DOKEZO Morogoro: Kuharibika kwa daraja la miti la milioni 31

DOKEZO Morogoro: Kuharibika kwa daraja la miti la milioni 31

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Update!!
Leo asubuhi daraja limekatika loteee katikati,
Hakuna mawasiliano kabisaView attachment 2463009View attachment 2463010View attachment 2463011

Komaeni na viongozi wenu wanaoleta maigizo kwa wananchi, mlimba, mgeta, ifakara kote huko kuna uzalishaji mkubwa wa mazao ikiwamo mpunga mwingi ambao unaliwa Uganda na Sudani kusini na mapato wanakusanya lakini unajenga daraja la miti kua la muda na hauna plan yoyote kwa muda mfupi, ndio maana tunasema moro ni shamba la bibi lisilo na viongozi
 
Aina ya viongozi wao ni akina kalogeresi, shabiby, aboody hawa walijistation moro kwa kilimo na kuua tembo, matajiri kama superstar wanatokea huko, viongozi wao wengine ni marehemu mkulo, kabudi, amatus liyumba unaweza kuona hao hawana chembe ya msaada na kwao
 
View attachment 2463055

Kwanza tunashukuru Serikali kwa kutuletea daraja la muda kwa wakazi wa kata ya Mngeta, limetusaidia Sana katika kuepukana na adha ya mto Mngeta hasa hasa Tatizo la Mamba.

Hivi karibuni kulifanyika ukabati wa korongo linalojulikana Kama "Madandoni" ktk ukarabati huo wajengaji waliinua tuta kubwa na kufukia makaravati matatu ambayo husaidia kupitisha maji toka upande mmoja kwenda mwingine.

Juzi kuamkia Jana yametokea mafuriko makubwa yaliyoleta madhara makubwa Sana;

1) kuvunjika kwa lile daraja
Hii inanesabishwa na maji kushindwa kupata njia sahihi ya kupita baada ya makaravati matatu Yale kufukiwa hivyo kumpelekea kutafuta njia mbadala na pia kubeba magogo makubwa Hadi kuvunja nguzo za daraja.

2) Kuharibika kwa korongo la Madandoni
Hii imesababishwa na uzembe wa mafundi waliojenga lile tuta kubwa, maji yapojaa yakakosa njia yakaoasua barabara kwenye yale Yale makaravati yake matatu ya Asili,

3) mafuriko mashambani
Kwa kawaida mwezi 12 huwa hauna mafuriko lakini kutokana na uzembe wa wahandisi imepelekea kuleta mafuriko mashambani, watu walishapanda mpunga hivyo wamepata hasara kubwa Sana.

4) kukatika kwa mawasiliano ya miundombinu
Barabara hii inahudumia maelfu wa watu vijiji vingi Sana Mgudeni, Isago, mkangawalo, Ilole, Itongowa, Mngeta, mchombe, Lukolongo n.k kote hutumia daraja hili, kwa Sasa Hali Ni mbaya na Ni ngumu kupitika.

MAOMBI
~ Tunaomba Serikali itusaidie kwa haraka Sana kutatua hii changamoto.

~ Mkuu wa wilaya hatuna (wilaya ya Mlimba), tuna mkurugenzi tu, mbunge Kunambi, Diwani, ofisi ya Tarura, Ofisi ya Waziri mkuu (kitengo Cha maafa) n.k tunaomba msaada wenu haraka ili kutusaidia kupata ufumbuzi wa daraja na lile korongo la Madandoni.

~ Tunaelekea msimu wa mvua kubwa na masika wananchi tutataabika Sana, Mto Mngeta mamba wengi Sana kwa Sasa Ni hatari kubwa iko mbele yetu.

~ Tunaomba Sana hatua za haraka zifanyike kutusaidia wananchi.

Ushauri
~ Tunaomba Serikali isaidie kusimamia mazingira vizuri, watu wanalima Hadi mtoni hii inapelekea kina Cha mto kupungua na kusababisha mafuriko.

Walau watu wangeacha kulima mita 20 Hadi 30 tu nje ya mita 60 zile za sheria ya mazingira ya 2004.

Naambatanisha picha.
View attachment 2463059

View attachment 2462997

View attachment 2463051
Hii ni picha ya lile korongo linalojulikana Kama Madandoni baada ya kuharibika.

Update
Leo asubuhi daraja limekatika loteee katikati, hakuna mawasiliano kabisa!
View attachment 2463056
Poleni sana.
Haya mambo ya kutengeneza vya muda mfupi yataligharimu taifa.
Bado kwenye mabehewa ya kukarabatiwa, tutegemee gharama za ukarabati kuwa kubwa zaidi.

