magnifico
JF-Expert Member
- Jan 14, 2013
- 11,075
- 24,634
Mungu katuumba na akili na utashi kusudi tuweze kukabiliana na changamato tunazokutana nayo.Hawa manabii feki wameharibu sana watu, hususani akina mama. Kuna mama mmoja aliugua brucellosis kama ilivyo bainishwa na madaktari, lakini ndg wa huyo mama hususani mama yake mzazi na dada yake mgonjwa walikataa katakata huyo mama kutibiwa hospital wakadai wampeleke kwa Mwamposa ili aombewe apone. Kidogo huyo mama akate kamba. Bahati nzuri mgonjwa alijiongeza na kurudi kuendelea na dawa za hospital, hadi sasa ni mzima wa afya.
Unajua kabisa haya ni Malaria na dawa zake unazijua na pesa mfukoni unazo hutaki kutumia unataka kuombewa. Kama sio kumjaribu Mungu wako ni nini?