Morogoro: Jovita adaiwa kumuua mumewe kisa kanyimwa unyumba

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Abel Charles, Mkazi wa Mtaa wa Mambi, Kata ya Mafisa, Manispaa ya Morogoro amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa kwa panga na Mke wake wakati wakiwa nyumbani usiku.

AyoTV imefika katika eneo la tukio na kuzungumza na Mjumbe wa Mtaa huo ambaye amesema alipokea taarifa kutoka kwa Mpangaji katika nyumba hiyo kwamba wakati wa usiku vilisikika vishindo vikubwa kutoka katika chumba walichokuwa wakiishi wawili hao.

Kwa mujibu wa Mjumbe huyo, asubuhi Mwanamke anayedaiwa kuhusika na tukio hilo alionekana akiwa na majeraha mdomoni na alipoulizwa Mume wake alipo, inadaiwa alieleza kuwa alikuwa kazini na kwamba hakuwa na funguo za chumba alichokuwa akilala kutokana na wawili hao kuwa na ugomvi na kulala vyumba tofauti.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limetangaza kumkamata Jovita Bateguye Budyo (30), fundi cherehani na Mkazi wa Mafisa, kwa tuhuma za kumuua Mumewe, Abeli Charles (44), Mfanyabiashara na mkazi wa Mafisa.
 
Attachments

  • IMG-20260901-WA0039.jpg
    IMG-20260901-WA0039.jpg
    50.9 KB · Views: 14

Huyu mwanamke ni mpumbavu sana. Atauaje mume wake kwa sababu ya utamu wakati wagawa utamu tumejaa tele mitaani?
 
Back
Top Bottom