Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Magufuli: Wizara itaangalia mpya ranchi walizopewa wawekezaji
John Nditi, Morogoro
Daily News; Tuesday,March 11, 2008 @00:04

WIZARA ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi inakusudia kupitia upya mashamba ya ranchi za taifa yaliyotolewa kwa wawekezaji na kuyageuza kuwa ya shughuli za kilimo badala ya kuendeleza mazao ya mifugo kama yalivyokusudiwa na serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Wizara hiyo, John Magufuli, jana mjini hapa wakati akizindua Baraza la Wadau wa Sekta Ndogo ya Nyama lililowashirikisha wataalamu wa mifugo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Alisema hayo baada ya kubaini kuwa baadhi ya watu wamejipenyeza kuyanunua mashamba ya ranchi za Taifa, lakini hawakuwa na nia ya kuendeleza sekta hiyo ya mifugo na badala yake kuyatumia kwa kilimo cha mazao mbalimbali.

Hivyo kutokana na kubainika huko, Magufuli amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya uchunguzi wa mashamba yote ya ranchi za Taifa yaliyogeuzwa kuwa mashamba ya kilimo na kutoa taarifa kwake.

Alisema baadhi ya mashamba hayo yanamilikiwa na wageni bila ya kuwashirikisha Watanzania ambako ni kinyume cha utaratibu wa kuyagawa mashamba hayo. Alisema endapo kuna mgeni aliyepewa mashamba hayo bila kuwa na ubia na Watanzania, Serikali itafanya utaratibu unaofaa wa kuhakikisha wanaingia ubia na Watanzania kwa umiliki wa hisa kwa asilimia 51.

Alisema iwapo wageni waliochukua hayo mashamba kwa kupitia sheria ya uwekezaji na kubainika kuwa hawajaingia ubia na wazawa, lazima wakodishiwe maeneo hayo kwa mkataba wa kipindi maalumu na sio kumilikishwa.

Akizungumzia sekta ya nyama nchini, Magufuli alisema kiwango cha ulaji wa nyama ni mdogo kwa Watanzania ambacho kwa wastani mtu mmoja hula kilo 10 za nyama kwa mwaka ambapo ni chini ya kiwango cha kimataifa kilichopendekezwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) cha kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Hata hivyo, alisema takwimu za uzalishaji wa nyama zinaonyesha kuna upungufu katika uzalishaji wa nyama kutoka tani 210,370 katika kipindi cha mwaka 2005/06 ukilinganishwa na tani 180,629 za mwaka 2006/07.

Alisema uzalishaji katika kipindi cha mwaka 2007/08 unatarajia kuongezeka kutokana na kutokuwapo na milipuko ya magonjwa kama ilivyojitokeza ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF) uliojitokeza kati ya mwaka 2006/07.

Alisema tayari serikali imeshaanza jitihada mbalimbali za kuboresha miundombinu ya masoko katika sekta ya mifugo ili kuongeza upatikanaji wa mifugo na nyama kwa lengo la kukidhi soko la ndani.


Source: HabariLeo
 
Jamaa mchapakazi, hata wadau wanamfagilia kinoma. Inasemekana baada ya kuripoti pale Wizarani akazama kwanza kwenye mafile. Sasa anaanza kuibua mambo.

Tayari kuna kampuni moja ya wazawa makini imeapa kusaidia kuwatengenezea wadau wa mifugo; mifumo ya ufuatiliaji, packaging na label yaani "Livestock Identification, Registration, and Traceability System" Hii itawasaidia ku-comply na Food Safety Standards hatimaye kuuza nyama na mazao ya wanyama katika masoko yenye tija.
 
Tatizo ni fitina za viongozi wetu
Wakiona mtu anafanya kazi wanakaa kumpigia majungu na kumwondoa pale, kumbuka jinsi alivyokuwa anashughulikia mambo ya barabara, ukiuliza kwanini walimwondoa pale wakati alikuwa akifanya vizuri kuliko waziri yeyote yule, uwezi kupata jibu

Hilo ni kweli kabisa, wivu ubinafisi na fitina zinachangia sana kudumaza maendeleo yetu TZ.

Magufuri pamoja na mapungufu yake kazi ya barabara aliiweza sana, kama si nia mbaya angepewa muda zaidi atukamilishie barabara zetu! Ila tangu aondoke ndo basi tena hakuna barabara hata moja ilo kwisha kamilika!!

Ardhi nako alikuwa amekunyoosha, sasa walipo ona anafanya vyema eti wanampeleka kitoweo, Ila bwana kama mtu ni chapakazi, bado hata huko kazi yake itaonekana tu

Ninacho shindwa elewa, hivi kweli hao wakuu wanapenzi na nchi yetu? ama ni wabinafsi tu wa kutofurahia muona mtu akipata sifa kwa ajili ya utendaji kazi wake?
 
