JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Alaudin Hasham amemtaka Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Ulanga kuangalia miundombinu ya maji katika hospitali ili kurekebisha maeneo yenye mivujo ya maji.
Salim amesema hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo na kuoneshwa bili ya maji yenye gharama ya milioni moja na laki nane (M 1.8) kwa mwezi Oktoba jambo ambalo Mbunge huyo hakukubaliana nalo.
Mbunge Salim amesema haiwezekani kuwe na bili yenye gharama kubwa kiasi hicho wakati hata maji hayatoki katika hospitali hiyo ambapo mwezi Septemba bili ilikuwa laki nane (800,000) na mwezi Agosti bili ilikuwa milioni moja na laki nne (M 1.4) ambapo ndani ya miezi mitatu wamepelekewa bili ya zaidi ya Tsh. Milioni nne.
Aidha, Mbunge Salim ameshauri kisima cha pampu cha maji kilichochimbwa katika hospitali hiyo kifufuliwe ili kitumike kusambaza maji katika hospitali hiyo ili kuepusha gharama zisizokuwa za lazima.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Ulanga, Stephano Liwemba amesema bili wanazopewa kutoka idara ya maji haziendani na maji wanayotumia kwa kuwa maji baadhi ya wodi hazifikiwi na na maji.
Liwemba ameeleza kuwa wastani wa matumizi ya maji katika hospitali hiyo kwa mwezi ni laki sita hivyo ameshangazwa na bili zenye ghalama kubwa wanazopewa.
Chanzo: Wasafi FM