Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Uuzwaji wa nyumba za serikali ni wa serikali nzima ya BM akiwemo JK ambaye hapa mnasema ni mkombozi na ana nyumba ya kununua sasa leo kumpa lawama juu ya hizo bwana Pombe ni kumuonea JK anayo na alificha hadi last minutes .Je ndiyo usafi wa JK ?
Kabisa
 
Cha kujiuliza ni kwa nini Gazeti la Rai linalomilikiwa na Rostam Azizi limemuandama Magufuli? Ni wazi huyu ni mawe katika mchele na itabidi apembuliwe hivi karibuni. Lakini kwa kupenda madaraka atasubiri hadi aumbuliwe!
Kitila
 
Huyu Magufuli ni mtoto yatima katika familia ya JK. Ni ubishi na kukosa ujasiri kinachomfanya abaki katika serikali ya JK na CCM. Ingekuwa katika nchi zingine kama Kenya, Senegal, Ghana, n.k., huyu mtu angekwisha kujiunga na CHADEMA tangu Julai 2006. Zile makala kwenye gazeti la Rai zilitosha kumuonesha jinsi asivyotakiwa. Katika CCM kuchapa kazi na kusisimamia sheria kama zilivyo ni tatizo. Kwa CCM sheria na taratibu ni kwa walala hoi tu, kitu ambacho Magufuli haelewi. JK alimpa uwaziri kwa sababu za kisiasa, kwani jamii isingemuelewa. Kinachofanyika sasa ni kujaribu kumtoa Magufuli katika nyoa za watanzania ili watakamtema akose wa kumtetea. Na tayari Magufuli polepole ameshaanza kutoka katika nyoa za Watanzania kama tunavyoona humu katika forum. Sasa kwa kukosa ujasiri atasubiri hadi wamtose na aishe kisiasa. Wakimhurumia sana watamuacha hadi kura za maoni za 2010, na hapo inafanyika namna ashindwe. Ndipo atakapoanza kupaparika na kukimbilia katika vyama vya upinzani kama alivyofanya Njelu, but it will be too late, na ataonekana hakubali kushindwa. Katika kundi hili yumo pia Mwandosya. Namhurumia sana Magufuli, maana nathamini utendaji kazi wake.
Mkuu
 
Mhariri
HabariLeo; Tuesday,February 20, 2007 @00:01

STAILI ya utendaji ya John Pombe Magufuli, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, ina mwelekeo wa kuifanya serikali ya awamu ya nne isieleweke kwa wananchi. Baadhi ya maamuzi ya mheshimiwa huyo yanakwenda kinyume na utaratibu wa kuheshimu sheria na wakati mwingine yanakejeli mfumo mzima wa utawala bora.

Katika hali isiyoeleweka, Magufuli inasemekana ameidhinisha utoaji wa hati ya kumiliki ardhi katika eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya akiba ya barabara huko Mikocheni Dar Es Salaam.
Wale wanaolifahamu eneo hilo watakubali kwamba kilichojengwa pale hakikustahili kuwapo.

Kwanza, kuna jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kulikofungwa vifaa vya kudhibiti na kufuatilia mwenendo wa masafa yote ya mawasiliano, kuanzia redio, televisheni na simu za mkononi na upepo ili kusiwe na muingiliano.

Eneo hilo lingehitajika kuwa na ulinzi wa hali ya juu na kutokuruhusiwa kwa aina yoyote ile shughuli za biashara, hasa biashara ambazo zinaendeshwa hadi usiku wa manane. Isitoshe, katika hali ya kejeli na dharau, wamiliki wa eneo ambalo Magufuli amelitolea hati wamediriki kujenga choo ambacho kimeegemea ukuta wa eneo la mitambo hiyo nyeti ya Taifa.Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wameshalalamikia kuwapo kwa jengo kwenye eneo la barabara.

Manispaa imehoji uhalali wa hatua ya Waziri Magufuli kutoa hati ya kumiliki ardhi kwenye eneo la hifadhi ya barabara. Hivi ni nani anaielewa zaidi wilaya ya Kinondoni kama sio madiwani wake? Nini maana ya serikali za mitaa kama zinaingiliwa na mawaziri ambao hata hawahusiki na sekta hiyo?

Tunajiuliza: hivi si Magufuli huyu huyu aliyeongoza ubomoaji wa kituo cha mafuta kilichojengwa kwenye kile alichokiona kuwa ni hifadhi ya barabara kule Mwanza? Hivi si Magufuli huyu huyu, aliyesimama Bungeni na kumkosoa hadharani Naibu wake, ambaye kwa wadhifa wake wa ubunge ni diwani Kinondoni akimshutumu kuwa emehodhi viwanja? Madiwani wa Kinondoni na Watanzania kwa ujumla wana uhalali wa kutaka umiliki wa eneo hilo la Mikocheni ubatilishwe mara moja ili kulinda hadhi ya serika
Nawatakia siku njema sana lusungo Chakaza Daudi Mchambuzi Tabu tupu @sifileo na wengine
 
