Morogoro: Baba amshambulia mwanaye kwa sime. Naye afariki kwa tatizo la upumuaji

Morogoro: Baba amshambulia mwanaye kwa sime. Naye afariki kwa tatizo la upumuaji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mtoto mwenye umri wa miaka 9, mkazi wa Kitongoji cha Batini, wilayani Gairo, mkoani Morogoro, amenusurika kifo baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni na baba yake mzazi aliyefahamika kwa jinala Yakobo Taolo (38), huku chanzo kikidaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa, amesema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 15 mwaka huu, majira ya 7:00 usiku ambapo baba wa mtoto huyo alivamia chumba alicholala binti yake huyo, anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Kibedya na kuanza kumshambulia kwa sime ambapo kwa sasa anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Gairo

Kamanda Mutafungwa ameongeza kuwa mara baada ya baba huyo kutekeleza tendo hilo la kutaka kuua alitokomea pasipojulikana kabla ya jeshi la polisi kumkamata akiwa nyumbani kwa Robart Chidaka 45, mkazi wa kibedya ambaye anashikiliwa na jeshi hilo.

Kamanda Mtafungwa amesema kuwa baada ya baba huyo kushikiliwa na jeshi la polisi, alianza kuumwa na kukimbizwa katika kituo cha afya Gairo kwa ajili ya matibabu na baadaye aligundulika kuwa na tatizo la kupumua na ilipofika alfajiri ya Novemba 16 mtuhumiwa huyo alipoteza maisha.
 
Imani za kishirikina kivipi? Waandishi leteni habari kamili.
 
Kamanda Mtafungwa amesema kuwa baada ya baba huyo kushikiliwa na jeshi la polisi, alianza kuumwa na kukimbizwa katika kituo cha afya Gairo kwa ajili ya matibabu na baadaye aligundulika kuwa na tatizo la kupumua na ilipofika alfajiri ya Novemba 16 mtuhumiwa huyo alipoteza maisha.
 
Kamanda Mtafungwa amesema kuwa baada ya baba huyo kushikiliwa na jeshi la polisi, alianza kuumwa na kukimbizwa katika kituo cha afya Gairo kwa ajili ya matibabu na baadaye aligundulika kuwa na tatizo la kupumua na ilipofika alfajiri ya Novemba 16 mtuhumiwa huyo alipoteza maisha.
Dah! Ukakasi mtupu
 
Polisi wameua bila shaka weled ulikosekana wakati wa kumuhoji polisi hutumia nguvu hata kwa vitu visivyohitaji nguvu.
 
Back
Top Bottom