UVCCM: Mbona tupo na negativity sana, kufungwa ni football. Sio timu hamasa sio CCM, hata ingekua CHADEMA hata ingekua wewe ndio upo kwenye timu hamasa TUSINGETOBOA kwa Morocco. Sisi ndio tunakuja na wao walishafika siku nyingi, tupo kupata Experience. Tuache kutoa maoni hasi kwenye swala ambalo hatuna uwezo nalo. Sijui timu hamasa sijui UCCM na UCHADEMA hausaidii kitu hapa. Kufungwa ni football tuache kubeza wengine. Tunashusha Nyota zetu kwa aina hii ya NEGATIVITY.
WASIO CCM: Hakuna haja ya kuwalaumu watu wa hamasa. Wao wanamajukumu mengine kabisa,tusichanganye. Nakubaliana na wewe kwa asilimia zaidi ya 99 kwa mipango na mapendekezo uliyoyaainisha, hakuna short cut katika soka. Mwaka 1994/95 alikuja Kocha wa timu ya Taifa kutoka Romania Victor Stanslescu na alikuja na mapendekezo ya kuboresha michezo kwa mipango ya Miaka 20 baadaye kila mmoja alimdharau na aliamua kusepa kwani hakuona dira wala mipango.
WASIO NA CHAMA: Wanaomba stars ifungwe game zote, hakuna timu duniani hata zilizochukua kombe la dunia captain akahojiwa akataja raisi wa nchi, hata kama raisi alikuwa uwanjani kushuhudia fainali hatajawi, atashukuriwa kocha na Mungu, sasa huu upuuzi ulioingizwa kwenye soka na kutekwa na siasa waendelee , wengi wetu tuna chi tunzishabikia ila siyo hii ya wanasiasa.
Waziri unatumia masaa mawili ni injili unawahubiria? Muda wote mara simu kapiga mama, mara Mwana FA kaja, Mara takataka gani za hamasa, mara kuzindika saa ngapi wachezaji watapumzika na kuwaza game?
Mumewapa tension ya kila aina, yaani sasa hivi tunasika mkia kwenye kundi na hatuna goli, yutadundwa kama ngoma, na hatutakaa tupate akili, ni kujipa magonjwa kushabikia timu za wanasiasa.
Masaa mawili! hapo ni kuwachosha tu. Inabidi wapunzike. watawapiga Zambia, DRC tunaaambulia nafasi ya tatu na kusonga mbele.