidi sasa waziri anafungua ukurasa mpya kwamba watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya barabara nchini kote, watakuwa na haki ya kumilikishwa viwanja hivyo - amejenga precedent.

Pamoja na haya yote, sasa Magufuli inabidi akiri kwamba wale wakazi wa Ubungo, tena masikini wa kutupwa, aliosimamia wakabomolewa nyumba zao ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo hadi Mbezi Luis, aliwaonea na sasa anawajibika kuwaomba radhi kwa sababu eneo la hifadhi ya barabara linaweza kumilikishwa mtu, kwani hata pale Ubungo Kibo walikuwako watu waliokuwa na hati za kumilikishwa viwanja vyao.

Kama Magufuli hawezi kuomba radhi, anachofanya sasa kwamba eti anafanyiwa vita ya kisiasa, ni sawa na machozi ya mamba, tunamwomba aendelee kusimamia haki na sheria za matumizi ya ardhi kama alivyofanya akiwa Ujenzi, sheria ya ardhi ni moja tu, tunamshauri afikiri upya.

Maamuzi kama haya hayasaidii kujenga nchi wala kutanda kwa utawala bora na matumzi mazuri ya ardhi kwa maendeleo ya taifa hili.


HAKUNA ANAYEONEWA !! SASA BASI, MZEE MWANAKIJIJI KAMA UNGEKUWA DAR NA UNGECHAPISHA MADA YAKO ILE YA UUZAJI NYUMBA ULIOFANYWA NA MAGUFULI, NADHANI KICHWA CHA HABARI KILIKUWA "JE MAGUFULI NI MCHAPAKAZI AU NA YEYE NI MJANJA MWINGINE" SOMETHING LIKE THAT, NADHANI UNAJUWA NINI KINGEKUTOKEA...............
 
Kada Mpinzani,
Nimeisoma makala yako kwa makini. Nimeisoma yote. Basi kama hayo usemayo ni kweli, mimi ningependa sheria ichukue mkondo wake. Sheria isiingiliwe na yeyote hata kama ana sifa alizo nazo Magufuli. Ukweli ni ukweli tu hauwezi kupindwapindwa.
 
KadaMpinzani

Mimi naona unazunguka wakati hutaki kujibu issues ukurasa wa 9 (http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1797&page=9) nilikuuliza maswali lakini ukasema watu wanakutishia, lakini baada ya kurudi unajifanya kwamba hujayaona tukuelewe vipi? Narudia tena hapa chini ili ujibu hii issue ili tuendelee kukata issues hapa:

Maneno ya waziri Magufuli ni haya hapa:

`Namshangaa mmliki wa mgahawa wa Rose Garden kwa kutowashtaki mahakamani watu wanaomkwaza kufanya kazi zake? Hata akienda mahakamani, mimi na Kamishna wa Ardhi ni mashahidi wake,`alisisitiza.

Pia Waziri Magufuli alisema ni Wizara pekee iliyopewa mamlaka kisheria ya kuidhinisha matumizi ya ardhi nchini kote.

`Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999, inampa Waziri wa Ardhi mamlaka ya kuidhinisha au kubadili matumizi ya ardhi katika vijiji na miji yote nchini, hivyo hata kama ningefanya hivyo, bado ningefanya kwa mujibu wa sheria hiyo,` alisema.

Sasa angalia wewe unavyosema

magufuli anakwambia yeye kama waziri ana protection ya kubadilisha cheti chochote "kama waziri", mhm, here he goes ! sasa now we know inakuwaje akina richmonduli wanapata ulaji eehh, je huyo pm si ndio atatumia mamlaka yake yoooote ahakikishe anakula ulaji ! mheshimiwa magufuli angalia unachosema, utatoa siri zako bure bila ya kukusudia mwenyewe, duh halafu huyu braza 'gufuli nasikia aliwafukuza wafanyakazi wa wizara yake kwa tuhuma kwamba wanatoa siri za wizara yake juu ya RG !!

Vipi unausongo na Magufuli?

Kama hutaki kujibu hili where is your credibility?
 
hiyo article sijaandika mimi, iliandikwa na waandishi wa bongo.

source:www.freemedia.co.tz

dua, labda swali lako sikuliona na sio kwamba sitaki kujibu. swali ni lipi ? na kama silijui au sina jibu kwa nini nifiche kwamba sijui ? mie binadamu kama wewe, na mtu atakuwa jasiri kukubali ukweli, hivyo kama unadhani siwezi kujibu na kama kweli siwezi nitakwambia siwezi ! NI KWELI WATU WALINITISHA NA HIYO HAIUSIANI KABISA NA SWALI LAKO ( USIONE NIMESEMA HIVYO ILI KUKIMBIA SWALI, HAPANA ) otherwise tuendelee kukata ishu, na sina usongo na magufuli ila nimeona article ni interesting ndio nikaamua kuileta hapa, najua baadhi ya watu wanachukia ninapopost kitu ( sijui kwa kutokukubaliana na saa nyingine hata sijui lakini kati ya hao watu wewe sio mmoja wao Dua )

endelea...........
 
