Moro: Ajiua kutokana na stress za ugumu wa maisha

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Nungu Nassoro (25), Mfanyabiashara na Mkazi wa Kata ya Lukobe, Wilaya na Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwenye mti wa mwembe uliopo kwenye makazi yake huku Polisi wakisema chanzo cha kujiondoa uhai wake ni msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha.

Taarifa iliyotolewa leo March 02,2025 na Kamanda wa Polisi Morogoro imesema “Tukio hili limebainika mapema jana March 01, 2025 katika Mtaa na Kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro”

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo kujiondoa uhai ni msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha, maiti imekabidhiwa kwa Ndugu wa marehemu baada ya kukamilisha uchunguzi wa
maiti hiyo”
Polisi wamefikiaje hitimisho hilo?
 
Juzi wametangaza kijana 22yrs kajinyonga kwa mawazao Leo kijana 25yrs kajinyonga Nini shida Kwa Hawa watu under 30's still young Kuna mengine ya ziada tofaut na hayo mawazo
 
Matatizo yapo kwa wote na pesa na maisha mazuri si kila kitu kwani nakumbuka Maghayo The Mongolian Savage The Nyabumbu aliwahi kupitia msongo mkali wa mawazo kiasi ya kwamba tulihiofia kuwa atajitoa uhai na aliacha kabisa humu Uzi eti "Liwalo na Liwe" hata bange hazikuweza kupunguza depression yake hiyo na akapotea Jf.

Pamoja na Mandinga na ukwasi wake Mamtoni jamaa alikuwa very depressed ila ndio hivyo tu 'Time heals' jamaa ameweza kuovervome that problem sasa hivi anasumbua..
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Nungu Nassoro (25), Mfanyabiashara na Mkazi wa Kata ya Lukobe, Wilaya na Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwenye mti wa mwembe uliopo kwenye makazi yake huku Polisi wakisema chanzo cha kujiondoa uhai wake ni msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha.

Taarifa iliyotolewa leo March 02,2025 na Kamanda wa Polisi Morogoro imesema “Tukio hili limebainika mapema jana March 01, 2025 katika Mtaa na Kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro”

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo kujiondoa uhai ni msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha, maiti imekabidhiwa kwa Ndugu wa marehemu baada ya kukamilisha uchunguzi wa
maiti hiyo”

Je, amejinyonga au amenyongwa?

Marehemu alikuwa anafanya kazi gani hasa enzi za uhai wake?
Alikuwa anakaa au alikuwa anaishi na nani?
Rekodi za mawasiliano yake ya kimtandao zinasemaje kuhusiana na suala hili? Alikuwa anawasiliana na akina nani hasa siku chache kabla ya kifo chake? Marafiki zake wa karibu walikuwa akina nani hasa? Je, Marehemu alikuwa ana ugomvi wowote ule dhidi ya Mtu yoyote yule? Je, Marehemu alikuwa ameoa, au kuwa na mwenza au mchumba? Mahusiano yao yalikuwaje kabla ya kifo chake? Wazazi au walezi wake wako wapi hasa? Mahusiano yao yalikuwaje kati ya huyo Marehemu na Wazazi/walezi wake pamoja na ndugu zake wengine? Hakuna kabisa ugomvi wowote ule kama vile Mgogoro wa kugombea mali/Mirathi au Mgogoro wa Ardhi?

Polisi wamefikiaje hasa hilo hitimisho kwamba amejinyonga???
 
Watu wengi wanaofikia hiyo hatua wanakua wanajitenga sana na watu, wanapendelea kukaa peke yao muda mwingi, Hili liwe kama funzo hata upitie nagumu kiasi gani tuepuke kujitenga changamoto zingine zinapata ufumbuzi kama mwenye changamoto atakua huru kufunguka
Kingine hawa watu hawataki kukubaliana na uhalisia wa mambo, wengi wao wanakua na matarajio makubwa, mambo yakienda kombo ni rahisi kufanya maamuzi ya hatari
 
Matatizo yapo kwa wote na pesa na maisha mazuri si kila kitu kwani nakumbuka Maghayo The Mongolian Savage The Nyabumbu aliwahi kupitia msongo mkali wa mawazo kiasi ya kwamba tulihiofia kuwa atajitoa uhai na aliacha kabisa humu Uzi eti "Liwalo na Liwe" hata bange hazikuweza kupunguza depression yake hiyo na akapotea Jf.

Pamoja na Mandinga na ukwasi wake Mamtoni jamaa alikuwa very depressed ila ndio hivyo tu 'Time heals' jamaa ameweza kuovervome that problem sasa hivi anasumbua..
😀😀nyau de adriz na Mufti kuku The Infinity
 
Back
Top Bottom