Morocco kwenda Ulaya (Uhispania na Ureno) ni karibu kuliko Zanzibari na Dar (umbali wa fukwe ni 14km)

Morocco kwenda Ulaya (Uhispania na Ureno) ni karibu kuliko Zanzibari na Dar (umbali wa fukwe ni 14km)

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Hili taifa la Morocco wana kila sababu kujiita ni watu wa Ulaya!

Umbali kutoka fukwe za Morocco na Uhispania iliyoko bara la ulaya ni 14km tu! Umbali huu unaruhusu muingiliano rahisi sana kama ilivyo Pemba na Unguja!

Koo nyingi za uhispania wameoleana na Wamorocco kama ilivyo kwetu bara na visiwani!

Kwa usafiri wa ndege kutoka miji muhimu ya Morocco na Uhispania ni mwendo wa saa moja na dakika kumi tu kwani kuna umbali wa takriban kilomita elfu moja tu, umbali ambao ni sawa na kutoka Dar to Mwanza!

Kiufupi hawa waarabu wapo Afrika basi tu lakini asili yao ni Ulaya! Matendo yao ni ulaya, elimu yao ni ulaya, mitaala yao ni ulaya n.k

Tabia za Mreno na Mhispania nyingi zinaingiliana sana na Wamorocco!

Kuiweka kundi moja Morroco na Tanzania ni sawa na kulinganisha nywele za utosini na vinyweleo vya miguu! Hatufanani hata kidogo!

Screenshot_20221215-194511.png
 
Hajatolewa na mwafrika wa ulaya,katolewa na mtu mweusi wa ulaya,thuram ni mtu mweusi wa ulaya kadhalika dembele,siyo waafrika wale
Nimeandika kwa muktadha wa mjadala, mtoa mada ame refers statement na mjadala wa Sofiane Boufal, na ndio maana hata yeye hajataja rangi hapo bosi..

Kwanza ukisha taja rangi ina sound kama racism.
 
Hajatolewa na mwafrika wa ulaya,katolewa na mtu mweusi wa ulaya,thuram ni mtu mweusi wa ulaya kadhalika dembele,siyo waafrika wale

You are too correct,Ila Dembele ni Mfaransa mwenye asili ya Afrika,Ila siyo mwafrika, Commoro ni Waafrika wenye asili ya Arabic countries siyo Waarabu.

Asilimia kubwa ya wazungu wapatikanao South Afrika ni Waafrika ingawa siyo weusi.
 
You are too correct,Ila Dembele ni Mfaransa mwenye asili ya Afrika,Ila siyo mwafrika,Commoro Ni Waafrika wenye asili ya Arabic countries siyo waarabu.

Asilimia kubwa ya wazungu wapatikanao South Afrika Ni Waafrika ingawa siyo weusi.
Yeah, watu wanadhani uafrika ni ngozi nyeusi, sijui wameambiwa na nani!?
 
Kwa sasa wanakubali kuitwa waafrica ila kadri walivyokaribia kombe walikuwa wanaukana uafrica
Watu mnapenda kukuza mambo yenye negativity!

Mahojiano yao niliyaona...

Kati ya WOTE ambao walihojiwa ni MMOJA TU ndie hakuitaja Afrika lakini wachezaji wengine WOTE, including Kocha, wali-dedicate ushindi kwa nchi za Kiarabu na Kiafrika.

Wengine wakaongezea na kwa Waislam, yule MMOJA TU ndie ali-dedicate ushindi kwa nchi za Kiarabu na Muslims World!

Wapenda negativities, wakaacha maelezo ya wengine WOTE wakayachukua ya yule mmoja tu!!
 
Story mbaya ni nzuri kwa mwanahabari, na nzuri ni mbaya!

Kuna mwanahabari wa matukio alikuwaga akisikia polisi wakisema wanatokomeza ajali alisikitika kwa kukosa habari
 
Back
Top Bottom