Pax Vobiscum
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 450
- 757
Kwanza tunashukuru Serikali kwa kutuletea daraja la muda kwa wakazi wa kata ya Mngeta, limetusaidia Sana katika kuepukana na adha ya mto Mngeta hasa hasa Tatizo la Mamba.
Hivi karibuni kulifanyika ukabati wa korongo linalojulikana Kama "Madandoni" ktk ukarabati huo wajengaji waliinua tuta kubwa na kufukia makaravati matatu ambayo husaidia kupitisha maji toka upande mmoja kwenda mwingine.
Juzi kuamkia Jana yametokea mafuriko makubwa yaliyoleta madhara makubwa Sana;
1) kuvunjika kwa lile daraja
Hii inanesabishwa na maji kushindwa kupata njia sahihi ya kupita baada ya makaravati matatu Yale kufukiwa hivyo kumpelekea kutafuta njia mbadala na pia kubeba magogo makubwa Hadi kuvunja nguzo za daraja.
2) Kuharibika kwa korongo la Madandoni
Hii imesababishwa na uzembe wa mafundi waliojenga lile tuta kubwa, maji yapojaa yakakosa njia yakaoasua barabara kwenye yale Yale makaravati yake matatu ya Asili,
3) mafuriko mashambani
Kwa kawaida mwezi 12 huwa hauna mafuriko lakini kutokana na uzembe wa wahandisi imepelekea kuleta mafuriko mashambani, watu walishapanda mpunga hivyo wamepata hasara kubwa Sana.
4) kukatika kwa mawasiliano ya miundombinu
Barabara hii inahudumia maelfu wa watu vijiji vingi Sana Mgudeni, Isago, mkangawalo, Ilole, Itongowa, Mngeta, mchombe, Lukolongo n.k kote hutumia daraja hili, kwa Sasa Hali Ni mbaya na Ni ngumu kupitika.
MAOMBI
~ Tunaomba Serikali itusaidie kwa haraka Sana kutatua hii changamoto.
~ Mkuu wa wilaya hatuna (wilaya ya Mlimba), tuna mkurugenzi tu, mbunge Kunambi, Diwani, ofisi ya Tarura, Ofisi ya Waziri mkuu (kitengo Cha maafa) n.k tunaomba msaada wenu haraka ili kutusaidia kupata ufumbuzi wa daraja na lile korongo la Madandoni.
~ Tunaelekea msimu wa mvua kubwa na masika wananchi tutataabika Sana, Mto Mngeta mamba wengi Sana kwa Sasa Ni hatari kubwa iko mbele yetu.
~ Tunaomba Sana hatua za haraka zifanyike kutusaidia wananchi.
Ushauri
~ Tunaomba Serikali isaidie kusimamia mazingira vizuri, watu wanalima Hadi mtoni hii inapelekea kina Cha mto kupungua na kusababisha mafuriko.
Walau watu wangeacha kulima mita 20 Hadi 30 tu nje ya mita 60 zile za sheria ya mazingira ya 2004.
Naambatanisha picha.
Hii ni picha ya lile korongo linalojulikana Kama Madandoni baada ya kuharibika.
Update
Leo asubuhi daraja limekatika loteee katikati, hakuna mawasiliano kabisa!