kadaMpinzani

24th February 2007, 12:26 AM
KadaMpinzani
Member Join Date: Wed Jan 2007
Posts: 75
Rep Power: 21

magufuli anakwambia yeye kama waziri ana protection ya kubadilisha cheti chochote "kama waziri", mhm, here he goes ! sasa now we know inakuwaje akina richmonduli wanapata ulaji eehh, je huyo pm si ndio atatumia mamlaka yake yoooote ahakikishe anakula ulaji ! mheshimiwa magufuli angalia unachosema, utatoa siri zako bure bila ya kukusudia mwenyewe, duh halafu huyu braza 'gufuli nasikia aliwafukuza wafanyakazi wa wizara yake kwa tuhuma kwamba wanatoa siri za wizara yake juu ya RG !!

Today
Today, 04:08 AM
KadaMpinzani
Member Join Date: Wed Jan 2007
Posts: 75
Rep Power: 21

hiyo article sijaandika mimi, iliandikwa na waandishi wa bongo.

source:www.freemedia.co.tz

Sasa leo imekuwa ya waandishi wa Tanzania. Hatutaki majungu hapa na msemakweli ni mpenzi wa Mungu. Kama kweli uliitoa huko freemedia kwa nini huku-quote? Na hii ya leo umeitoa wapi? Wewe kubali unaleta wrong information hapa kwa agenda zako.

Swali ni kwamba information uliyokuwa umeleta ni wrong?
 
sawa Dua naleta wrong info kupotosha wanajambo ur 101% right, kadampinzani 0. wewe ndio associated press (ap) wa jf ur always right !!

Na majungu, mie sina majungu ! nenda freemedia angalia sehemu ya nakala za leo, na zilizopita ili uone !!

dua=AP
 
Kada Mpinzani

Soma hii habari hala linganisha ni hiyo yako:

Magufuli awekwa kikaangoni tena
na Mwandishi Wetu

MGOGORO wa kiwanja ilipojengwa baa maarufu ya Rose Garden jijini Dar es Salaam, umeanza kubadilika na kuchukua sura inayoonyesha jitihada za baadhi ya wakubwa serikalini kuutumia kumkaanga Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli.

Mpango huo ambao tayari unaonekana kuanza kuiva umemfanya waziri huyo kujiandaa kukabiliana na kile ambacho watu wake wa karibu wanakielezea kuwa ni mashambulizi ya wazi wazi dhidi ya mwanasiasa huyo aliyepata umaarufu mkubwa enzi za Serikali ya Awamu ya Tatu. Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Manispaa ya Kinondoni vimeieleza Tanzania Daima kwamba, Magufuli anawekwa katika wakati mgumu kwa sababu ya uamuzi wake wa kumlinda mmiliki wa baa hiyo.

Wakati tayari Manispaa ya Kinondoni inalitaja eneo hilo la Rose Garden kuwa la hifadhi ya barabara, Wizara ya Ardhi inaliona vinginevyo. Kauli aliyoitoa Magufuli mwanzoni mwa wiki hii, wakati akizungumza na waandishi wa habari akimtetea mmiliki wa baa hiyo, akisema ana hati halali iliyotolewa na Kamishna wa Ardhi, tayari imepokewa kwa hisia tofauti na watu mbalimbali walio na masilahi yanayokinzana juu ya umiliki wa kiwanja hicho.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima unaonyesha kuwa, Magufuli alitoa kauli hiyo akitumia kumbukumbu zilizopo wizarani hapo ambazo zinaonyesha kuwa kiwanja hicho hakipo katika hifadhi ya barabara. Dokezo linalohusu eneo hilo ilipo Rose Garden lililosainiwa na Kamishna wa Ardhi, Albert Msangi, ambalo Tanzania Daima imepata nakala yake linaonyesha kuwa barabara inayopita hapo iko katika kundi la Barabara za Mikoa (Primary Distributor Road) na si Barabara Kuu za Kitaifa.

Kwa mujibu wa dokezo hilo, ambalo linazingatia Mpango Kabambe wa Jiji la Dar es Salaam wa mwaka 1979, upana wa barabara za mikoa unapaswa kuwa wa kati ya mita 30 hadi 40 na ‘carriage’ ya kati ya mita saba hadi 10, viwango ambavyo vinakidhiwa na Rose Garden, na hivyo kuifanya kuwa nje ya eneo la hifadhi ya barabara.

