Morocco kutupiga 3 kavu imetuheshimisha, Zambia na DRC msituangushe!


Masaa mawili! hapo ni kuwachosha tu. Inabidi wapunzike. watawapiga Zambia, DRC tunaaambulia nafasi ya tatu na kusonga mbele.
 
Mimi siyo mtu wa mpira wala shabiki. Jana niliangalia mpira.

Mtangazaji alidai kwenye Timu ya Taifa kuna wachezaji 6 ambao walipitia Azam Academy, akiwemo ndugu yangu Novatus Didas Miroshi (Chuga).

Picha ya haraka ni kwamba Azam wameweza kuleta mabadiliko sana kwenye soka la Tanzania kwa kuwekeza kitaalam.

Kwa vyovyote vile, Serikali ilipaswa kuwekeza kwenye soka kama anavyofanya Bakhresa, badala ya kutegemea wachezaji kutoka kwenye vilabu.

Kauli ya Mwinyi kwamba Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu bado inafanya kazi.

Kama Bakhresa kaweza kutoa wachezaji 6 kupitia Azam Academy, je, Serikali ikiwekeza tungefika mbali kiasi gani?
 
Mimi maoni yangu nikuwa Kila jambo katika nchi yetu ni siasa, kufungwa sio kitu kigeni lakini kuifanya timu ya Taifa kuwa ni timu ya chama na serikali ndo hapo tunaharibu

Sasa hivi Kila kitu samaia,Samia kwani tushaanza kampeni za uchaguzi wa urais.

Samia tunampenda ila kundi la mafisadi limeiteka serikali na sasa linampofusha macho mama Ili asione urafi wao kwa kutengeneza mapambio ya sifa Kila mahali.

Ndo maana Kila kinachofanywa na serikali wananchi wanatilia mashaka wanaona kuwa ni upigaji, hata michango ya Hamasa nayo inaweza kuwa ni upigaji.

TUKUMBUKE KUWA SUKARI KILO TSH 4500,UNGA KILO 1500, MCHELE 3000 bado nauli, Hakuna kiongozi aliyetoka kuja kulisemea hilo ila mna kusanya watu kuchangia Taifa stars mnaziacha shida za msingi za watu Harafu mnataka Watanzania wawe na uchungu na Taifa stars.
 
Kwani ile mechi ni ya Chama?
 
Kati ya Marais waliofanya vizuri sana, tena katikati ya mazingira magumu sana ni Hayati Benjamin Mkapa, lakini kipindi chake, hatukusikia sifa za kijinga na kinafiki toka kwa mawaziri wake kama hawa wa sasa.
Huu ujinga aliuasisi magufuli a.k.a dikteta jiwe, sasa machawa wote wameambukizwa
 
Ku
Nimefurahi jana tumepigwa kipigo cha kutufunza adabu kama taifa, mpira ni uwekezaji sio hamasa za machawa. Next match Congo na Zambia wanatukanda pia turudi bila point.
Matokeo yana sehemu tatu kufungwa, kufunga na sare.Ni matokeo tu. South Africa imefungwa na Mali, nao waitaji uwekezaji? Brazil alifungwa na Germany, 7-0 nae aliitaji uwekezaji? Ureno alifungwa na Morocco nae aliitaji uwekezaji? Hayo ni matokeo tu ya mpira.
 
Huu ujinga aliuasisi magufuli a.k.a dikteta jiwe, sasa machawa wote wameambukizwa
Tumefikishwa pabaya, haya machawa ukifuatilia. i ma-graduate ya UDSM na IFM , yaani vyuo vimezalisha takataka mjini.
Unakuta jitu liko baa siku nzima linakula WiFi bure na maji kubwa kumbe ni kazi za kufoward na kumsifia mama, wna group zao za kutumiana post ili waipambe serikali.
 
Zambia na DRC zisikuangushe?🤣🤣🤣aiseeeee!!!
Kwani hizo nchi zinakuhusu nini mkuu
 
Khaaa masaa mawili anaongea nao kitu gani? Hata mpirs wenyewe ni lisaa na nusu tu
 
Waziri anahubiri injili ya CCM mungu wao Nyerere 😝😝😝😝
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…