Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
Magufuli: Wizara itaangalia mpya ranchi walizopewa wawekezaji
John Nditi, Morogoro
Daily News; Tuesday,March 11, 2008 @00:04
WIZARA ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi inakusudia kupitia upya mashamba ya ranchi za taifa yaliyotolewa kwa wawekezaji na kuyageuza kuwa ya shughuli za kilimo badala ya kuendeleza mazao ya mifugo kama yalivyokusudiwa na serikali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Wizara hiyo, John Magufuli, jana mjini hapa wakati akizindua Baraza la Wadau wa Sekta Ndogo ya Nyama lililowashirikisha wataalamu wa mifugo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
Alisema hayo baada ya kubaini kuwa baadhi ya watu wamejipenyeza kuyanunua mashamba ya ranchi za Taifa, lakini hawakuwa na nia ya kuendeleza sekta hiyo ya mifugo na badala yake kuyatumia kwa kilimo cha mazao mbalimbali.
Hivyo kutokana na kubainika huko, Magufuli amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya uchunguzi wa mashamba yote ya ranchi za Taifa yaliyogeuzwa kuwa mashamba ya kilimo na kutoa taarifa kwake.
Alisema baadhi ya mashamba hayo yanamilikiwa na wageni bila ya kuwashirikisha Watanzania ambako ni kinyume cha utaratibu wa kuyagawa mashamba hayo. Alisema endapo kuna mgeni aliyepewa mashamba hayo bila kuwa na ubia na Watanzania, Serikali itafanya utaratibu unaofaa wa kuhakikisha wanaingia ubia na Watanzania kwa umiliki wa hisa kwa asilimia 51.
Alisema iwapo wageni waliochukua hayo mashamba kwa kupitia sheria ya uwekezaji na kubainika kuwa hawajaingia ubia na wazawa, lazima wakodishiwe maeneo hayo kwa mkataba wa kipindi maalumu na sio kumilikishwa.
Akizungumzia sekta ya nyama nchini, Magufuli alisema kiwango cha ulaji wa nyama ni mdogo kwa Watanzania ambacho kwa wastani mtu mmoja hula kilo 10 za nyama kwa mwaka ambapo ni chini ya kiwango cha kimataifa kilichopendekezwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) cha kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka.
Hata hivyo, alisema takwimu za uzalishaji wa nyama zinaonyesha kuna upungufu katika uzalishaji wa nyama kutoka tani 210,370 katika kipindi cha mwaka 2005/06 ukilinganishwa na tani 180,629 za mwaka 2006/07.
Alisema uzalishaji katika kipindi cha mwaka 2007/08 unatarajia kuongezeka kutokana na kutokuwapo na milipuko ya magonjwa kama ilivyojitokeza ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF) uliojitokeza kati ya mwaka 2006/07.
Alisema tayari serikali imeshaanza jitihada mbalimbali za kuboresha miundombinu ya masoko katika sekta ya mifugo ili kuongeza upatikanaji wa mifugo na nyama kwa lengo la kukidhi soko la ndani.
Source: HabariLeo