“Kulingana na viwango hivyo, upana wa barabara ambayo upo sambamba na ‘Rose Garden’, inayounga Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Barabara ya Mikocheni, unatakiwa kuwa kati ya mita 30 hadi mita 40 kwa kuwa ni ‘Primary Distributor Road’. “…Kwa mantiki hiyo, upana wa barabara iliyopo kwenye eneo hilo la Rose Garden unakidhi viwango hivyo vya mita 30 kwa ‘carriage way’, inatakiwa iwe kati ya mita saba hadi 10, kwa maelezo hayo eneo la Rose Garden halipo katika ‘road reserve’ kama inavyodhaniwa (angalia kiambatanisho kinachoonyesha upana wa barabara kulingana na G.N 157 ya mwaka 1997 ), eneo husika limegawiwa kwa matumizi ya cafes and restaurants,” linasema dokezo hilo.

Mbali ya dokezo hilo, Tanzania Daima pia imebaini kuwapo kwa mawasiliano ya barua kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri Magufuli kuhusu suala hilo la Rose Garden. Moja ya barua ambayo gazeti hili limeiona, imeandikwa na Waziri Magufuli kwenda kwa waziri mkuu ikitoa ufafanuzi wa uhalali wa umiliki wa kiwanja hicho. Barua hiyo ya Agosti 14, 2006, yenye kumbukumbu namba LD 247419 iliyosainiwa na Magufuli mwenyewe, inasisitiza kuwa eneo hilo limegawiwa kwa matumizi ya migahawa.

Sehemu ya barua hiyo ambayo ni majibu ya barua aliyoandikiwa Magufuli na Katibu wa Waziri Mkuu, B. Olekuyan, ya Agosti 4, 2006, yenye kumbukumbu namba PM/P/1/567/38, inasomeka: “Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa mujibu wa sheria Na. 167 ya mwaka 1967 inayohusu hifadhi ya barabara, tangazo la serikali G.N 157 la mwaka 1997 likisomwa kwa pamoja na kifungu cha 78 cha sheria ya mipango miji na vijiji.

“…..Sura 378 (The Town and Country Planning (Town Planning Space Standards) Regulation, 1997) na kwa kuzingatia mchoro wa mipango miji na. 1/518/369 wa eneo la Mikocheni ilipo barabara ambayo iko sambamba na Rose Garden inayoungana na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. “…..Inaonyesha eneo la Rose Garden halipo katika hifadhi ya barabara (Road Reserve) kama ilivyodhaniwa. Hali kadhalika, eneo hilo limegawiwa kwa matumizi ya cafes and restaurants.”

Barua hii inadhihirisha kuwa msimamo wa Waziri Magufuli kuhusu mgogoro wa Rose Garden hauwezi kubadilika, na kwa sababu mmiliki wake analindwa na sheria ambazo Magufuli alizitumia kujibu barua aliyoandikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Katika kuthibitisha kuwa Magufuli amekwishatambua mpango wa watu wanaotaka kummaliza kwa kutumia sakata la mgogoro wa umiliki wa kiwanja cha Rose Garden, hivi karibuni, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema haogopi matokea ya uamuzi wake.

Magufuli, ambaye mara kadhaa amekumbana na misukosuko, ikiwamo kuokotwa bunduki nyumbani kwake, anaonekana kuzidi kuandamwa baada ya hivi karubini kuzushiwa kuwa amefariki dunia akiwa nchini Ujerumani ambako alikuwa akitibiwa.
 
KadaMpinzani

Tafadhali fahamu kitu ambacho mimi ninakupinga, maneno haya hayatoki kwa chombo chochote cha habari bali ni ya kwako:

magufuli anakwambia yeye kama waziri ana protection ya kubadilisha cheti chochote "kama waziri", mhm, here he goes ! sasa now we know inakuwaje akina richmonduli wanapata ulaji eehh, je huyo pm si ndio atatumia mamlaka yake yoooote ahakikishe anakula ulaji ! mheshimiwa magufuli angalia unachosema, utatoa siri zako bure bila ya kukusudia mwenyewe, duh halafu huyu braza 'gufuli nasikia aliwafukuza wafanyakazi wa wizara yake kwa tuhuma kwamba wanatoa siri za wizara yake juu ya RG !!

Maneno haya sio ya Waziri Pombe Magufuli kama vile unavyotaka wanabodi tuamini na ndio issue. Nimeonyesha kwa ufasaha hapo juu kuonesha kwamba tafsiri yako si sahihi na ndipo nikauliza where is your credibility? Kama una uhakika wa maneno haya kutoka popote ambapo unadai kwa nini usi-quote hizo sentesi tano au sita uweke hapa? Mimi sijasema niko 100% right bali tafsiri yako inaonyesha upeo mdogo ambao siutegemei kutoka kwako na member yeyote ambaye anachangia hapa. Hakuna associated press wa JF na ndio maana ikaitwa forum, hapa tunakata issues - PERIOD.