Tatizo ni fitina za viongozi wetu
Wakiona mtu anafanya kazi wanakaa kumpigia majungu na kumwondoa pale, kumbuka jinsi alivyokuwa anashughulikia mambo ya barabara, ukiuliza kwanini walimwondoa pale wakati alikuwa akifanya vizuri kuliko waziri yeyote yule, uwezi kupata jibu

HATA MIMI HUWA NINAMKUBALI.
 
Mchapa kazi ni mchapa kazi tu, hata umpeleke jangwani, bado atapata kazi ya kufanya.

Huyu jamaa ni kama Mrema tu, maana Mrema alipopelekwa wizara ya kazi, mimi nikajua huko basi tena. Jamaa akaanza kuwavurumisha wafanyakazi wasio Watanzania.

Tunahitaji akina Magufuli wengi.
 
sasa ni nani anamuonea wivu Magufuli wakati bosi wake ni Muungwana!.Muungwana angekuwa anamuonea wivu wa uchapakazi si angemwacha ili asikombe ujiko?. Mimi nadhani Muungwana ametambua utendaji wa huyo jamaa ndo maana amempa wizara nyingine nyeti,suala la chakula halihitaji mchapa kazi?
 
sasa ni nani anamuonea wivu Magufuli wakati bosi wake ni Muungwana!.Muungwana angekuwa anamuonea wivu wa uchapakazi si angemwacha ili asikombe ujiko?. Mimi nadhani Muungwana ametambua utendaji wa huyo jamaa ndo maana amempa wizara nyingine nyeti,suala la chakula halihitaji mchapa kazi?

huyu ni pattern kwa hio kuhama wizara ni kuonesha mfano wa jinsi gani kazi zinaweza kufanyika.


mie sioni kama kuhamishwa wizara kuna maana ya kumtosa bali ni kumjenga maana hii inajenga CV yake pili inampa uzoefu wa sehemu mbali mbali za wizara zetu.

SHUJAAA POMBE MAGUFULI
 
huyu ni pattern kwa hio kuhama wizara ni kuonesha mfano wa jinsi gani kazi zinaweza kufanyika.


mie sioni kama kuhamishwa wizara kuna maana ya kumtosa bali ni kumjenga maana hii inajenga CV yake pili inampa uzoefu wa sehemu mbali mbali za wizara zetu.

SHUJAAA POMBE MAGUFULI

Kumpa uzoefu wa Wizara mbalimbali si wazo baya sana, lakini pia angekuwa ana achwa Wizara moja muda mrefu zaidi ili yale aliyo anzisha ayakamilishe. Kwenye barabara jamaa alitufaa sana. Sasa hivi hakuna kitu, Chenge mwanasheria na ujenzi wa barabara wapi na wapi?
 
kwa kweli magufuli ni mchapa kazi na mie ningelipendekeza awe rais wetu baada ya jk.


ukweli ni mtu safi

Mtu wa Pwani...after JK ni zamu ya Zanzibar..msianze mapema kampeni...kama anafaa asubiri Vice President...
 
Hivi kweli Magufuli ndo dingi wa Vitoweo Tz!

Du.. basi poa naamini shida zote za vitoweo zitaisha!

Yaani nimekumbuka sana supu ya kuku wa kienyeji na kongoro kwa ndizi mzuzu za kuchoma!
 
kwa kweli magufuli ni mchapa kazi na mie ningelipendekeza awe rais wetu baada ya jk.


ukweli ni mtu safi


true story,...pia huyu Jah-Kaya hajui kuspot potential people, yaani leo magufuli anapewa wizara ya ng'ombe na kilimo cha jembe!!...anyway may be he(Magufuli) can spark the change(s)
 
Lugha ya mtaani mtu kama Magufuri tunamwita jembe/Kichwa/Kubwa Lao.

Apo ndo ujue ukiwa smart na kazi yako lazima wakuchukie Tz.

Umegundua kila aendapo Magufuli mambo yanakua shwari na hakai mda wanamwamisha.

Unajua reason behind ya kumwamisha mwamisha lengo lao ni kuhakikisha hapati umaarufu na kuwa our next president by any means.Tatizo wanakwazwa na popularity yake na uchapa kazi wake.

Magufuri tuko nyuma yako,keep it up
 
sasa ni nani anamuonea wivu Magufuli wakati bosi wake ni Muungwana!.Muungwana angekuwa anamuonea wivu wa uchapakazi si angemwacha ili asikombe ujiko?. Mimi nadhani Muungwana ametambua utendaji wa huyo jamaa ndo maana amempa wizara nyingine nyeti,suala la chakula halihitaji mchapa kazi?

