Morogoro: DC Ngollo Malenya anawasaka Wazazi Waliotelekeza watoto 3 Ulanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro, Ngollo Malenya ameagiza kukamatwa kwa Wazazi wawili Thomas Ulanda
na Adelyda Nakashawa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria baada ya kuwatelekeza Watoto wao watatu Emerinda Thomas Ulanda (17) Christina Ulanda (13) na Slyvia Ulanda (9) wanaoishi Kijiji cha Gombe, huku Emerinda akipambana kuwahudumia Wadogo zake.

Wazazi hao waliachana, Mwanamke akaolewa na Mwanaume mwingine na Baba akaoa Mwanamke mwingine na kuwatelekeza Watoto kwenye Kijumba ambacho mda wowote kitaanguka na kimewekewa miti kusimamisha ukuta, Emerinda alikuwa analazimika kufanya vibarua vya kulima ili aweze kuwahudumia Watoto wenzie nae pia kujikimu.

DC Ngollo amechukua hatua za haraka kunusuru hali hiyo na kupata Mdau John De Vries (Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Faru Graphite) ambaye kuwajengea Watoto hao nyumba na kuwahudumia mahitaji yote maalum, kuhakikisha Mabinti hao wanasoma na pia ameahidi kuunga mkono kampeni iliyoanzishwa ya Kemea Chagulaga ambayo ni mila kandamizi inayofanywa na Vijana wa Jamii ya Kisukuma ya kulazimisha Wanawake kufanya nao mapenzi kwa nguvu.

DC amewapongeza Majirani wa eneo hilo waliojitolea kuwasitiri Watoto hao hasa wakati wa masika na wakati wa njaa huku aomba Asasi za kiraia zinazopambana na haki za watoto na wanawake waunge mkono hatua alizochukua.
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.


 
masikini vibinti vizuri na Rozali shingoni[emoji122][emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…