Kama umeshindwa kuonyesha hiyo source omba msamaha kwa wanabodi kwamba umekosea hakuna aibu hapa ni kukata mzizi wa fitina tu. Vilevile na mimi mahali pengine naweza kukosea na nitaomba radhi, lakini siwezi kukomalia maandishi yangu ambayo yatakuwa si sahihi au yana upendeleo fulani kama inavyoonyesha hapo juu.
 
HAKUNA ALIYEBANWA HAPA : link hiyo hapo na inaelekea dua hukusoma articles zilizokuwa posted au huu mjadala umeuignilia kati kati kiasi kwamba ulikuwa hujui nini kilichokuwa kinaongelewa mwanzo :

http://jambotanzania.net/v2/content/view/1061/2/

baadhi ya quotes hizi hapa:"Naye, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa, alisema aliwahi kwenda kwa waziri anayehusika kuzungumzia suala hili, lakini hakuonyesha ushirikiano kwa kutoa majibu ya kukatisha tamaa na kuwafuta kazi baadhi ya watumishi wa chini, aliodai wanavujisha siri za wizara.

"Nakumbuka tuliwahi kwenda kwa waziri anayehusika katika kutafuta suluhu ya hili, nilikuwa na Mheshimiwa Charles Keenja, Janeth Kahama, na baadhi ya wabunge wengine.

Majibu tuliyopata siku hiyo yanasikitisha, huwezi kuamini kama ni kiongozi mkubwa serikalini… tena baadhi ya wafanyakazi wa chini walifukuzwa kazi kwa madai kuwa walivujisha siri za waziri," alisema Londa."

Na sasa subiri niangalie "stock" yangu ya news ili nikupatie hiyo aliyosema ana protection yeye kama waziri !!

Sasa Dua fuata link hiyo na usome kwa makini na uone kwamba mie sio hivyo unavyodhani !!!! hapa mbona patamu !!

Well, lastly nadhani unataka kunifanya nionekane sijui ninachosema kwa kuomba msamaha, no way ! najua ninachosema, naamini ninachosema !!
 
KadaMpinzani

Maneno yako yapo hapo juu tuonyeshe umalize huu ubishi, just copy and paste tuone ukweli.

Kwa lugha nyepesi copy haya maneno yako:
magufuli anakwambia yeye kama waziri ana protection ya kubadilisha cheti chochote "kama waziri", mhm, here he goes ! sasa now we know inakuwaje akina richmonduli wanapata ulaji eehh, je huyo pm si ndio atatumia mamlaka yake yoooote ahakikishe anakula ulaji ! mheshimiwa magufuli angalia unachosema, utatoa siri zako bure bila ya kukusudia mwenyewe, duh halafu huyu braza 'gufuli nasikia aliwafukuza wafanyakazi wa wizara yake kwa tuhuma kwamba wanatoa siri za wizara yake juu ya RG !!

Halafu tuonyeshe huyo mwandishi aliyeandika. Haya ni maneno yako, kitu gani huelewi? Sina sababu ya kufuata link kwa sentesi chini ya sita.
 
hayo maneno ni kweli yangu, and thats what is called summarizing. nimetoa sehemu nyingine na kusummarize hapa, kuna tatizo na hilo ?? endelea, lingine ??
 
Ukisha-summarise hapo tayari unatoa ya kwako; kada lisimamie tu hilo ulilosema, hamna noma
 
KadaMpinzani

Sasa hiyo summary yako siyo ya kweli waziri alikuwa hakusema hivyo. waziri alisema hivi.

`Namshangaa mmliki wa mgahawa wa Rose Garden kwa kutowashtaki mahakamani watu wanaomkwaza kufanya kazi zake? Hata akienda mahakamani, mimi na Kamishna wa Ardhi ni mashahidi wake,`alisisitiza.

Pia Waziri Magufuli alisema ni Wizara pekee iliyopewa mamlaka kisheria ya kuidhinisha matumizi ya ardhi nchini kote.

`Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999, inampa Waziri wa Ardhi mamlaka ya kuidhinisha au kubadili matumizi ya ardhi katika vijiji na miji yote nchini, hivyo hata kama ningefanya hivyo, bado ningefanya kwa mujibu wa sheria hiyo,` alisema.

Jaribu kujifunza summarization iliyo fasaha.
 
wewe Dua yaani ni mbishi way out, all the way down ! Hii issue ilitolewa na vyombo tofauti sasa wewe naona una-rely on one source which differs from the sources i got, unalazimisha kitu. kuna sources nyingi sana, kwani wewe unasoma ipp tu peke yake ? waulize wana jf wakupe links za news za bongo !!!!! well, wat i said is wat was written in the news na sioni sababu ya waandishi kuongopa !! am out
 
Back
Top Bottom