Tatizo si kuwa wizara hii haiitaji mchapa kazi bali katika historia ya nchi yetu mifugo haijapewa kipaumbeli mpaka wizara yake ikawa na maana. Tazama ofisi zao. Hivyo kinachofanyika ni kumdidimiza Pombe kwa kujaribu kumpoteza kwa kumpa eneo ambalo wanaisi watanzania wengi hawaguswi. Lakini jamaa ni kichwa. Huko Moro aliwashangaa wale wazee wa PHD za mifugo kutokuisaidia nchi hii. Pombe anauliza ni kwa nini waliamua kusomea hiyo fani, kwa nini awakubaki kuwa wafugaji. Hivi sasa natambua kuwa nchi hii inang'ombe 18,000,000.00 na pia asilimia 60% ya nchi hii inafaa kwa ufugaji. Lakini hata issue ya Ranch kutumika vibaya kaliweka bayana.

Mr. Pombe ni Waziri pekee aliyefanikiwa kuifanya serikali japo kuwa mbele ya wananchi. Upimaji viwanja vya makazi na mabadiliko ya sheria muhimu za ardhi, makandarasi na miji. Nchi hii watu ujitafutia makazi na kisha kuanza kuitafuta serikali yao iko wapo maana hakuna miundombinu ya maji, barabara, umeme nk. I believe atleast we have someone to praise after Mrema mzee wetu wa Kiraracha. Hawa watu wanasifa moja. Wanafanya mambo mengi sana kuliko kawaida. Kama wangekuwa ni madaktari pale muhimbili naamini wangekuwa wapasuaji wazuri na wangeudumia watu wengi.

Mtu asiye fisadi utamtambua kwa namna anavyotumia muda wake kutatua matatizo ya wananchi. Mtu fisadi atakulaghai kwa maneno ya juu juu tena ya kupewa si ya kusoma.

Big UP Mh. Augustino Lyatonga Mrema a great leader of his time and Hon. John Pombe Magufuli a growing Leader of his Kind that the Nation deserve to have especially after this UFISADI Error disappeared.
 
huyu ni pattern kwa hio kuhama wizara ni kuonesha mfano wa jinsi gani kazi zinaweza kufanyika.


mie sioni kama kuhamishwa wizara kuna maana ya kumtosa bali ni kumjenga maana hii inajenga CV yake pili inampa uzoefu wa sehemu mbali mbali za wizara zetu.

SHUJAAA POMBE MAGUFULI

Hiyo CV anayoijenga ni kwa faida ya nani? Je, wewe uliitambua saana CV ya Kikwete? Kama ni kwa faida yake sawa lakini kama wangetaka kumjenga wangempa wizara nyeti. Wangempa wizara ya ndani, nje, fedha, ulinzi au moja kati ya wizara ya utalii na maliasili ama wizara ya nishati na madini maana ni wizara zenye maslai kwa taifa lakini zimekosa watendaji wenye nembo kama ya Magufuli.
 
Big UP Mh. Augustino Lyatonga Mrema a great leader of his time and Hon. John Pombe Magufuli a growing Leader of his Kind that the Nation deserve to have especially after this UFISADI Era disappeared.

Who told you ufisadi error has gone. It is strongly still persisting!

On the other hand, namkubali pia magufuli!
 
Heshima Mbele Wakuu,

Baada ya Mhe. Chenge kushindwa kujenga hata barabara moja toka achaguliwe kuwa waziri wa Miundombinu na kwa kuwa imedhihirika kwamba tuhuma alizonazo ni nzito na amekubali kuwajibika kwa manufaa ya umma.

Huu ni wakati muafaka wa kupendekeza ni nani anafaa kuchaguliwa kuwa Waziri wa Miundombinu. Kipindi cha Awamu ya tau Mhe. Magufuli alijitahidi sana kujenga barabara kwa kiwango cha rami mpaka nchi ikaanza kupendeza, mojawapo ya kazi ambazo ninamsifu ni ujenzi wa barabara za Mwanza mjini ambapo hapo kabla kulikuwa hakuna barabara za kiwango cha rami aliweza kujua barabara zote kwa jina na kujua ni wapi panatakiwa papewe kipaumbele.

Mie nadhani kuna haja ya yeye kurudishwa ili akamalize ahadi yake ya kuweka rami barabara ya Mtwara mpaka Mwanza.

Najua chaguo la Muungwana linaweza kuwa Ezekiel Maige kwa silimia 70, ila Namuomba mkuu wa kaya amrudishe Magufuli katika wizara hiyo!
 
Back
Top Bottom