Huyu Magufuli ni mtoto yatima katika familia ya JK. Ni ubishi na kukosa ujasiri kinachomfanya abaki katika serikali ya JK na CCM. Ingekuwa katika nchi zingine kama Kenya, Senegal, Ghana, n.k., huyu mtu angekwisha kujiunga na CHADEMA tangu Julai 2006. Zile makala kwenye gazeti la Rai zilitosha kumuonesha jinsi asivyotakiwa. Katika CCM kuchapa kazi na kusisimamia sheria kama zilivyo ni tatizo. Kwa CCM sheria na taratibu ni kwa walala hoi tu, kitu ambacho Magufuli haelewi. JK alimpa uwaziri kwa sababu za kisiasa, kwani jamii isingemuelewa. Kinachofanyika sasa ni kujaribu kumtoa Magufuli katika nyoa za watanzania ili watakamtema akose wa kumtetea. Na tayari Magufuli polepole ameshaanza kutoka katika nyoa za Watanzania kama tunavyoona humu katika forum. Sasa kwa kukosa ujasiri atasubiri hadi wamtose na aishe kisiasa. Wakimhurumia sana watamuacha hadi kura za maoni za 2010, na hapo inafanyika namna ashindwe. Ndipo atakapoanza kupaparika na kukimbilia katika vyama vya upinzani kama alivyofanya Njelu, but it will be too late, na ataonekana hakubali kushindwa. Katika kundi hili yumo pia Mwandosya. Namhurumia sana Magufuli, maana nathamini utendaji kazi wake.
Kuna watu watayakana maandishi yao wenyewe
 
Hii ilikuwa ni jamboforums, baadae ikawa jamiiforums
Hii ilikuwa ya viwango vikubwa sana, lakini sababu mojawapo ni kuwa kulikuwa na uhuru wa habari enzi hizo kwa hiyo kulikuwa na source ya information nyingi hata serikalini
 
Gazeti la Rai la Alhamisi [Oct 5 - Okt 11] limekuja na habari yenye kichwa hicho hapo juu.

Dondoo ni kuwa:

Wakala wa majengo, taasisi iliyo chini ya wizara ya Miundo mbinu, imemuuzia nyumba bwana Musa Joseph Magufuli (mdogo wake waziri Magufuli) huku akiwa na mkataba ambao unaonyesha angefanya kazi kwa miezi mitatu tu (26/09/2005 - 31/12/2005). Nyumba aliyouziwa iko ubungo, na ameuziwa kwa Tshs. 1.5M (!). Wakati anapewa ajira hiyo (Afisa tawala, business support unit), bwana Musa alikuwa na bado ni mwanafunzi wa masters UDSM. Alipoanza kazi tu akaanza kushughulikia ununuzi wa nyumba na within one month akawa na nyaraka zote muhimu za kumiliki nyumba hiyo. Wahadhiri wake UDSM wamesema kwa ratiba ya masomo yake ilivyokuwam masomo na kazi visingewezekana. Bwana Musa Magufuli aliacha kazi siku mbili kabla ya mkataba kwisha, akiwa na nyumba!

Mpo hapo? Sijui waziri atatuambiaje katika hili. Otherwise makeke yoote yale ya nyumba za NHC etc itakuwa anatuzuga tu.. nae yumo. ... labda aseme huyu ndugu alichakarika kivyake katika hili suala na yeye hakuhusika.
Alaah!

Mzalendo huyu huyo wa Chato?
 
Nchi hii kuna shida kwenye vyombo vyetu vya usalama hasa katika eneo la ujasusi, kuna watu hawakustahili kuwa viongozi wa ngazi za juu lakini unashangaa imekuwaje wamefika huko na vyombo vyetu vipo na eti wamejiridhisha kwamba wamestahili lakini hata wewe mtu wa kawaida tu ukiangalia utendaji na maamuzi mbalimbali yanayofanywa na watu hao unabaki kujiuliza bila majibu.
Vyombo vya ulinzi na usalama viko sawa. Hakuna linalofanyika kwa bahati mbaya.
Kila kitu kimepangiliwa.
 
Hii nchi inaharibiwa na wana mtandao...

Hawa jamaa wamejaza machawa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii yote...

Kazi yao ni kupaka matope wasiowataka na kujisifia wao...

Bahati mbaya wameteka hadi vyombo vya ulinzi.
 
Umenena vyema sana.
Na inaonekana wanalipwa vizuri sana na waajiri wao.
Maana si kwa kucharuka hivo
 
Magufuli,

Kwa maoni yangu anayo matatizo, tena serious ones, lakini sio kwenye kuuza nyumba isipokuwa kwenye pesa za kutengeneza mabara bara, yeye na Keenja, walienda shue moja ya uongozi wakajifunza kuwa wabongo dawa yao ni kujenga kitu wakione,

halafu tumia hela zozote unazotaka hawatauliza zimetukaje, so far hawa waandishi hawajazigusa data zake vizuri, ila kuna siku watazikuta!
R.I.P Le Mutuz
Ila watu walikua na maono sana humu JF duuu
Rest easy Legends!
 
Hii nchi inaharibiwa na wana mtandao...

Hawa jamaa wamejaza machawa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii yote...

Kazi yao ni kupaka matope wasiowataka na kujisifia wao...

Bahati mbaya wameteka hadi vyombo vya ulinzi.
Upo sahihi mkuu
 
Jambo Forum ilipokua Jambo. Kabla haijaletwa ubatizo wa Jamiiforums ya kina rikiboy kimasihara na Kina Bichwa komwe.
 
Jamii forums ya miaka ile ilikuwa na miamba kweli kweli na pia vyombo vya habari vilikuwa vinafanya kazi yake ipasavyo.

Kurudisha hii culture kwenye jamii yetu sasa hivi ni mtihani mkubwa

Magufuli anayesemwa huku ndio kwenye vyombo vya habari katurudisha miaka 50 nyuma

Maisha haya dah!
 
Back
Top Bottom