Pre GE2025 Morogoro Das awataka vijana kuacha kujipendekeza kwa Viongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,011
Reaction score
1,681
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro Said Nguya amekemea tabia iliyoanza kujengeka miongoni mwa vijana nchini ya kusifiana sifa za uongo wakiwa ana kwa ana ama kusemana vibaya.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vijana wa
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) na Chuo Kikuu Mzumbe katika Semina maalum iliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Patriotic Organisation inayojishughulisha na uhamasishaji uzalendo kwa vijana.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan anawapenda vijana na kwenye kila fursa lazima aguse kundi hilo, lakini vijana wenyewe kwa wenyewe wamekuwa mstari wa mbele kusemeana mabaya, jambo ambalo lisipokemewa litaota mizizi na baadaye kuwa na Taifa lisilo na staha.


Your browser is not able to display this video.
 
Katika hicho kikao/Mkutano yeye kamtaja Samia mara ngapi?
 
Kwa hiyo Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi SUA ndio kaona kapata bwana, boga kabisa
 
Mbona yeye amepata hiyo nafasi kwa kujipendekeza alikuwa Chawa wa Bashiru pale CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…