Kwanini haraka haraka? Wanamfurahisha nani? Na sio hilo tu, vipo vingi tu awamu hii vimefanywa haraka haraka pasipo hat ubora!
Nchi ngumu sana hii!
 
Hapo ni pafupi sana wajenge daraja la magogo mfano zile nguzo kubwa za Tanesco unaziunganisha mbili hazihitaji sapoti kati hata gari tani 5 inapita.
 
Uhandisi hausomewi, hilo nina uhakika nalo; unachosomea ni lugha ya kihandishi ili muweze kuelewana baina ya wahandisi, basi. Kama wewe si mhandisi, huwezi kuwa mhandisi, hata ukasome China.
 
Hayo maeneo nayafahamu fika! nimeishi huko kwa miaka mingi. Kiufupi serikali ya ccm imewekeza sana kwenye siasa, kuliko kwenye mambo ya msingi.
Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi zina umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa nchi yetu! Lakini linapokuja suala la miundombinu ya barabara, hali ni mbaya kupitiliza.

Hayo maeneo yanazalisha sana mpunga, miwa, ndizi! kuna samaki wa mto Kilombero, nk. Lakini barabara zake ni mbovu mpaka basi.

Hizo Wilaya tatu zinafanana sana na Wilaya za Mufindi na Kilolo Mkoani Iringa. Nako mambo ni hayo hayo. Kuna uzalishaji mkubwa wa mazao yatokanayo na miti, pamoja na chai! Lakini barabara zake hazipitiki wakati wa masika.

Cha kujiuliza; hii serikali haina pesa za kujenga barabara za lami kwenye haya maeneo muhimu kwa uchumi wa nchi? Hivi hawaoni wakijenga barabara kwenye hayo maeneo, bidhaa muhimu kama chakula, mbao, nk. Zitawafikia walaji kwa gharama nafuu?
Hizo hela mnazochezea kununulia magari ya kifahari, kwa nini msijenge barabara za uhakika ili kuwaondolea wananchi hizi kero za miaka nenda?
 
Viongozi wao ni akina babu tale
Babu Tale yuko Morogoro Kusini! Mbali kabisa kutoka hayo maeneo ya Mlimba, Mngeta, Chita, Mbingu, nk. Mbunge wa hilo eneo alikuwa ni kijana wa magu anayeitwa Godwin Kunambi. Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma enzi za utawala wa awamu ya 5.

Na ikumbukwe amechukua hiyo nafasi kutoka kwa Suzan Kiwanga wa Chadema, aliyeshinda ubunge wa hilo Jimbo la Mlimba kwa tiketi ya Chadema mwaka 2015.
 
"Na hilo nalo mkalishughulikie"
Kishakusema hayo akapanda ndege akaenda zake.
 
Morogoro hamjawahi kupata viongozi wanaowasaidia kwa dhati ndio maana mnakila kitu lakini maendeleo yenu mko nyuma, anzia wabunge, wakuu wa wilaya, na DED, na kadhalika wengi wakata viuno na mipasho na sio watendaji
Wilaya ya Moro mjini ndo wilaya inao ongoza kwa maendeleo kuliko wilaya zote tz
 
Ilitakiwa kuanzia mkuu wa mkoa mpaka kiongozi wa chini aliyehusika na ujenzi huo wachukuliwe hatua. Hela ya mlipakodi imepotea bure
 
Hayo maeneo nayafahamu fika! nimeishi huko kwa miaka mingi. Kiufupi serikali ya ccm imewekeza sana kwenye siasa, kuliko kwenye mambo ya msingi.
Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi zina umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa nchi yetu! Lakini linapokuja suala la miundombinu ya barabara, hali ni mbaya kupitiliza.

Hayo maeneo yanazalisha sana mpunga, miwa, ndizi! kuna samaki wa mto Kilombero, nk. Lakini barabara zake ni mbovu mpaka basi.

Hizo Wilaya tatu zinafanana sana na Wilaya za Mufindi na Kilolo Mkoani Iringa. Nako mambo ni hayo hayo. Kuna uzalishaji mkubwa wa mazao yatokanayo na miti, pamoja na chai! Lakini barabara zake hazipitiki wakati wa masika.

Cha kujiuliza; hii serikali haina pesa za kujenga barabara za lami kwenye haya maeneo muhimu kwa uchumi wa nchi? Hivi hawaoni wakijenga barabara kwenye hayo maeneo, bidhaa muhimu kama chakula, mbao, nk. Zitawafikia walaji kwa gharama nafuu?
Hizo hela mnazochezea kununulia magari ya kifahari, kwa nini msijenge barabara za uhakika ili kuwaondolea wananchi hizi kero za miaka nenda?
Inasikitisha Sana mkuu, huku kuanzia mbunge wote sifuri tu, CCM Ni janga kubwa
 
Back
Top Bottom